Victor Orban nani asiyemjua. Hiyo sio surprise, vipi mkuu ndugu yenu
Narendra Modi alivyomkaripia Putin aache vita mlijisikiaje na hiyo BRICS yenu mliyokuwa mnatutisha humu eti ndio itakuwa mbadala wa West kwenye biashara.
Na vipi umoja wenu wa CSTO ambao eti ni mbadala wa NATO hadi sasa uko umelala wakati Armenia imevamiwa na Azerbaijan. Na wakati huo wanachama Kyrgyzstan na Tajikistan wako na mapigano. Na muda huo Armenia baada ya kuona umoja huo hamna kitu ameomba msaada wa US, UK na nchi nyingine sijui ni Canada.
Bado China juzi hapo kaihakikishia ulinzi Kazakhstan kwa hali yoyote ile, sasa Kazakhs wanatishiwa na nani kama sio Russia kaka yao wa Kaskazini.
Russia namna gani huyu, dharau kila kona
Victor Orban nani asiyemjua. Hiyo sio.
Dah wewe jamaa wewe!,kwamba Orban kwako wewe si lolote si chochote.kwa hiyo sio mwanachama wa EU? Na Hana haki ya kukosoa au kupinga?
Kwa hiyo wewe unaijua ulaya kuliko yeye?
Narendra Modi alivyomkaripia Putin aache vita mlijisikiaje na hiyo BRICS yenu mliyokuwa mnatutisha humu eti ndio itakuwa mbadala wa West kwenye biashara.
Amemkaripia?
Au amemshauri?
Kwana ushauri wa kuacha vita ni mbaya?
Mbona Kuna Warusi wengi TU pia hawaungi mkono vita hii?
Hata Mimi siungi,lkn je unaweza kujua hofu ya Urusi juu na NATO kuliko Warusi wenyewe? Unafikiri majasusi wote wa Urusi ni wajinga Hadi kushauri Urusi iivamie Ukraine.?
Modi ni rafiki wa Putin,na sio lazima mawazo ya marafiki yafanane.
Kwa hiyo kwako wewe kwa vile Modi "kamkaripia" Putin basi ndo BRICS Haina faida na itavunjika.?
Na vipi umoja wenu wa CSTO ambao eti ni mbadala wa NATO hadi sasa uko umelala wakati Armenia imevamiwa na Azerbaijan. Na wakati huo wanachama Kyrgyzstan na Tajikistan wako na mapigano. Na muda huo Armenia baada ya kuona umoja huo hamna kitu.
CSTO "eti" ni mbadala wa NATO.
Kwani sio kweli ni mbadala wa NATO?
Uko umelala.
Kwani kua na umoja Fulani kunazuia migogolo isitokee?
Migogolo IPO TU kwa sababu ya tabia za kibinadamu.
Unasemeaje juu ya mgogolo wa Cyprus na Greece na Turkey ndani ya NATO?
Au baadhi ya Wanachama wa EU kupingana na vikwazo vya EU dhidi ya Urusi?
Mfano Hungari.
Au mwanachama mmoja wa EU Poland, kumdai fidia ya vita vya mwaka 47 mwanachama mwezie German wa EU.
Au mwanachama mkubwa kabisa wa NATO Turkey kununua S400 kwa Urusi badala ya USA NATO mwenzake?
Na katika kipindi hiki Cha vita yeye Turkey kaenda hukoo kwa akina Urusi kununua gesi na kushiriki mikutano Yao ya SCO?
Na muda huo Armenia baada ya kuona umoja huo hamna kitu ameomba msaada wa US, UK na nchi nyingine sijui ni Canada.
Bado China juzi hapo kaihakikishia ulinzi Kazakhstan kwa hali yoyote ile, sasa Kazakhs wanatishiwa na nani kama sio Russia kaka yao wa Kaskazini.
Russia namna gani huyu, dharau kila kona.
Dah hili nimeshalieza pia huko juu.
Kuwa katika umoja Fulani sio Kinga ya Wanachama kutovurugana.
Mbona Uturuki alizigomea SWEDEN NA Finland zisijiunge NATO?
Au unasemeaje baadhi ya nchi Wanachama wa EU kujitoa EU mfano Brexit,
Au baadhi ya nchi majimbo Yao kutaka kujitoa kwenye nchi mama,mfano Catalonia kujitoa Spain.
Jaribu kufikiri ndugu,sio Kila kitu unapinga TU kwa sababu Urusi yupo.
Wewe huwezi kua na akili kuliko wataalamu wote zaidi ya billion 3 wananchi wa Nchi za BRICS na SCO.
Wasomi watafiti na wachambuzi wa siasa na uchumi wa ukweli.
Wewe mtu mmoja TU huwezi kua na akili kuzidi watu billion 3.