Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Tazameni video iikionesha eneo shambulizi limepigwa huko Kherson baadhi wameuliwa na wengine kukimbia Counter offensive ni balaa

Kweli??? Je, hii ni siku ya ngapi tuonyeshe ushahidi wa jimbo la Kherson na viunga vyake kukombolewa - on papers and social media, Yes, lakini sio kwenye frontline at all
Sasa mnao beza jeshi la Urusi someni habari hizi zinazo zungumza jinsi Russian inavyo weza ku-contain mashambilizi yote yanayo tekelezwa na jeshi la Ukraine - hivi ukipitia taarifa hii iliyo kwenda shule unaweza kweli kuamini kwamba Zelensky na genge lake wana means and ways za kuweza kuikomboa Kherson kweli??

Nyie endeleeni kudanganywa na propaganda za Zelensky na wapambe wake - wanawaleteeni video clips and photos zilizo pigwa na jeshi la Urusi wanazigeuza na kuzifanya mi za jeshi la Ukraine na nyinyi mnachotwa akili bila ya kuhoji swali - ajabu sana!!

Mkapa mwezi mwishoni mwa mwezi huu tutashuhudia mengi - sijui wanao kejeri jeshi la Urusi watajificha wapi - labda niwakumbushe kwa mara nyingine tena kwamba huwezi kushinda vita kwa kupitia mitandao ya kijamii na MSM hiyo ndio vita wanayo shinda akina Zelensky na western MSM usanii mtupu - tukiwambieni ukweli mnatuona wabaya na kutubatiza majina ya kila sampuli.

Mark my word: Zelensky and his western backers will never,repeat never win this war.
 
Unajua active members wako wangapi JF?Unajua thread hii inatembelewa na watu wangapi Kwa siku ambao ni members?
 
Kama humu Kuna watu timamu basi jaribu kujipiga Ile picha yako ya Facebook ukionyesha ulivyo na makalio makubwa ,halafu uone kama hutapata likes [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Unajua active members wako wangapi JF?Unajua thread hii inatembelewa na watu wangapi Kwa siku ambao ni members?
Mtu yeyote hasiye na account jamiiforum anaweza kupitia google au kiunganishi kingine na aka view habari habari hapa jamiiforums

Huyo mtu hawezi kulike Wala kukoment isipokuwa anakuwa msomaji tu,usikariri kwamba kila anayepata habari hapa jukwaani basi ni active members
 
Kuna watu wengi walikuwa wqnajiuliza kuhusu uwezo wa urusi na kutumia muda mrefu na Kwa gharama kubwa kuiendesha hii operation, kuna watu walisema kuwa operation hii imechukua muda sababu ni



1) Ni kutokana na ukubwa na uimara wa jeshi la Ukraine



2) Ni uwezo mdogo wa urusi kijeshi



3) Ni Kwa kuwa urusi anajali Sana raia Kwa hiyo hataki kuua watu wasio na hatia, ndiyo maana anaenda taratibu Kwa uhakika ili kupunguza madhara ya kivita



Lakini kwangu Mimi naweza nikachukua namba tatu, lakini Siyo Kwa uzito huo,

Sababu ninayoiona Mimi hii operation inaenda taratibu Kwa mkakati maalumu kutoka Moscow, kitendo cha operation hii kwenda taratibu ni Kwa sababu hii



Wakati Vita inaanza mrusi alikuwa mkali na aliwapiga bit nchi zote za ulaya kuwa wasijaribu kuingilia ugomvi huo na atakaye jaribu atakiona cha Moto, na katika kipindi hiki ndicho urusi ilikuwa inatishia kutumia nukes, na KOSA KUBWA ambalo EU,NATO na USA walifanya ni kuogopa na kukaa pembeni Kwanza wakimsoma mrusi, katika kipindi wanamsoma mrusi ndipo west wakaanza Kwa kujaribu kupeleka silaha Ukraine na walipolleka silaha urusi akaonyesha kama kazidiwa na kurudi nyuma na kuachana na Kyiv, kitendo hiki kiliwatia moyo Sana Ukraine, NATO na USA Kwa kudhania kumbe wanaweza kuimaliza urusi,
Ndipo USA na NATO pamoja na EU wakaungana Kwa kupeleka silaha nyingi Ukraine ili waweze kummaliza moja Kwa moja urusi, na ikiwezekana wakomboe Crimea huku wakiweka vikwazo vingi zaidi Kwa urusi ili ashindwe kuiendesha operation yake yake, unajua baada ya urusi kugundua kuwa west wameshanasa akifanya nini? 😄😄😄😄😄 Ndipo Putin alikwenda China na taarifa zikavuja kuwa urusi imeishiwa silaha na chakula, hapa west wakavimba kichwa wakiona Zama za urusi zinaenda kuisha,

Baada ya west kupeleka silaha nyingi na za kisasa ndiyo muda mzuri mrusi alikuwa ameua ndege wawili Kwa jiwe moja

