Wakajiuliza karibu nishati ya dunia nzima tunaimiliki sisi kwa nini hii itushinde???Nishati ya Mashariki ya kati,Afrika,Amerika kwa asilimia kubwa tunaimiliki na kuitawala sisi huyu ni nani mpaka atubabaishe na kutupora sauti na nguvu yetu kwenye nishati??Zikafanyika tafiti na tafiti kuhusu nishati huko huko Ulaya.
Mjomba unafaham kama Venezuela na Iran, hizi nchi 2 tu kwa pamoja wana miliki world share ya zaidi ya 27% ya Oil reserves duniani? Ukilinganisha vs Russia mwenye reserves ya share ya below 5% au United state mwenye 2.1%?
Vile vile upande wa Natural Gas, Top three countries. Russia 24% Share, Iran again 17.3% na Qatar 12.5%. Ondoa Qatar baki na hizo mbili Russia na Iran nchi mbili ambazo hazina influences ya west pa1 ni over 41%
Sasa unaposema almost zote una maana ipi? Point yako hapo imejikita wapi? Uzalishaji au reserves? Na kama ni uzalishaji vipi kuhusu vinavyotakiwa kuzalishwa? Yes am asking kuhusu reserves?
Tafiti zikaonyesha kuwa upande wa Mashariki wa Ukraine kuna hazina kubwa sana ya rasilimali za asili ambazo kwa asilimia kubwa zinahusiana na nishati!!Wamagharibi wakafurahi sana !! Tukiibeba Ukraine yote basi Urusi atapoteza sauti na nguvu (soko) kwenye nishati kwao Wamagharibi na dunia nzima kwa ujumla.!!!
Kwenye hizo tafiti uliangalia kiasi kilichogunduliwa? Let me help you with some data. Kiasi kilichopo kilichopo Ukraine Upande wa natural gas ni 39 millions MMcf, ambazo ni 0.6% ya world share. Na upande wa Oil reserves ni 395 millions barrels ambazo pia ni kama 0.024%
In comparison, Russia ana Natural gas reserve mara 40 zaidi ya zile zilizopo Ukraine, Russia ana Oil reserves mara 195 zaidi ya zile zilizogunduliwa hapo Ukraine.
Kwa hizo data vipi unahisi hayo madai unayo yaita ukweli ni sahihi? Kama tu kiasi kwamba kile kilichogunduliwa hakikidhi mahitaji ya Ukraine yenyewe vipi for that case unafikiri wanaweza kukidhi mahitaji ya nchi zingine?
Vikundi vya kirusi vikaonekana kuzidiwa na Ukraine ikafanikiwa kuyarudisha majimbo yaliyogunduliwa hizo rasilimali!!!!
Unaweza kutusaidia majina ya hayo majimbo yaliyo rudishwa na Ukraine yenye hizo rasilimali mjomba?
Tulitumia vikundi vikafeli sasa ni lazima jeshi liingie!!!
Sababu ipi zipi zitakuwa na mashiko???
- Tunajilinda dhidi ya Nato.
- Tunalinda maisha ya jamii za Kirusi zilizo hatarini huko Ukraine.
- Kuna Wanazi huko Ukraine.
- Kuna maabara ya silaha za kikemikali huko Ukraine.
So hapa unajaribu kutuambia kwamba hayo madai yote si ya ukweli bali ni visingizio vya Urusi tu kwenda kuiba Ukraine mali zao?
Kwamba hakuna Nazi, Hakuna wa Ukraine waliokua wanauwawa hapo Donbass, wala hakuna maabara za US hapo Ukraine. Kwamba vyote ni visingizio. Na kitendo cha Pentagon kukiri uwepo wa hizo Labs nao waliteleza, ni Uongo wa Urusi kutaka kuiteka mali ya Ukraine au sio?
Unafikiri kwanini Russia asiende kuibeba Qatar, Saudia Arabia au Iran UAE au kwa Venezuela mbali kutoka kwake. Nchi zote hizo aziweke mikononi ziwe chini yake abaki kujisumbua na Ukraine ambae resorces zilizopo hapo upande wa nishati zote zinasoma figure chini ya 1% ya world share?
Unaweza kuona na kuhisi vita ni siasa au dini ndiyo inasababisha lakini ukweli ni rasilimali asili kwa kiasi kikubwa sana ndiyo msingi mkuu na siasa au dini ndiyo hutumika kama kichocheo.
Kwenye hii kauli yako hapa nusu nakubali na nusu nakupinga, Vita vina sababishwa na siasa pia nakubaliana na wewe kua vita havisababishwi na dini n.k
Unapozungumzia siasa, haziishii kwenye kampeni kushinda uchaguzi. Unapozungumzia siasa unazungumzia power, na ili uwe na power lazima uwe na nyenzo za hizo power.
Hizo nyenzo za power kubwa kabisa ni Pesa na nyingine ni rasilimali. Kwenye uchumi hizi Raw materials ni Primary sector. Hupati Secondary sectors bila kua na Primary sectors. Nina maana ya kua hupati uzalishaji kama hauna malighafi/rasilimali.
Lakini world power system imebase kwenye pesa pekee as a nyenzo of power kuliko rasilimali. Angalia nchi kama Iran, ina resources nyingi mara dufu kuliko bara lolote ulaya. Je Iran ina nguvu kuliko Germany? Kuliko Italy? Kuliko Spain au France au UK?
Mwenye pesa anahitaji rasilimali na mwenye rasilimali anahitaji pesa. Rasilimali ngumu kupatikana but pesa printer zipo na wino wa kutosha. Prrrrr ni mlio mwepesi kusikika kwenye masikio zinapohitajika.
Russia rasilimali anazo lakini anaendelea kuziuza kwa mataifa yanayo mpa vikwazo kwasababu anahitaji pesa. Why pesa? Coz hizo pesa ndio nyenzo kuu ya power katika mfumo mzima wa dunia tulio nayo hivi leo.
Hapa Tz si tuna gesi? Bila pesa tunawezs kuitoa ardhini? Na tukiitoa ardhini kutafuta nini?
Any way kuhusu huo upande wa mashariki mwa Ukraine ndipo kumejaa vile vinavyomtambulisha Ukraine duniani. Issue nzima ya chakula kama ngano shairi n.k ambazo west wamekua wakipiga kelele kila siku kua wanazihitaji. Wala sio issue ya nishati.
Ni mtazamo wangu binafsi!!!!
Yah ni mtazamo wako binafs, upendezeshe uulishe nyama usogelee karibu uhalisia.
Mitazamo ipo mingi kuhusu kile kinacho endelea Ukraine. Hapa a hata mmoja bali nimejikita katika katika "faults" za mtizamo huo ulio nao.
Kesho mwanao amekuwa wa 7 darasani, muulize kwanza kapata wastan upi ulinganishe na top wao uone kama anastahili pongezi au achapwe aongeze juhudi. Kwani anaweza kua kapata wastani wa 10 out of 100 ila kawa wa 7 ihali wa kwanza ana wastani wa 94.
Mimi ni mmoja katika watu tunao amini sana katika number, Huh Numbers never lies na zilizo DATA ndio msingi wa ukweli na silaha ya kutokomeza uongo.