Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kwa kipindi kirefu tangu Ukraine iwe taifa huru kutoka USSR ilikuwa ni nchi yenye misukosuko mingi ya kisiasa, rushwa iliyokithiri, jeshi na serikali zilizo dhaifu sana. Mwaka 2014 ilifikia katika kilele cha matatizo ya kisiasa pale Rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych aliyekuwa Pro Russia alipokaata kusaini mkataba wa kibiashara na Umoja wa Ulaya(EU)uliodhinishwa na bunge la Ukraine. Wananchi waliandamana nchi nzima hadi akaondoka madarakani(Maidana Revolution) na kukimbilia Urusi.

Urusi ilikasirishwa sana kuondolewa kibaraka wao kupitia mapinduzi ya kiraia ndipo Putin akatuma jeshi lake kuichukua Crimea na huko Luhansk na Donetsk waasi waliopandikizwa na Russia wakajitangazia uhuru. Serikali na jeshi la Ukraine havikuweza kufanya resistance yoyote ya maana kipindi hicho kwa sababu ya udhaifu. US akaingia kati kuipa msaada Serikali na jeshi la Ukraine ili nchi hiyo isisambaratike, Serikali ikawezeshwa kupambana na ufisadi, jeshi likapewa mafunzo, fedha na silaha. Ukraine ikawa na serikali kweli inayoweza kudhibiti nchi na utawala wa sheria. Uchaguzi wa mwaka 2019 uliomuinguza Zelenskyy ukafanyika vizuri bila dhoruba, vurugu au malalamiko kama ilivyozoeleka kwenye chaguzi za nyuma.

US ns Ulaya wakazidisha misaada ya fedha, mafunzo ya utaalamu kwa serikali na vyombo vya ulinzi vya Ukraine, pia Ukraine ikazidi kusogea katika ulimwengu wa magharibi ikijitahidi kupiga hatua zote ili ifanikiwe kukidhi vigezo vya kujiunga EU na NATO miaka ya baadaye, 2022 Putin kaivamia na sasa iko vitani ikitetea Uhuru wake. Laiti kama Putin angeivamia Ukraine 2014 kurudi nyuma huu uvamizi wake ungedumu wiki moja tu na angeshewaka kibaraka wake Kyiv.

Hii ni kwa ufupi sana.
Nafafanulie vizuri ndugu yangu

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] wazee wa ARV na Vyoo vya kushushia mzigo.
 
108th battalion of Ukrainian army has been completely defeated and many soldiers captured, only 30 out of 350 service men remain in the unit. High missile precision strike have destroyed 4 command posts at Kharkov-1 and Kharkov-2 territorial defense battalion near Kharkov as well as a training base of mercenaries deployed near Nikolayev.
 
Akisaidia mnanuna na kulaani, asiposaidia mnakereka pia, sasa mnataka nini?!
Hapo alikuwa na maslahi,mbona hajaisaidia Sudan kusini,DRC,Mali nk mpaka sasa? Wakati Rwanda wanauana alikuwa wapi?
 
Dah...imeniuma Sana Patrice Lumumba alipozikwa leo rasmi ...na kilichozikwa ni jino lake moja tu lililorudishwa 'majuzi' tu kutoka Ubelgiji...mwili wa Lumumba aliyeuawa kikatili na wasaliti kwa njama za wazungu uliyeyushwa kwenye Sulphuric acid ( nadhani ilikuwa ni oleum) miaka hiyo ya 1960 mwanzoni...wazungu ni washenzi kabisa...
 
Sawa...kwa hiyo?!?!
 
Ndo maana unaambiwa huna hoja, badala ya kulinganisha BRICS na G7 wewe unalinganisha BRICS na EU. Are you real serious?
Jana nilikushauri kabla hujajibu hoja tuliza akili kwanza usikurupuke kujibu, hakuna mtu anaekukimbiza hapa hadi ushindwe kuelewa hoja.


EU ni Muunganiko wa nchi baadhi za bara la ulaya pekee. BRICS&G7 ni muunganiko wa nchi kutoka mabara tofauti.

Sasa naomba nikuulize maswali kutoka kwenye vihoja vyako ulivyo andika.
☆G7 members wanatumia pesa moja kama EU?

☆G7 members wana mashindano ya mpira ya pamoja kama UEFA?

☆G7 member countries wana free movement kama EU?
 
Wakati Rwanda wanachinjana wenye pua ndefu na fupi zilizobonyea US alikaa pembeni akitizama tu kwa sababu ndio kwanza ilikuwa imepita miaka minne tu tangu wanajeshi wake 18 na wengine wauwawe na kudhalilishwa na wanamgambo wa Mogadishu huku sehemu kubwa ya watu kama nyie wakishangalia na kusema akome kuingilia mambo ya watu wengine.Clinton alifanya maamuzi ya kisiasa zaidi kwa kumbukumbu ya Somalia, ila alikiri baadaye ilikuwa ni kosa US kutoingilia Rwanda

Pia US walikuwa hawaelewei hasa ni kitu gani kilikuwa kinafanya watu weusi wanaowaona wanafanana kila kitu wanachinjana wenyewe kwa wenyewe.

US au EU kutoingilia Rwanda ni kadi turufu sana pia kwa dikteta Kagame kila mara anapoulizwa kuhusu haki za binadamu na utawala bora kwani huwa anajigamba na kuuliza walikuwa wapi wakati alipomaliza mauji ya kimbari bila msaada wa nje(japo kuna tuhuma yeye mwenyewe ni mojawapo ya watu waliohusika kusababisha!.)
Ni mchanganyiko wa hovyo sana.
Hapo alikuwa na maslahi,mbona hajaisaidia Sudan kusini,DRC,Mali nk mpaka sasa? Wakati Rwanda wanauana alikuwa wapi?
 
Da ila wewe jamaa hizi sio akili zako,hizi ni akili za baba Yako kabisa.
Wewe mtoto mdogo unawezaje kuwa na akili za kikubwa namna hii?
Hahah! Mkuu siyo kwamba nina akili nyingi sana ni namna tu ambavyo najitahidi kukitumia kichwa ipasavyo nasiyo kukitumia kama kifaa cha kuhifadhia meno na kufugia nywele.

All in all, shukrani sana mkuu kwa kunie heshimisha mimi na baba yangu, naamini uwepo wetu humu na hoja zetu kwa pamoja ndo zinatufanya tuendelee kupanuka ubongo siku hadi siku, bila kujali umri wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…