Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Baada ya Urusi kupoteza vifaa vingi vya kijeshi dhidi ya Vita vyake na Ukraine sasa yaomba msaada wa Drones toka Iran.Hiki ni kichekesho🤔
Na wewe unajifunza propaganda???? Hiyo ni vita au SMO kama wanavyosema Warusi...sasa ulidhani Warusi hawawezi kupoteza vifaa? Kuna ubaya gani kwa Russia kupokea drones kutoka Iran? Mbona Ukraine inapokea vifaa na fedha kutoka nchi zaifdi ya 30 zikiwemo za NATO? au hamjui hayo?? Russia haipambani na Ukraine peke yake...Russia in apigana vita na USA, Ujerumani, UK, Poland, Ukraine yenyewe, Canada, Ufaransa na nchi nyingine kadhaa za ulaya. Do you know that. Pamoja na hayo Russia inazidi kusonga mbele kilomita kw akilomita kwenye uwanja wa vita...

Halafu kwenye mapambano ya kiuchumi nchi za ulaya na Marekani zinaumia vilivyo. Maandamano ya wananchi kwa maelfu yanafanyika kwa baadhi ya nchi huko ulaya kupinga vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Russia. Maana yake ni kuwa kwenye uwanja wa kiuchumi Russia pia inashinda vita hivyo. Ni kweli Russia nayo inaumia kiuchumi lakini nchi za ulaya nazo ziko katika hali mbaya kiuchumi....
Wito wangu kwenu nyie vijana pro-mabeberu acheni kushabikia upuuzi. Hii ni vita ...wanajeshi wa Russia wanakufa lakini wale wa Ukraine na askari wa nchi za ulaya waliopo huko Ukraine kwa mgongo wa raia wanaojitolea nao wanakufa kwa maelfu.....Mwisho wa yote atapatikana mshindi na wala hakutakuwa na draw. na mshindi atakuwa mmoja tu naye ni Russia. Lakini ushindi wake utakuwa wa damu nyingi kama ilivyokuwa wakati wa WWII.
 
Kuna jamaa wanaoiunga mkono Russia na wengine wanaoiunga mkono Ukraine,walikuwa na nondo kweli kweli!Ila Sasa kila nikiingia humu siwaoni wakichangia!Ile shauku ya mtu unapiga kazi,ukipata ka break ndio unachungulia thread hii haipo Tena!
Hii thread imeingiliwa na ushabiki mavi.

Hao mashabiki wenyewe hawajui chochote kuhusu hii special operation hawajui chochote kuhusu Ukraine na Russia lakini wanachangia lazima uzi upoteze ladha
 
Kuna jamaa wanaoiunga mkono Russia na wengine wanaoiunga mkono Ukraine,walikuwa na nondo kweli kweli!Ila Sasa kila nikiingia humu siwaoni wakichangia!Ile shauku ya mtu unapiga kazi,ukipata ka break ndio unachungulia thread hii haipo Tena!
Wengi wa pande zote wameondoka kwa kuwa uzi huu umevamiwa na mashabiki na wapuuzi wachache wasiokuwa na nondo bali ushabiki wa kipuuzi. wewe fikiria watu wawili wanajaza uzi kwa mipichapicha fake kutoka youtube yaani hata maana ya mjadala haipo tena....utadhani ushabiki wa simba na yanga...mwingine anadiriki kuandika eti analeta mipicha hiyo ili 'kuwakera'...yaani hayupo kutoa elimu bali kukera...utoto mwingi umejaa humu, kwa hiyo wachambuzi wa maana wamepungua mno.
 
Siyo tu kwamba hawaijui Russia na Ukraine tu bali nakuthibitishia hata Tanzania hawaijui.
Kweli mkuu nimeliona hilo taifa lao hawalijui ndo wataijua Russia

Yaani siku hizi JF ina vijana wanajiita wasomi lakini wana hoja dhaifu sijapata ona. Miandiko ya ovyo, hoja za ovyo, kiingereza cha ovyo.

