Ona mfano wa propaganda ya Kirusi kijinga sana (kutoka vyanzo vilevile tunavyolishwa hata hapa..)
View attachment 2304931
Bwana Russian Bear anataka kutuaminisha kwamba wananchi katika Ulaya wanapinga usaidizi kwa Ukraine. Kushoto anaonyesha kibao kilekile kimoja mara mbili "No war with Russia", kulia ni tangazokwenye nyumba nchini Ujerumani inayotangaza " Warusi si maadui zetu, maadui wako Washington, Berlin n.k."
Upande wa Poland anataka kutuaminisha: “Watu wa kawaida hawataki kuvutwa katika vita dhidi ya Urusi kwa maslahi ya wtu wengine. Serikali haijali maoni ya ananchi inatakakupendeza tu tu mbwana wa Magharibi"
Hali halisi vibao hivi ni uthibitisho wa hali ya uhuru ambao haupo Urusi! Dola linakinga wananchi wenye mawazo kinyume cha watu wengi, ila Mrusi wetu anataka kupumbaza wasomaji wake eti hao wachache ni raia wengi.
Maana huko Poland
97 % za Wapoland wanaona Urusi hasi (91 % hasi sana)
91 % za Wapoland wanpendelea Marekani
89% za Wapoland wanasimama upande wa NATO
84% za Wapoland wanakubali kutuma silaha Ukraine.
View attachment 2304959