Urusi na Ukraine, ili kuelewa chanzo cha mgogoro wao vizuri ni muhimu kujua kidogo historia ya nyuma kuhusu uhusiano baina yao.
Hapo zamani nchi hizi zote zilikua zinaunda Umoja wa kisovieti (USSR), na muungano huo uliundwa rasmi mwaka 1922 na kuvunjika mwaka 1991.
Umoja huo ulipovunjika Ukraine ilijipatia uhuru wake kwa mara ya pili mwaka huo huo 1991,
hapo awali walipata uhuru wao mwaka 1917 lakini baadae ndio waliunganishwa kwenye umoja wa Kisovieti mwaka 1922 ambao kwa wananchi wengi wa Ukraine waliona hauna manufaa yoyote kwao.
Tangu kuvunjika kwa muungano huo, Urusi na Ukraine zimekua na mvutano wa hapa na pale chanzo kikuu kikitajwa kua maslahi ya kiusalama zaidi, Na Urusi ndio amekua tishio zaidi sababu ndio taifa lenye nguvu zaidi kwa ukanda huo na Dunia kwa ujumla.
CHANZO CHA UGOMVI ni pale Serikali ya Ukraine ilipo badiri mpango wake na kutaka kujiunga na NATO,
Uamuzi huu haukuwafurahisha Urusi ambao waliamua kujibu kwa kupeleka wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka wa Ukraine.
Kwa mujibu wa picha zilizotolewa na Wizara ya ulinzi ya Urusi zilionesha vikosi vyake vikiendelea na mazoezi ya kijeshi kwenye eneo la mpaka huo.
NATO - Ni jeshi la pamoja linaloundwa na nchi 27 za ulaya, Marekani, Canada na Uturuki. Nchi zinazounda umoja huu kwa kiasi kikubwa zinafuata misingi ya Kibepari na nyingi pia zimekua na uadui na nchi ya Urusi katika masuala mbalimbali kama vile uchumi na siasa
KWANINI UKRAINE WANATAKA KUJIUNGA NA NATO ,Chanzo kikuu ni kujiimarisha kiusalama, Tangu Umoja wa Kisovieti ulivyovunjika, Hofu mara kadhaa imekua ikitokea kwamba Urusi anaweza kuivamia Ukraine, Lakini mara zote Urusi amekua akipinga mpango huo.
Licha ya kupinga,
Mwaka 2014 Urusi walifanikiwa kutwaa Rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, Na kuanza kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi ambao waliteka sehemu kubwa za Mashariki mwa Ukraine.
Urusi walitwaa Pwani hiyo baada ya kutokea kwa Mapinduzi Ukraine mwaka huo huo 2014
ambayo yalimuondoa madarakani Rais wa wakati huo Viktor Yanukovych ambae anatajwa kua alikua ni kibaraka mkubwa wa Urusi.
Na mpaka sasa sehemu kama Donetsk na Luhansk kutokea Ukraine ni maeneo ambayo yalijitangaza kuwa huru na hata vita iliyokua inaendelea Ukraine kabla ya hii inayotaka kutokea ilikua ni kutokea vikosi vya hizo sehemu ambazo zinataka kuendelea kujiongoza zenyewe.
Inasemekana Urusi amekua akitoa msaada wa kijeshi kwa waasi hao ili kuiondoa kabisa serikali ya Ukraine, Na ndio maana serikali ya Ukraine ikaja na mpango wao wa kujiunga NATO ili kutaka kupata misaada ya usalama sababu kadili siku zilivyo enda ndio serikali hiyo ilizidi kua hatarini kwani Urusi ilifanya mbinu nyingi hatari za chinichini.
Moja ya hatari nyingine inayoendelea pia ndani ya Ukraine, Ni mipasuko ambayo kuna watu wanatamani kuwa chini ya Urusi na wengine wanataka kubaki kama walivyo.
Kwenye mgogoro huo NATO haikuingilia moja kwa moja, Lakini jibu lao lilikua ni kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania.
Sasa hali hiyo ndio inawafanya Urusi kila siku kupiga kelele kwamba vikosi hivyo viondolewe, Ina maana kama NATO wataendelea kupeleka vikosi zaidi Ukraine ni kuzidi kuongeza tishio zaidi kwa usalama wa Urusi.
HIVYO BASI, Chanzo cha mgogoro wa Urusi na Ukraine ni; Urusi hataki kuona Ukraine akijiunga na NATO kwa hofu ya usalama kwake wakati nao Ukraine wanataka kufanya hivyo kwa hofu ya usalama ndani yake yote ni kwa sababu ya matendo ambayo wanadai yanafanywa na Urusi ndani ya nchi hiyo.
Je hii ni WW3 [emoji848]
Kama vita itazuka inaweza kua Vita ya Tatu Ya Dunia, sababu itahusisha mataifa mengi kwa wakati mmoja na zaidi ni hofu ya matumizi ya silaha za Nyuklia ambazo zinaweza kuathiri karibia dunia nzima, Na ikumbukwe Urusi yeye anaungwa mkono na Korea Ya Kaskazini, Venezuela na China ambazo nazo ni nchi zenye nguvu kijeshi.
.