LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
kwa hadi sasa vita ya ukraine na urusi , marekani na member wa nato washasurrender ina maana ukraine inamalizwa soon,kinachosubiliwa endapo akimaliza kwa ukraine je atashambulia member kamili wa nato walioko karibu na urusi,na hapo ndo nadhani vita kamili itaibuka kwa sababu mkataba wa NATO unasema mmoja akivamiwa lazima wengine wampe sapoti ya kijeshi
Hii chai ulisahahu kuweka sukari,imekuwa chungu mno Mkuu.
 
So ile operation ya masaa 24 sasa hivi itakuwa ya mwezi mzima kwakuwa Kyv ina watu wengi si ndiyo Mkuu.
Mkuu nani alisema itakuwa operation ya masaa 24?? Weka hapa hiyo statement. Nilivyomsikia Putin alisema wataenda kulinda watu pale DONBAS Region, hiyo ndio operation yao maalum.
 
Kama ni hivyo kilichokuwa kinawafanya mseme Russia anakwenda kufanya operation maalum tu ndani ya masaa 24 anamaliza mchezo Ukraine ni kipi sasa (japokuwa unaweza kuwa si wewe but Pro Russia wengi humu ndiyo walikuwa wanatupigia makelele hayo ) kama mnalijua hilo la uwezo wa Ukraine kijeshi pia.Tunajua ni aibu the so called Super Power kijeshi kupewa upinzani mkali na Underdog Ukraine,tunawaelewa mnavyojaribu kumsitiri mtu mzima aliyevuliwa nguo na mtoto

Shida yako unataka uone kyiv iwe majivu? [emoji28]
 
Watu wamechafukwa
Screenshot_20220302-112214.png
 
Hapa ndugu zetu warusi itagharimu maisha vijana wao ambao wako front, humu ndani wachangiaji wengi hawaijui principles za medani zaidi yakuwa na mahaba kwa Putin na jeshi lake. Military supply kwenye uwanja wa medani ni kitu muhimu sana ambapo mara nyingi unafanikiwa kama ukipata air superiority yaana kuharibu air defence system ya adui yako, urusi ilijua itamaliza vita mapema kumbe Ukraine sio wezembe wamekata supplies kwa kuharibu barabara kwenye baadhi ya maeneo, Kuna baadhi ya convoys zimeshambuliwa na kuharibiwa vibaya, vijana wa Ukraine wengina wanatumia guerrilla warfare strategy kuharibu military hardware za urusi ndio maana urusi wameanza kurusha makombora kutokea black sea kama fire support
IKo hiviii, Urusi kwenye vita hii haiko peke yake. Nchi zote zenye ugomvi na mataifa ya magharibu ni wadau muhimu kwenye vita hii. Nchi zote ambazo zinanyonywa na nchi za magharibi ni wadau kwenye vita hii, nchi zote zilizowahi kutawaliwa na mataifa yanayounda NATO ni wadau kwenye vita hii.

Ikumbukwe kuwa kinachotafutwa hapa ambacho Urusi inakipigania ni kuzuia Marekani na mataifa yanayounda NATO kuweza kuwa na uwezo wa kujiamulia chochote kwenye dunia hii. Anaeona Urusi anakosea ni nchi za NATO na Marekani wenye ajenda yao ya muda mrefu na ya kudumu. Nchi za Kiafrika lazima zimuunge mkono Urusi na nafahamu zinafanya hivyo kimyakimya kuepuka kunyimwa misaada na mabeberu.
 
Duh, nimekula ban huko twitter. Yaan ukicomment vibaya kuhusu UKRAINE unakula mua.
Ikiwezekana wakupe permanent ban kabisa 🙂. Nenda kwa Putin mkaanzishe Twitter yenu huko mcomment kwa uhuru,au mambo ya maendeleo hamna habari nayo mko busy na masilaha ya Nyuklia peke yake,halafu mnataka kuja kutumia uvumbuzi wa wenzenu kuwatole povu.
 
Hawezi!

Kwa sababu kila mtu anajua consequences zitakazotokea. Njia pekee ambayo ni salama ni Ukraine akubaliane na masharti ya Mrusi, awe neutral.
Akiwa neutral ndo anavamiwa pale Mrusi akijisikia kuivamia Ukraine
 
Propaganda zimewaathiri sana watu humu. Utumwa wa kifikra utumwa mbaya mno!
Wakati mdogo nilkuwa naamini kabisa Iddi Amin ana kichwa cha nyoka usiku na pia anachinja watoto zake anaweka kwenye fridge na hata mkewe akimtamani anamchinja na kumla. Joka. kuja kuwa mkubwa na kujuwa ukweli kumbe jamaa alikuwa na watu wengi tu wanampenda.
 
Sasa mkuu unaamini ulikuwa unatoa hoja nzito nzito za kueleweka bado wakapiga kofuli?
Ndio, unajua ukichangia mada kwa kiingereza inakuwa rahisi kuwa detected. Mi nilikuwa nadeal na CNN, BBC, REUTERS nk wakipost kitu na kama nimeona wazi hii ni propaganda huwa nashindilia comment huku nikimaalizia kuunga mkono URUSI wazidi kuifumua UKRAINE.
 