1) Kwanza alipata kujua technology iliyotumika kwenye kutengeneza silaha zile akaangalia udhaifu wake na pia aliangalia ni Kwa jinsi gani anaweza kuzidhibiti zisilete madhara makubwa

2) Kupitia hili nchi kama Poland ilisafisha ghala lake la silaha lote na kupeleka Ukraine, Kwa namna moja ama nyingine mrusi alisababisha nchi nyingi za ulaya zipunguze hifadhi zao za silaha Kwa kutegemea Ukraine atashinda Vita

Kitu ambacho hawakuamini ni pale mrusi alipoziangamiza zote na nchi nyingi zimejikuta zimeishiwa silaha mpaka zinaomba msaada

Sasa mrusi baada ya kuona jamaa wamekiuka makubaliano akaja na mtego mpya

1) akaweka vikwazo Kwa nchi za EU kuwa wakitaka gas wanunue Kwa rubo, ulaya walivyo vilaza wakaingia kichwa kichwa kwenye mtego wakagoma kulipia gas Kwa rubo mrusi akakata gas, nchi nyingi ulaya wakajikuta wanatumia gas Yao ya akiba Kwa kuwa hawataki kulipia Kwa rubo lakini baada ya siku chache Ile gas ya akiba ikaisha wakakubali kulipia Kwa rubo lakini tayari wameingiza damage kwenye hifadhi ya gas, na mrusi Kwa kujua west wamemaliza gas Yao ya akiba, akaja na mtego wa pili akapunguza kiwango cha kupeleka gas ulaya hii ikasababisha gas wanayoipata ni Ile itakayowawezesha kuishi sasa hivi tu hakuna gas ya akiba

2) baada ya kuona tayari vile zile nchi ndogo ndogo zimenasa akaanza kudeal na nchi kubwa kama ujerumani ambayo ina hifadhi kubwa,
Akafunga bomba la kupeleka gas ujerumani Kwa kisingizio kuwa pangaboi lilipo Canada ndilo linahitajika ili kuweza kufungwa ili gas iende ujerumani, yakaingia mabishano Kati yao wenyewe west na kipindi hicho chote ujerumani alikuwa anatumia gas yake ya akiba mpaka wanakuja kupata muafaka na kufunga bomba mjerumani kashatia damage kwenye hifadhi yake ya gas, kibaya zaidi mrusi akaja na tangazo la kupunguza kiwango cha kupeleka gas ujerumani kutoka 100% hadi 60%, hii maana yake ujerumani atumie hiyo gas bila kuweka nyingine akiba ,
Baada ya kufanikiwa hilo mrusi kaja na njia mpya kila mwezi anafunga bomba Kwa ajili ya matengenezo kipindi hicho nchi za EU zinalazimika kutumi gas ya akiba, lengo kuu la urusi ni kuhakikisha ulaya nzima kipindi cha baridi hakuna nchi yenye akiba ya gas

Sasa ulaya ndiyo wanagundua sasa lengo la mrusi ndiyo maana zimezuka hoja za kuwasha vinu vya nuclear vilivyopo ulaya ili kupata nishati, kibaya zaidi hii mitambo ya nuclear imekaa muda mrefu bila kufanya kazi kwahiyo wanahitajika wataalamu ili kuweza kufufua hiyo mitambo kibaya zaidi hao wataalamu wanapatikana urusi,
Kitu kingine hiyo mitambo inahitaji kufungwa vipuri vipya, ambapo hivyo vipuri vinapatikana Russia
Pia wanahofu kutokana na mitambo hiyo kukataa Kwa muda mrefu bila kutumika kuna uwezekano wa baadhi ya maeneo kuwa yameliwa na kutu na ikatoka mionzi ikavuja,
Kitu kingine ni kuwa hata wakiwasha hiyo mitambo ili upate umeme unaohitaji itabidi wasubiri kama mwaka mmoja, kitu ambacho matatizo waliyokuwa nayo ulaya hayawapi nafasi ya kusubiri Kwa muda huo

Sasa faida ambayo mrusi kapata baada ya hii operation kuchelewa ni

1) kujua ulaya Wana silaha gani na zinauwezo gani, na wamejua ni namna gani wanaweza kuzizuia ili zisilete madhara makubwa

2) kupunguza hifadhi kubwa za silaha zilizopo kwenye mataifa ya ulaya

3) kupunguza uwezo wa NATO na EU kwenye nishati hii inasaidia mpaka sasa kuwa hawana uwezo wa kuzalisha silaha nyingi Kwa wakati mmoja kutokana na upungufu wa nishati WA kuendeshea viwanda vyao vya silaha

4) kupitia vikwazo ambavyo ulaya wamaiwekea urusi nchi nyingi za ulaya zimeyumba kiuchumi na hivyo kupunguza uwezo wao wa kuendesha Vita ya muda mrefu na mrusi

