Mkuu
Kuna mchambuzi wa kiroho anasema kuwa Russia ndio waisrael HALISI na wanapigania dhidi ya waisrael feki hao waliopo hapo NCHI ya israel wakiiisapoti NATO na Marekani!!!na eti Russia ambao ni waisrael HALISI watashinda vita eti Mungu you pamoja nao!!!
Kuna ukweli katika Hayo!!!!au ni porojo za kijiweni tu!!?
Mkuu, kama wafahamu waisraeli wapo kila kona duniani ni watu ambao huchukuliwa kuwa ni "special" kwa sababu ya chuki kwao.
Leo wametimiza miaka 80 ya waisareli wapatao 10,000 kukamatwa na polisi wa Ufaransa na kisha kupelekwa kule Auschwitz na kisha kuuawa na askari wa kinazi mauaji yaitwayo "Holocaust".
Yaani kwenye katongoji kitwacho Vichy kalichopo mjini Paris kuliendeshwa msako mkubwa wa kuwatafuta wayahudi na kuwapeleka kwenye stesheni ambayo walipandishwa garimoshi kwenda kuuawa yaitwa Vel' de' Hiv.
Putin alizaliwa mwaka 1952 na kaka zake wawili Albert na Viktor walizaliwa mwaka 1930 na 1940 lakini walikufa kutokana na madhila ya walokuwa wavamizi wa kinazi wa Ujerumani ambao walisababisha kuwepo kwa njaa katika sehemu ya Leningrad.
Kwa mujibu wa historia, wazazi wake Putin walikuwa ni wafanyakazi na baba yake alikuwa askari wa majini kwe ye manowari na mama yake alikuwa akifanya kazi kiwandani.
Bibi yake Putin pia aliuawa wakati wa uvamizi wa majeshi ya kinazi kwenye jimbo la Tver na baba zake wakubwa na wadogo waliuawa wakipigana kwenye vita kuu ya pili ya Dunia.
Hivyo leo Putin akisema kwamba anachukia tabia ya hawa watu wa Zelenski walokuwa wakifanya kule kwenye jimbo la Donbass ya kuuwa raia wanozungumza Kirusi, kundoa lugha ya Kirusi isifundishwe mashuleni na kufanya uharamia mwingi wa kinazi, ndo akaja na neno Denazification yaani kuondoa tabia na stratejia za kinazi nchini Ukraine.
Hii "denazification" ilikuwepo baada ya vita kuu ya pili ya Dunia ambapo nchi za Ujerumani na Austria zilishikiwa bango ziondokane na unazi katika jamii zao kwenye maeneo ya utamaduni, uchumi, siasa na hata masuala kama mahakama.
Hivyo unazi ambao umekuwa ukirudi kwa kasi na kufadhiliwa na baadhi ya nchi nyingi za Ulaya magharibi ni pamoja na ule ulokuwa ukifanywa nchini Ukraine na Zelesnki akaunyamazia.
Sasa tukirudi kwenye suali lako la msingi kwamba je warusi ni wayahudi halisi yaai waisraeli? Jibu ni kwamba ipo 50-50 kwasababu wayahudi wengi wa Russia ni asilimia kubwa na pia wapo pia katika nchi za Poland, Lithuania, Slovakia, Ukraine, Moldova, Estonia, Belarus na Latvia.
Hata Roman Abramovich ni myahudi ambae leo anatumia pasi ya kusafiria ya Israeli kwasababu ya kubughudhiwa kwenye biashara zake nchini Uingereza. Wapo wayahudi wa Kirusi wengi sana nchini Israeli wakiendesha maisha na kuishi sehemu zote mbili.
Ndo kusema hata Joe Biden ziara yake mashariki ya kati imepigwa ubaridi kutokana na kwamba Israeli yaona kwamba Marekani inakosea kuwachonganisha wayahudi wote, isipokuwa ni Putin ambae anataka kuwakutanisha kwa kuiadhibu Ukraine.
Ndo kusema kwamba Wayahudi wengi wanaunga mkono kiaina operesheni inofanywa na Putin ili kumsaidia Zelenski aondokeane na hawa wanazi.
Mwisho , hakuna muisraeli feki waliopo Israeli bali ni wahamiaji wa kiyahudi ambao mwaka 1948 walipewa eneo hilo kwa baraka zote na nchi za magharibi na UN.
Wayahudi wa Russia ni uzao wa Ashkenazi ambao ni wale walianza kulowea katika sehemu nilozitaja hapo juu baada ya kutangatanga kitambo sana.
Ukitaka kuwatambua kizazi cha Ashkenazi soma biblia kitabu cha Mwanzo sura ya 10.
Mwisho eti kwamba warusi waisraeli watashinda vita "kwasababu Mungu yupo nao" hiyo ni imani na kila mtu atafrisi kwa namna yake vita hii na mwisho wake.
Nafikiri utaelewa mkuu, sorry kwa urefu wa hii kitu nilitaka kukuelimisha.