LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
kinacho fuata ni kuondoa serikali ya Ukraine madarakani na kuweka serikali nyingine tiifu
Yani apigane atumie resources zote ili tu aweke Madarakani serikali tiifu,ndio utakuwa upumbavu gani sasa.Hapo lengo ni kuichukua Ukraine yote na kuwa sehemu ya Urusi kama ilivyokiwa awali-au hujasikiliza speech ya Putin babu.
 
Muda huu tunavyongea mji wa Chernobyl imeshangukia kwenye mikono ya Warusi
Yah! Nimeiona wamekamata na nuclear plant ya huko!

Screenshot_20220224-212156.png
 
Putin Ana sema Ana weza kukupiga na kitu chenye ncha kali kilicho changanywa na mlipuko mkubwa kuliko ulio wahi kusikia au kuambiwa akiwa chooni kwake wewe ukiwa kokote kwenye angle ya Dunia! kumbuka mambo ya kutumiana barua kwenye bahasha yalisha pitwa na nyakati!
Au kitu kizito
 
Zile drone za uturuk zikiwashwa itakuwa kama Ethiopia, mrusi ataomba poo.muache aingize magari kwa pupa nahisi analiwa timing kama ilivyokuwa ethiopia, syria kwa jeneral khalifa, na armenia.
Huyu huyu aliyesaidiwa na Putin pindi alipotaka kupinduliwa?

Huyu huyu alipoingiza mguu Syria alipata tabu sana na air defensive ya Mrusi na askari wake wengi kuuliwa?
 
Adui mkubwa na mbaya sana ni jirani yako. Ukraine ni jirani wa karibu sana na Russia.

Lengo kuu la NATO na Marekani ni kaziangusha Russia, China, N.Korea, Iran na Venezuela ili kuondoa mizania duniani. Hizi nchi zikianguka kutakuwa hakuna kikwazo kwao kwenye kila jambo, na hata ukoloni utarudi upya.

Ukraine jirani mkubwa na Russia anapokuwa na uswahiba na NATO na Marekani ni hatari sana kwa Russia, China, n.korea, Iran na dunia.

Marekani anapeleka silaha nzito Ukraine kwa kisingizio Cha kuihami Ukraine dhidi ya Russia.

Muwahi Adui yako kabla hajamaliza kujipanga, hicho ndicho anachofanya Putin kwa Ukraine. Naungana na Putin kwenye safari yake, dunia atakuwa salama zaidi kama urusi itakuwa na nguvu pia.

Putin anataka kuionyesha dunia vita ya kigiditali.
Apigwe tu
 
Huku kwetu tanzania naona kila mtu kawa mshangiliaji wa kusifu urusi kuwa mbabe.

sawa ni mbabe ila unafahamu mzozo wa vita vya pili vya dunia ulianzaje.

Hii ni historia ambayo inaweza kutokea na kwa nini mataifa makubwa yamebaki kukemea na sio kuunga mkono.

Urusi bado inatafuta njia ya kurudisha maeneo yake iliyopoteza kwa kuvunjika umoja wa USSR.kuvinjika kwakwe ni moja ambalo taifa tunalitegemea labda linaweza kuipa nguvu ukrain ni USA akifatiwa na washirika wake.

katiba taarifa ambazo watu wengi wanaziipuzia kuwa urusi alishaandaa kila target ya nchi yoyote itakayo taka kuungilia jambo lolote.

na kama hizi nchi zitaingilia basi ile sinema inayo itwa Terminal ikionesha kila nchi ikilusha kombora ndio itakuwa mwanzo wa vita vya tatu kwenye dunia.

sisi tunaoshangilia hata dawa kufikisha vijijini ngumu embu tujitafakari kuomba amani ya dunia.

kutokufikia na uchumi kuyumba wa dunia na vita ambazo kila kona zimetawala
Tusiposhangilia ulitaka tufanyaje:

Hatuna huwezo wa kuathiri maamuzi ya Marekani, Umoja wa Ulaya, Uchina Wala Urusi.

Wengi wenu mnaokemea Sasa mlikuwa mnashangilia wakati Russia anadharauliwa na akikanywa kama mtoto kumbe jidume linawapimia tu.

Mpaka sasa team Russia inaongoza.

Kumbuka sio Urusi tu jumlisha na Mchina, Korea ya kaskazini, Iran, Nicaragua, Venezuera, India, Serbia, Montenegro.

Mpaka Sasa Croatia, Hungary zimesema haziwezi kuingia kwenye ugonvi wa kuua waslav wenzao.

Turkey haieleweki.

Mjerumani Yuko pembeni

Mfaransa anasita sita

Bado babu Biden hajaamua
 
Rais Vladmir Putin ameufungua mlango wa vita ambayo itakwenda kuyagharimu maisha ya warusi wengi katika siku za usoni. Vita hii hatapigana na Ukraine peke yake bali itaingiliwa na kila anaefungamana na serikali ya ukraine.

Vikwazo vya kiuchumi vinavyoendelea kuwekwa dhidi ya serikali ya Putin vitakwenda kuyagharimu maisha ya warusi wengi na huu ni mwanzo wa vita kuu ya tatu ya dunia na itasambaa ulaya yote ya mashariki mpaka mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom