1. Kwanza hiyo kauli ya military contingents and infrastructures' Putin anaitoa kuzionya nchi ambazo zimeshapeleka maombi ya kujiunga na NATO na zinazusubiria maombi yao kukubaliwa, Hii inahausiana vipi na Ukraine nchi ambayo haijawahi kupeleka maombi ya kujiunga na wala haijawahi kuwa hata NATO partner kama Japan, Australia au Korea??
2.Terrritorial disputes ni upuuzi na propaganda tu za Putin, narudia tena Russia haina madai yoyote Rasmi kuhusu mipaka au maeneo ya Ukraine, imekuwa na madai rasmi na nchi nyingine majirani zake kama China na Japan ila kwa Ukraine hawana malalamiko yoyote rasmi yanayohusiana na mipaka kwamba kuna maeneo yao wanahitaji warudishiwe.
3.Madai ya Russia Speaking people ni zaidi ya utopolo, hembu fikiria leo hii Uingereza ivamie Cameroon kuwasaidia English(Anglophone) speaking people wanaolalamika kukandamizwa na kubaguliwa na French speaking(Francophone) wanaotawala Cameroon, Leo Kenya ije ivamie Tanzania kwa sababu kuna matatizo ya watu wanaouzungumza Kimasai Ngorongoro au Loliondo, Rwanda iivamie Congo kwa sababu kuna watu wanazungumza Kitusi huko wanalalamika kunyanyaswa. Kama hii itakuwa ndio njia ya kutatua mambo unafikiri hapa duniani patakalika tena??
(Bado sijazungumzia hakuna watu wanaozungumza Kirusi waliokuwa wananyaswa Ukraine, ni porojo tupu)