Mimi
ninachofahamu kuhusu ukweli wa hii vita (operesheni ya kijeshi ) ni uchumi. Karibu
vita vyote duniani vimehusika kwa
namna moja au nyingine kuhusiana na uchumi.Siku zote shughuli za kiuchumi hufanyika katika
ardhini kwa sehemu kubwa.
Shughuli nyingi za kiuchumi hutumia nishati kwa sehemu kubwa sana kama siyo zote.Kwa maana hiyo
msingi mkuu wa shughuli za kiuchumi ni nishati ambayo kwa sehemu
kubwa inapatikana kwenye ardhi.
Vita kubwa kwa sehemu kubwa zimehusiana na
umilikaji na utawaliwaji wa nishati.Ukimiliki na kuitawala nishati
utakuwa na sauti na nguvu kubwa kwenye uchumi ambayo itakupa vilevile
nguvu ya kisiasa.
Russia (Urusi) ni nchi
iliyojaaliwa na kubarikiwa kwa kumiliki na kutawala rasilimali za asili zenye kuhusisha nishati.Hali hii imeifanya
kuwa na sauti na nguvu kwenye bara la ulaya kama siyo duniani kwa ujumla.
Wewe mwenyewe utakuwa
shahidi kwa kinachoendelea sasa hivi duniani kuhusu
nishati.
Hali hii
iliwakera na kuwauma watu wa Magharibi wakiongozwa na
kiranja mkuu Marekani.Wamagharibi kwa miaka mingi walitamani huu
utajiri wa rasilimali waumiliki na kuutawala wao peke yao.
Mikakati ilipangwa na kupangwa lakini
ikashindikana!!!
Wakajiuliza
karibu nishati ya dunia nzima tunaimiliki sisi kwa nini hii itushinde???Nishati ya Mashariki ya kati,Afrika,Amerika kwa asilimia kubwa
tunaimiliki na kuitawala sisi huyu ni nani mpaka atubabaishe na kutupora sauti na nguvu yetu kwenye nishati??Zikafanyika tafiti na tafiti kuhusu nishati huko huko Ulaya.
Tafiti zikaonyesha kuwa upande wa
Mashariki wa Ukraine kuna hazina kubwa sana ya rasilimali za asili ambazo kwa
asilimia kubwa zinahusiana na nishati!!Wamagharibi wakafurahi sana !!
Tukiibeba Ukraine yote basi Urusi
atapoteza sauti na nguvu (soko) kwenye nishati
kwao Wamagharibi na
dunia nzima kwa ujumla.!!!
Warusi wakapata
taarifa (ujasusi) kuwa nguvu yao kuhusu nishati inaenda
kupotea kutokana na
ugunduzi huu!!! Wakati wanatafakari
kibaraka wao waliomuweka hapo Ukraine akaondolewa kwa
maandamano ya wanaotaka demokrasia!!
Baada ya Wamagharibi kupeleka kete ya kwanza, warusi nao wakapeleka
kete yao ambayo ni kulibeba jimbo mojawapo ndani ya Ukraine.!!!Wamagharibi wakajua kuwa
ngoma imeanza na inabidi waicheze!!
Tunaichezaje?? Piga vikwazo na
tulitengeneze na kuliboresha jeshi la Ukraine liwe la
kisasa halafu
tujiandae na kinachofuata!!!
Warusi wakaunda
vikundi vya kijeshi kisha wakapeleka
kete nyingine ambayo ni kuyabeba majimbo yote yanayohusiana na huu ugunduzi wa rasilimali!!! Hahah!!! Zikaanza kupigwa baina ya
vikundi vya Kirusi dhidi ya
vikundi vya Kimagharibi.Vikundi vya kirusi vikaonekana
kuzidiwa na Ukraine
ikafanikiwa kuyarudisha majimbo yaliyogunduliwa hizo rasilimali!!!!
Warusi
wakajiuliza na kutafakari itakuaje kuhusu
hatima yao mara baada ya haya majimbo kuchukuliwa!!! Wakaja na jibu moja
'kuwa tutakuwa hatuna tena nguvu na sauti'.!!!! Nini kifanyike?? Tulitumia vikundi vikafeli sasa ni lazima jeshi liingie!!!
Sababu ipi zipi zitakuwa na mashiko???
- Tunajilinda dhidi ya Nato.
- Tunalinda maisha ya jamii za Kirusi zilizo hatarini huko Ukraine.
- Kuna Wanazi huko Ukraine.
- Kuna maabara ya silaha za kikemikali huko Ukraine.
Wakati huhuo vyombo vya
kijasusi vya Kimagharibi
vikapata harufu ya nini kinachofuata!!!
Ikatangazwa
operesheni(vita??) ya kuipunguza nguvu za kijeshi ukraine pamoja na kuwaondoa Wanazi
(Demilitarization and Denazification)!!!!!Hahaha!!!!
Swali: Nani ataibuka mshindi kati ya anayetetea sauti na nguvu ya nishati (Urusi) na wanaotaka kuipora hiyo sauti na nguvu(Wamagharibi)??? Muda utaamua!!!!
Nb: Unaweza kuona na kuhisi vita ni siasa au dini ndiyo inasababisha lakini ukweli ni rasilimali asili kwa kiasi kikubwa sana ndiyo msingi mkuu na siasa au dini ndiyo hutumika kama kichocheo.
Ni mtazamo wangu binafsi!!!!