Mpaka sasa hii vita imeshathibitisha kuwa Urusi ni nchi yenye uwezo wa juu kivita na USA na NATO wanaiheshimu sana linapokuja suala la vita sababu Hawajakurupuka kupeleka majeshi na tumejionea energy crisis na inflation ilivyotikisa.
Ukraine ni nchi jasiri na hawakati tamaa kiwepesi, Mpaka leo bado wana ujasiri wa kudefend na sasa wanafikiria kuishambulia Urusi katika maeneo waliyonyang'anywa. Na iwapo Urusi haitaamua kuanzisha vita kamili bila kujali aina ya silaha basi Urusi inaweza zidiwa.(Hii haimaanishi kuwa Urusi ni dhaifu, ingekuwa dhaifu naamini USA na washirika wangeshafanya yao. Naamini Urusi na USA/NATO huenda hawajawa tayari kwa vita kamili sababu na wao watapoteza, Dunia itapoteza. Inaonekana hakuna win-lose wala win-win ila kuna Lose-Lose)
Jamii Forum kuna uzalendo wa kimihemko, utimu na ushabiki kwa nchi isiyo Tanzania.