LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
kinacho fuata ni kuondoa serikali ya Ukraine madarakani na kuweka serikali nyingine tiifu
Yani apigane atumie resources zote ili tu aweke Madarakani serikali tiifu,ndio utakuwa upumbavu gani sasa.Hapo lengo ni kuichukua Ukraine yote na kuwa sehemu ya Urusi kama ilivyokiwa awali-au hujasikiliza speech ya Putin babu.
 
Au kitu kizito
 
Zile drone za uturuk zikiwashwa itakuwa kama Ethiopia, mrusi ataomba poo.muache aingize magari kwa pupa nahisi analiwa timing kama ilivyokuwa ethiopia, syria kwa jeneral khalifa, na armenia.
Huyu huyu aliyesaidiwa na Putin pindi alipotaka kupinduliwa?

Huyu huyu alipoingiza mguu Syria alipata tabu sana na air defensive ya Mrusi na askari wake wengi kuuliwa?
 
Apigwe tu
 
Tusiposhangilia ulitaka tufanyaje:

Hatuna huwezo wa kuathiri maamuzi ya Marekani, Umoja wa Ulaya, Uchina Wala Urusi.

Wengi wenu mnaokemea Sasa mlikuwa mnashangilia wakati Russia anadharauliwa na akikanywa kama mtoto kumbe jidume linawapimia tu.

Mpaka sasa team Russia inaongoza.

Kumbuka sio Urusi tu jumlisha na Mchina, Korea ya kaskazini, Iran, Nicaragua, Venezuera, India, Serbia, Montenegro.

Mpaka Sasa Croatia, Hungary zimesema haziwezi kuingia kwenye ugonvi wa kuua waslav wenzao.

Turkey haieleweki.

Mjerumani Yuko pembeni

Mfaransa anasita sita

Bado babu Biden hajaamua
 
Rais Vladmir Putin ameufungua mlango wa vita ambayo itakwenda kuyagharimu maisha ya warusi wengi katika siku za usoni. Vita hii hatapigana na Ukraine peke yake bali itaingiliwa na kila anaefungamana na serikali ya ukraine.

Vikwazo vya kiuchumi vinavyoendelea kuwekwa dhidi ya serikali ya Putin vitakwenda kuyagharimu maisha ya warusi wengi na huu ni mwanzo wa vita kuu ya tatu ya dunia na itasambaa ulaya yote ya mashariki mpaka mashariki ya kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…