1. Kwanza hiyo kauli ya military contingents and infrastructures' Putin anaitoa kuzionya nchi ambazo zimeshapeleka maombi ya kujiunga na NATO na zinazusubiria maombi yao kukubaliwa, Hii inahausiana vipi na Ukraine nchi ambayo haijawahi kupeleka maombi ya kujiunga na wala haijawahi kuwa hata NATO partner kama Japan, Australia au Korea??
2.Terrritorial disputes ni upuuzi na propaganda tu za Putin, narudia tena Russia haina madai yoyote Rasmi kuhusu mipaka au maeneo ya Ukraine, imekuwa na madai rasmi na nchi nyingine majirani zake kama China na Japan ila kwa Ukraine hawana malalamiko yoyote rasmi yanayohusiana na mipaka kwamba kuna maeneo yao wanahitaji warudishiwe.
3.Madai ya Russia Speaking people ni zaidi ya utopolo, hembu fikiria leo hii Uingereza ivamie Cameroon kuwasaidia English(Anglophone) speaking people wanaolalamika kukandamizwa na kubaguliwa na French speaking(Francophone) wanaotawala Cameroon, Leo Kenya ije ivamie Tanzania kwa sababu kuna matatizo ya watu wanaouzungumza Kimasai Ngorongoro au Loliondo, Rwanda iivamie Congo kwa sababu kuna watu wanazungumza Kitusi huko wanalalamika kunyanyaswa. Kama hii itakuwa ndio njia ya kutatua mambo unafikiri hapa duniani patakalika tena??
(Bado sijazungumzia hakuna watu wanaozungumza Kirusi waliokuwa wananyaswa Ukraine, ni porojo tupu)
1. [emoji1787]
Ulikuja kwa speed kali na madai ya kwamba NATO haina silaha. Sasa hv umekuja na madai ya kwamba Ukraine haihusiki na 'military contingents and infrastructures' bali sweden na finland. Mchezo wa kuhamisha magoli! Kwa kukumbusha tu hakuna mtu aliyehusisha silaha za NATO na Ukraine kama ulivyodai hapa.
Nikukumbushe zaidi in brief. Kwenye post yangu uliyoniquote kwa mara ya kwanza mimi nilisema kuna tofauti kati ya #FinSwed kujiunga na NATO na Ukraine kujiunga NATO kisha nikasema hata hao wawili wakijiunga hawataruhusiwa kuruhusu deployment ya silaha za NATO kwenye nchi zao na wakifanya hivyo Moscow itarespond alafu nikaweka na statement ya putin mwenyewe. Wewe ukaja ukidai nato haina silaha nilivyokujibu madai yako umekuja na mengine kwamba 'silaha hizo' hazihusiani chochote na Ukraine bali #FinSwed. Hoja yako ya msingi ni ipi!? Nato haina silaha au haijawahi kupokea maombi ya kujiunga kutoka kwa Ukraine!?
Kuwa muadilifu.
a. Kama umebadili msimamo na sasa unakubali nato ina silaha basi ukane msimamo wako wa kwanza hapahapa jukwaani wa kudai nato haina silaha
b. Kama bado msimamo wako ni uleule kwamba nato haina silaha tupe tafsiri yako (kwa kiswahili) Putin anaposema 'military contingents and infrastructures' anamaanisha nini!?
2 & 3. Unalazimisha watu wakusikilize wewe kuhusu maswala ya ndani ya Urusi tena ya kiusalama kuliko raisi wa Urusi mwenyewe. unastaajabisha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani wewe unaongea Point kuhusu Urusi na putin anaongea porojo/utopolo kuhusu Urusi yake. Sio maajabu haya!?
Kwanza umeona sasa ulikosea kutafsiri niliposema Russian speaking Ukrainians wewe ukadai nimesema raia wa ukraine ambao ni raia wa urusi!?
LPR & DPR walitambuliwa kama organization za kigaidi na serikali ya Ukraine tangu mwaka 2014. Unafikiri Ukraine ilikuwa inawatreat vipi hao watu baada ya kuwa lebel kwa ni magaidi!? Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya sio!
Alafu Putin hajaingia tu donbass kwa kujiamulia bali waliomba msaada wenyewe (lpr&dpr) kutoka russia. Hata us & co Kuna mahali p3ngi tu waliombwa kwenda kutoa msaada na wakaenda. Au unataka kusema urusi hana haki ya kwenda kutoa msaada popote atapoombwa kwenda ikiwa yeye ameona vizuri kwenda!?
Kuwepo kwa mapigano tu ya lpr na dpr dhidi ya serikali ya Zelensky niushahidi kwamba hao watu ni wenyewe ndio walikuwa hawaridhishwi na jinsi walivyokuwa treated na bwana Zelensky hapo kbl otherwise kwa nini wapigane vita vikali namna hii wako radhi wafe na miji yao iharibiwe bila sababu za msingi!? All the people in donbass are stupid!? Watu wanasema wananyanyaswa na wanapigana kufa na kupona dhidi ya aliyekuwa anawanyanyasa wewe unakuja hapa kusema madai yao kuwa walikuwa wananyanyaswa ni porojo na propaganda, duh!