Forums nyingi saivi za JF zinaanza kupoteza mvuto
 
Wengi wa pande zote wameondoka kwa kuwa uzi huu umevamiwa na mashabiki na wapuuzi wachache wasiokuwa na nondo bali ushabiki wa kipuuzi. wewe fikiria watu wawili wanajaza uzi kwa mipichapicha fake kutoka youtube yaani hata maana ya mjadala haipo tena....utadhani ushabiki wa simba na yanga...mwingine anadiriki kuandika eti analeta mipicha hiyo ili 'kuwakera'...yaani hayupo kutoa elimu bali kukera...utoto mwingi umejaa humu, kwa hiyo wachambuzi wa maana wamepungua mno.
Hawa walikuwa na uzi wao wa picha na video kule "jukwaa la Photo " Nilikwenda kule nikawa nawanyoosha kwa kuwapa ukweli. Walinitimua kwenye uzi huo kuwa wao hawataki uchambuzi wa ukweli wanataka picha na video za front line ya Ukraine. Bahati mbaya sana video na picha nyingi walizokuwa wanaweza kule zilikuwa zinakiuka maadili ya upashaji habari na utu pia nyingine zilikuwa za kubumba!

Hata hivyo, ni nadhani uzi huu unaweza kuwa unachafuliwa kwa makusudi kuzuia watu wengi wenye shauku ya kujua ukweli wa kinachoendelea kwenye operation demilitarization and denazification huko Ukraine. Pia kuna uwezekano wachafuaji wa uzi wanalengo la kuficha aibu ya upande Fulani wanaoutete kwenye Mgogoro huu.
 
Yaani we acha tu....kizazi Cha sasa duh.....nilikuwa mahali Fulani nawasilisha mada nikauliza swali la kimtego kwa wanaojifanya wasomi...Waziri wa elimu wa TZ ni Nani?! Kimya!!!! Tanzania ina mikoa mingapi? Mmoja akasema 20... Vita vya Tanzania na Uganda vilikuwa lini? Mmoja akajibu 1984...
Basi ipo siku nikiwa mkoa Fulani kwa majukumu na mwenzangu mmoja tukaingia kwenye mgahawa Kula baada ya kumaliza tukaamua tuchukue Bajaj ..vijana Wengi wakatukimbilia na bajaji zao...Mimi nikawaambia atakayejibu swali tunachukua bajaji yake...swali: Waziri mkuu wa TZ ni Nani? Mmoja akajibu Sumaye (wakati huo alikuwa ni Pinda) Swali jingine...Rais wa Kenya ni Nani? Mmoja akajibu Kagame..
 
Kuna jamaa wanaoiunga mkono Russia na wengine wanaoiunga mkono Ukraine,walikuwa na nondo kweli kweli!Ila Sasa kila nikiingia humu siwaoni wakichangia!Ile shauku ya mtu unapiga kazi,ukipata ka break ndio unachungulia thread hii haipo Tena!
Tatizo lenu mliharibu uzi kuleta taarifa za upande mmoja nyingi zikiwa za kutunga sasa hivi mkiletewa fact kinachoendelea frontline mnakataa na kusema uzi umeharibiwa hatuwezi kubali mlete habari za upande mmoja tena za telegram wakati ukweli tunauona kwenye media tofauti.
 
Itoe Al Jazeera hapo hao jamaa hawapendelei
Si kweli,nilikuwa msikilizaji wa Aljazeera mwanzoni ilipoanza,lakini later I found it bogus.Siri ni hii,kama wewe unaitegemea Aljazeera kama your only source of information, utaona ni a credible source,because you have nothing to compare with,lakini kama una sources zingine independent,you immediately discover that it does not offer credible,truthful and unbiased information.
 
Yaani we acha tu....kizazi Cha sasa duh.....nilikuwa mahali Fulani nawasilisha mada nikauliza swali la kimtego kwa wanaojifanya wasomi...Waziri wa elimu wa TZ ni Nani?! Kimya!!!! Tanzania ina mikoa mingapi? Mmoja akasema 20... Vita vya Tanzania na Uganda vilikuwa lini? Mmoja akajibu 1984...
Basi ipo siku nikiwa mkoa Fulani kwa majukumu na mwenzangu mmoja tukaingia kwenye mgahawa Kula baada ya kumaliza tukaamua tuchukue Bajaj ..vijana Wengi wakatukimbilia na bajaji zao...Mimi nikawaambia atakayejibu swali tunachukua bajaji yake...swali: Waziri mkuu wa TZ ni Nani? Mmoja akajibu Sumaye (wakati huo alikuwa ni Pinda) Swali jingine...Rais wa Kenya ni Nani? Mmoja akajibu Kagame..
Kwa mwendo huu sijui tunaelekea wapi?

Daah! Mpaka aibu mkuu

Ndio maana wanasiasa wanaweza kufanya watakavyo kwa sababu taifa lina watu wajinga wasiojua kuhoji wala kupambanua mambo
 
Si kweli,nilikuwa msikilizaji wa Aljazeera mwanzoni ilipoanza,lakini later I found it bogus.Kama wewe mwenyewe unaitegemea Aljazeera kama your only source of information, utaona ni a credible source,lakini kama una sources zingine independent,you immediately discover that it does not offer credible,truthful and unbiased information.
Tofauti ya Al jazeera na vyombo vya habari vya Magharibi kwenye hili suala la special operation hawana propaganda.