5) mpaka sasa hivi mmarekani kajua wazi kitendo Chao cha kusubiria kumsoma Putin anawaza nini juu ya Ukraine lilikuwa kosa kubwa maana kama sasa hivi vikitokea Vita basi MTU pekee atakayewajibika ni USA Kwa kuwa ameshajua EU na NATO wamekwisha choka yaani hawana uwezo wa kupigana Vita na taifa kubwa kama urusi, Kwa hiyo akiingia Ukraine yeye ndiye atakayeandamwa na akipigwa yeye maana yake ulaya nzima imeanguka

Kiufupi mpaka sasa mrusi yupo kwenye nafasi nzuri ya kupigana Vita hasa muda huu ambao baridi linaanza ulaya, naona kila dalili ulaya ikisambaratika bila urusi kuingia vitani, na ikisambaratika ulaya na marekani inatafata maana bidhaa za marekani zitapigwa ban nchi za Asia na kusababisha marekani akose soko la kuuza bidhaa, na kutokana na hali ya uchumi wananchi watafunga mikanda na hapo ndipo anguko la marekani lilipo
 

Shukrani sana mkuu kwa kuwaelimisha vijana wengi ambao uki-analyse kwa kina utakuta wengi uelewa wao kwenye masula ya Geopolitics ni dismal kabisa - ila ni mabingwa sana katika nyanja za ubishi na hawataki kujifunza kitu, juzi hapa kwa mfano:niliona video clip mbili nikacheka sana moja inaonyesha eti Ukraine MiG-29 ikitungua helicopter ya Urusi, akiangalia clip kwa umakini inaonekana wazi wazi inaendeshwa na flight Simulation Software in other words the whole stuff is virtual not real lakini baadhi ya waswahili wana amini usanii huu, ya pili ni video clip iliyo onyeshwa na msemaji wa jeshi la Urusi kwenye briefing Drone za Urusi zilionyesha wanajeshi wa Ukraine wakianga hika kwenye mahandaki wakikimbia huko na kule msemaji wa jeshi la Urusi alisema drones ndio zinawapatia coordinates ili Howitzers na MRLS ziwalenge wanajeshi wa Ukraine kwa usahihi - na kweli hicho ndicho kilicho tokea, baada ya siku mbili tatu propaganda za Zelensky na wapambe wake wana copy na ku-paste same video clip lakini this time wanageuza maneno kwa kusema wanajeshi walio shambuliwa kwenye mahandaki actually ulikuwa ni mtaro wanasema eti hao ni wanajeshi wa Urusi - Zelensky na jeshi lake ni usanii mwanzo mwisho - sijui anawaza nini? Taifa lake linazidi kupoteza majimbo/miji wanajeshi wanakufa 600 - 1000 kila siku hayo kayasema Zelensky mwenyewe sio mimi, kwa hasara zote hizo bada anataka vita iendelee wanajeshi na raia wapoteze maisha na miji kugeuzwa magofu - wala hajali!!
 
Kwa mwendo huu sijui tunaelekea wapi?

Daah! Mpaka aibu mkuu

Ndio maana wanasiasa wanaweza kufanya watakavyo kwa sababu taifa lina watu wajinga wasiojua kuhoji wala kupambanua mambo
Yeah,it is catastrophic.Mmoja nakumbuka aliuzwa China iko wapi,akasema iko South Africa.

Okay,na wewe nataka niku-challege kidogo,wewe una-fikiri tatizo ni nini,maana zamani nakumbuka wakati wetu vijana walikuwa smart sana kweli kweli.By STD.VI we could speak English fluently and participate in Debating Societies.

Ni vizuri kujua kwamba we were using English Books in all subjects,and by Std.V you wasn't allowed to speak Swahili in School.English was only a subject! Leo kijana anakuambia Kingereza ni kigumu sana,wanasema wenyewe haki-pandi!You wonder,ugumu wake unatoka wapi,mbona ni lugha tu kama Kigogo?No, something is terribly wrong.

Anyway,back to my question,"why do you think today's generation is so dumb?"Na wengine ni hawa hawa humu JF wanaojiita Pro-NATO,they obviously do not know,I mean completely,what they are defending.
 
Tuletee hiyo video boss sijawahi ona video ya jeshi la urusi likifanya mashambulio ya hizi drone ndogo ambazo jeshi la Ukraine wamezi modify na zinaweza kubeba mabomu madogo.Unahangaika tu kukanusha ila ukweli unaujua[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unatapatapa najua zinawakera Pro Russia na nitaongeza speed ya kuleta[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hizi articles ndio Pro Russia wanaona ni independent source[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kweli wewe ni Mr Majanga huu muda uliyotumia kuandika huu UPUPU ungefanya jambo la msingi
 
Jana tu wamepoteza askari 300 lwa loss hii lazima waombe negotiations [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Njoo useme na hii ni video ya Urusi tumekopi kichapo ni kikali mnachanganyikiwa sasa hivi

 
Ubalozi wa Russia umeshambuliwa huko kabul wavaa kobazi nao wanamtunishia msuli Russia [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…