Mimi naomba kupingana na wewe.
Mwaka 2014, Raisi wa Ukraine ambaye alikuwa na Pro-Russian (hivyo kuhakikisha usalama wa Urassia kutoka EU) alipinduliwa, na kusemekana kwa msaada wa Marekani. Hiyo ndiyo sababu ya Crimea kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa Russia kwa kuwa Raisi mpya alianza kuwatenga na kuwauwa (inasemekana) watu wanao ongea ki Russia.
Eneo la Donbas ambayo ni Doneski na Luhaski waka jitoa Ukraini na kutaka uhuru.
Mwaka 2015, Russia, Ukraine na Germany wakafanya makubaliano yanayoitwa Minsk Agreement kwamba Ukraine itaacha kuipiga Donesk na kukubali uhuru wa Donesk na Luhask. Kumbuka haya maeneo yote yametengena na Russia.
Russia alikubali kwa kuwa shida yake ilikuwa usalama wake maana Ukraine baada ya mapinduzi walianza mchakato wa kutaka kujiunga na EU na NATO kitu ambacho Russia hataki kupakana nao.
Lakini mpaka 2022 bado Ukraine aliendelea kupiga Donbas na alikuwa kashaanda wanajeshi zaidi 60,000 ili kuivamia na kuimaliza Donbas kabisa.
Kama angefanikiwa, ina maana, Russia Angekuwa amepakana moja kwa moja na taifa linalotaka kujiunga na EU na NATO. Taifa ambalo lilikuwa limekubali kuwa neutral ili Russia na NATO wasi pakane.
Hapo ndipo Russia alipoanza kupeleka majeshi yake mpakani. Mazungumzo ya amani yaka feli, EU na NATO wakazidi kumpa kichwa Ukraine ambaye naye akazidi kuleta vitisho.
Russia akaingia kulinda eneo la Donbas. Na ndiyo mapigano yaliyopo sasa. Na siyo eti kutaka kuirudisha Soviet.
Nadhani somo limeeleweka.