Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Warusi wenzangu nadhani tulikwisha lisema Sana hili jambo kuwa USA, NATO na EU njia pekee ya kujinasua na kuanguka kiuchumi ni kuingia vitani na Russia, naona marekani kamuogopa mrusi na kwenda uchina tukae mkao wa kula Vita ya tatu ya dunia ipo karibu
 
Hilo USA amekwishalijua na njia pekee na karata ya mwisho aliyokuwa nayo ni kuingia vitani, kwanini marekani kaenda uchina na Siyo Russia ni kuwa anajua kitendo cha kuiangusha uchina kiuchumi inamaana dunia nzima itaanguka na ndiyo anachokitaka mmarekani, na nakuhakikishia marekani lazima aingie hapo China ndiyo karata aliyobaki nayo
 

Mkuu pia kilichopelekea US dolle kuwa strong sababu kubwa ni kuanguka kwa Euro. Sarafu ya Euro ilovaanza kuporomoka in value ilipelekea investors na Mataifa mengi kugeukia dollar na kuipiga chini Euro.
 
Uchumi wa marekani ni uchumi wa opportunity ya fedha yake tu ....kitendo cha dola kuwa ndiyo pesa kuu ya biashara duniani ndicho kinaifanya marekani kuwa tajiri ...hata ingekuwa leo pesa yetu ndiyo iwe pesa ya dunia kibiashara tz ingekuwa tajiri ndani ya mwaka mmoja tu maana tungechapa pesa nyingi kuliko matumizi yetu ya ndani pasipo kusababisha mfumuko wa bei kwa pesa yetu wala kuporomoka thamani ya pesa yetu
 
Mandonga katika utetezi
 
Uchumi hauko hvyo, ata suplly and demand haiko hvyo, ni kweli nchi zote duniani zikiamua hvyo itaanguka, ila swali ni kwamba nani atafanya aamue hvyo, dunia ishakubaliana kuwa Dolla ndo hella ya dunia
Hakuna ataetaka kuiacha, maana idea ni kuwa mtu akitaka kuacha kitu ina maana amepata kingine bora, sasa kwenye kingine ndo hamna
 
Au sio sasa nenda na kwa hawa world economic forum. Interest rate hikes vs inflation: How are different countries doing it?



Ukifika waambie wote mazuzu hawajui kitu uwafundishe vile inavyotakiwa wafanye au wazungumze.

Pro west usizungumzwe ushubwada wa US πŸ˜‚ akili zinawaruka ha ha ha lakini kazaneni kikubwa muwaambie wawaongezee posho.

Oh nimesahau nenda pia kwenye jarida la the Guardian, Why are central banks pushing to raise interest rates? | Bank of England | The Guardian



Watemee kila aina ya shit unayo ijua, wakalishe chini wafundishe Uchumi unao ujua wewe huo walio nao wanadanganya dunia.

Note; sijawahi kumjibu mtu from no where bila back up ya maelezo yangu. Ukinikurupukia kichwa kichwa utajidharilisha.
 
Mimi ni pro Russia lkn kwahili hapana. Typically photoshop
 
Kwan haiwezekan kuwa na jagi la maji unachemsha unapeleka bafuni kuoga na ndoo?
πŸ€£πŸ€£πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡Mkuu julaibibi umenichekesha sana aisee!

Hayo mambo ya kuwepo ndoo za kutunzia/kubeba maji hayapo Ulaya.

Maji hutoka masaa 24/7 na tayari kuna automated systems za kuchemsha maji. Umeme hali kadhalika huwa haukatiki, ukikatika ghafla mfano usiku mnafanya kushangaa na pengine mnaweza kutoka mbio ndani kwenda nje mkidhani kuna shoti. Maji ya moto yanahitajika si tu ktk kuoga bali kuoshea vyombo, kunawa n.k. kwa kuwa ktk majira ya winter maji huwa na baridi zaidi kiasi kwamba huwezi yatumia ktk matumizi mbalimbali pasi kuwa ya moto/vuguvugu.
 
Unajua maana yake kaka, mi ni mtu wa forex na hyo ni fundsmental analysis, increasing interest rate always makes yur money strong,
Hayo ni mambo ya kubalance inflation tu, na ya sahv ni Euro inashuka maana wana purchase sana hella ya Russia na yao inashuka thamani, soko sahv linacontrolliwa na DXY, ndo waana investors wengi wamekimbilia Dollar kutokana na kuwa strong, Dollar ilianguka enzi za Corona maana watalii wengi walipause na economics nyingi duniani zilisimama hivyo demand ya dolla ikashuka, enzi hizo Euro moja ilifika 1.25USD
 
Kua mtu wa forex haikufanyi we kuzijua principle za uchumi. So uwe na brake siku nyingine sio kuzungumza kwa mihemko.

Sikia ndugu kuna more than 7.8 trillions Euro (Banknotes and Coins) in circulation. Mauzo ya Gas kwa EU kutoka Russia ni around 1 Billions Euro kwa siku. Hii exchange kutoka Euro kwenda Ruble ni below 0.013% ya Currency ya Euro. Hio changes (Volume) huwezi kuiwekea hoja ya Nguvu kua ndio sababu ya Euro kuporomoka thamani.

Angalia pia vitu vinavyotoka EU(export ya EU) ambayo of course inalazimisha wengine wanunue Euro ni kiasi gani kisha angalia exchanges kutoka Euro kwenda Ruble na kwa fedha zingine kurudi Euro kisha linganisha.

Ukikutana na mjuzi atakushangaa sana... Uchumi ni hesabu , uchumi sio porojo wala maneno mepesi na sababu za hovyo kama hizo zinazo kutoka kinywani.

Mahaba yanakutia upofu kuzijua sababu haswa za kuporomoka thamani ya Euro ambayo kubwa haswa ni Inflation. Unaona Inflation hiyo sio deal eti exchange ya Ruble πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Msivamie taaluma za watu ndugu wala msikae uko mnamezeshwa point 2 tatu za ku'exchange fedha basi ndio mnajiona mshaujua uchumi.

Uchumi ni carrier ya watu bro, learn kabla hujajipa gut ya ku'argue na mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…