Na ndio maana media za West (CNN, BBC, SKY NEWS, DW, FRANCE 24, VOA, THE SUN) zimepoteza sana credibility kwenye vita vya Ukraine so far kwa sababu ya kusambaza habari za kipropaganda (chai nyingi sana yaani uongouongo)

Source independent ni zipi hizo mkuu?
 
Hawa walikuwa na uzi wao wa picha na video kule "jukwaa la Photo " Nilikwenda kule nikawa nawanyoosha kwa kuwapa ukweli. Walinitimua kwenye uzi huo kuwa wao hawataki uchambuzi wa ukweli wanataka picha na video za front line ya Ukraine. Bahati mbaya sana video na picha nyingi walizokuwa wanaweza kule zilikuwa zinakiuka maadili ya upashaji habari na utu pia nyingine zilikuwa za kubumba!

Hata hivyo, ni nadhani uzi huu unaweza kuwa unachafuliwa kwa makusudi kuzuia watu wengi wenye shauku ya kujua ukweli wa kinachoendelea kwenye operation demilitarization and denazification huko Ukraine. Pia kuna uwezekano wachafuaji wa uzi wanalengo la kuficha aibu ya upande Fulani wanaoutete kwenye Mgogoro huu.
Aisee uko sahihi...hata Mimi nadhani hi I no misinformation strategy ya west....Kuna Kila uwezekano taasisi za kijasusi za West zimeingilia Kati ....haiwezekani vijana baadhi wamo kwenye uzi huu for 24 hrs wakileta mipicha fake na hawachoki...why?!?! There must be something behind it, for sure...
 
Hawa walikuwa na uzi wao wa picha na video kule "jukwaa la Photo " Nilikwenda kule nikawa nawanyoosha kwa kuwapa ukweli. Walinitimua kwenye uzi huo kuwa wao hawataki uchambuzi wa ukweli wanataka picha na video za front line ya Ukraine. Bahati mbaya sana video na picha nyingi walizokuwa wanaweza kule zilikuwa zinakiuka maadili ya upashaji habari na utu pia nyingine zilikuwa za kubumba!

Hata hivyo, ni nadhani uzi huu unaweza kuwa unachafuliwa kwa makusudi kuzuia watu wengi wenye shauku ya kujua ukweli wa kinachoendelea kwenye operation demilitarization and denazification huko Ukraine. Pia kuna uwezekano wachafuaji wa uzi wanalengo la kuficha aibu ya upande Fulani wanaoutete kwenye Mgogoro huu.
Mlikuwa mmeugeuza huu Uzi kama sehemu ya kupiga porojo,na kuleta article ndeefu zisizo na uhalisia,..Mimi nilikuwa nawacheki tu hata kabla sijaamua kuwa member rasmi wa jamiiforum

Nilipozichoka hizo porojo zenu nikaamua kuingia front line kutetea ukweli..., uzuri ni kwamba sioni shida hata mtu akiniblock maana natambua jamiiforum Ina viewers wengi kuliko members wenyewe.., hivyo tunachokiandika hapa zaidi ni Kwa faida ya external viewers,

Huu Uzi haukuwekwa kwa ajili ya kulipigia promo taifa la urusi Kwa article zenu za kuokoteza kwenye telegram za warusi.., never..,hatutakubali...,upotoshaji mlioufanya unatosha Sasa

Sisi tutaendelea kuwaletea ushaidi wa """video game"" kutoka front line
 
Wengi wa pande zote wameondoka kwa kuwa uzi huu umevamiwa na mashabiki na wapuuzi wachache wasiokuwa na nondo bali ushabiki wa kipuuzi. wewe fikiria watu wawili wanajaza uzi kwa mipichapicha fake kutoka youtube yaani hata maana ya mjadala haipo tena....utadhani ushabiki wa simba na yanga...mwingine anadiriki kuandika eti analeta mipicha hiyo ili 'kuwakera'...yaani hayupo kutoa elimu bali kukera...utoto mwingi umejaa humu, kwa hiyo wachambuzi wa maana wamepungua mno.
Hapa bila mods kuingilia kati,tutapoteana!Au tusubiri vyuo vifunguliwe Ili huu upepo mchafu upite!
 
Back
Top Bottom