Kuna jamaa nipo naye hapa kijiweni ametujulisha habari za ndani ndani kabisa , Putin anafunga mahesabu Ukraine wiki hii anaendelea mbele kuichukua na Finland🐒
Muongezee Birika la kahawa mkuu,mpatie na kashata sinia zima awe anashushia,Bill yote kwangu 😂
 
Kama ni hivyo kilichokuwa kinawafanya mseme Russia anakwenda kufanya operation maalum tu ndani ya masaa 24 anamaliza mchezo Ukraine ni kipi sasa (japokuwa unaweza kuwa si wewe but Pro Russia wengi humu ndiyo walikuwa wanatupigia makelele hayo ) kama mnalijua hilo la uwezo wa Ukraine kijeshi pia.Tunajua ni aibu the so called Super Power kijeshi kupewa upinzani mkali na Underdog Ukraine,tunawaelewa mnavyojaribu kumsitiri mtu mzima aliyevuliwa nguo na mtoto

Mzee tatizo umekuja na ushabiki mkubwa na ushabiki unatabia ya kuondoa reasoning, hebu jiulize kwa nini Russia haikutumia nguvu sana mwanzoni kama inavyotumia sasa? Umeskia upinzani wowote kwa mashambulizi ya jana?

Leo camera zote zinaonyesha maafa tu yaliyotokea jana na hakuna resistance yoyote ya jeshi la Ukraine. Ukraine walifanya huo upinzani pale ambapo uvamizi haukua mkubwa ila kwa sasa Russia wamekua serious na operation yao hamna upinzani wowote Ukraine wenyewe wako kimya kila sehemu kunashambuliwa.

Hiyo akaunti ya twitter ilikua inajaza propanganda za Ukraine kuonyesha kwamba Russia wamezidiwa leo wenyewe wanatangaza sehemu zinazoshambuliwa na kuwaasa watu watafute nearest shelter.

Kwa mtazamo wako nguvu ya kijeshi kama hii ingetumika kuanzia mwanzo wa vita hii unafikiri leo Ukraine ingekua hatua gani? Wanajeshi wa Ukraine wako wapi kuonyesha upinzani waliokua wanaounyesha juzi?


View attachment 2136135View attachment 2136136
 

Attachments

  • Screenshot_20220302-104656.jpg
    Screenshot_20220302-104656.jpg
    57.1 KB · Views: 13
Sasa haya ni mawazo yako!
Wachambuzi wanasema Russia bado wanawahitaji raia wa Ukraine, ile nchi bado ipo na ni jirani yao na itabakia kuwa hivyo. Hakutakuwa na sababu ya kufanya uvamizi mkubwa kama alivyofanya Syria. Akifanya uvamizi wa namna hiyo atatengeneza adui mwengine mkubwa wa kizazi na kizazi ambaye ni jirani na ni mazingira hatari kwa usalama wa nchi ya Russia.

Kimkakati inambidi adili na wanajeshi tu baada ya amiri jeshi mkuu wa nchi ya Ukraine kukataa makubaliano waliyoyapendekeza. Na ndiyo maana akaanza na kupunguza nguvu ya jeshi la Ukraine kwa kushambulia base za kijeshi na maghala ya kuhifadhia silaha pamoja na viwanda vinavyojihusisha na utengenezaji wa silaha. Lengo no kupunguza nguvu za jeshi la Ukraine.

Operation inayofuata ndiyo hiyo ambayo anayoifanya sasa hivi na ni operation ngumu ambayo ni urban warfare. Ikiwa ni kuiondoa serikali ambayo kwake anaiona ni hatarishi. Kwa kuzuia uharibifu mkubwa wachambuzi wanasema ameingia na silaha za nyuma si za kisasa.

Urban warfare ni ngumu na ugumu wa hapa si kwamba Russia hana uzoefu. Ugumu wa hapa ni mnapambana kwenye makazi ya watu ambao ni raia, ambao sheria za kivita zinawalinda. Shambulio lolote dhidi yao ni uhalifu wa kivita kwa sababu umeshambulia wasiyostahiki. Na huu ni mtego kwa Russia, majeshi ya Ukraine yanajificha kwenye makazi/majengo ya makazi ya raia.

Kuna suala hapa umelisahau. Russia lengo la hii vita ni kulinda usalama wa nchi yake. Sote tunafahamu NATO ikiwa mlangoni kwake ni hatari. Ukraine pia inakuwa kijeshi ikiwa NATO na ikijijengea na uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia hatoweza kumdhibiti. NATO wanalijua hili na wanajua kuwa Ukraine ni kete muhimu dhidi ya Russia.

Naam; Ukraine ni nchi huru ina wajibu wa kufanya maamuzi yake lakini ni hatari kufanya maamuzi yatakayo hatarisha usalama wa nchi jirani yako. Russia anachofanya ni kumdhibiti Ukraine mapema. Ikiwa Russia mkakati huu utafeli wachambuzi wanasema itamlazimu alazimishe mazingira. Nayo ni kutunisha msuli wake. Akifanya hivyo maangamivu ya Syria miji kuwa gofu yatahamia Ukraine. Na Ukraine itaumia.

Russia inacheza mahesabu hapa! ni mahesabu yanayohitaji umakini wa hali ya juu. Atakayeumia zaidi ni Ukraine ikiwa akikaza msuli.
NATO iwe mara ngap mlangoni mwa Russia , Russia anatumia hiyo iwe sababu ya yy kuizuia Ukraine kujiunga NATO ila in reality ana sababu zake zakiuchumi na sio sababu za kiusalama kama anavyojigamba hadharani , Latvia na Estonia ji majirani wa Russia ila pia ni members wa NATO ila Russia did nothing to stop them from joining NATO
 
⚡️ Ukrainian delegation yet to arrive for negotiations with Russia (Sputnik citing source)

Negotiations between Russia and Ukraine will reportedly still take place - while the time has not yet been determined, it may be Wednesday evening. (RIA Novosti)
 
Back
Top Bottom