LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Bora zako wewe mwanajeshi (kama ulivyojigamba kuwa sio civilian) ambaye unaijua vita zaidi kuliko hata Defense Secretary wa Marekani General Lloyd Austin ambaye yeye aliongoza vikosi kadhaa ktk vita vya Baghdad. General Austin yeye anasema kuwa Russia bado wana uwezo na nguvu kubwa mno ya kupambana na Ukraine ambayo hawajaamua kuitumia.

Nitakutafuta unifundishe namna ya kuvuja/pasua matofali kwa kichwa ili niende nikatumie ujuzi huo huko Ukraine

 
Mkuu, wanasema dalili ya mvua ni mawingu.
Gharika ya mwisho (hatujui atatumia nini) ya ulimwengu mzima iko karibu sana.
Vurugu kila kona. Ndoa, ushirikina, kuuwana hovyohovyo, ni dalili kuu sana.
Lakini watu bado wanadharau sana.
Yeye Mwenyewe anasema:"Nitajitukuza Mwenyewe mbele ya macho ya mataifa yote. Nao hakika watalazimika kujua kwamba Mimi ni Mungu" Amechoka, subira imefika mwisho.
 
Ila mkuu nimegundua Marekani ni taifa moja lilijaa wana siasa wanafiki ebu ona hapa.View attachment 2138924

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Huo sio unafiki mkuu....diplomasia baina ya mataifa yenye nguvu ipo hivyo siku zote.....'ina usanii mwingi'..

Ndio maana wanasema wapo pamoja na Ukraine ila hawatapeleka jeshi ili kuepusha mzozo wa moja kwa moja na Urusi.

Maadam Ukraine imepakana na nchi wanachama wa NATO, mawasiliano kama hayo ni muhimu ili kuepuka mgongano wa bahati mbaya na Urusi inayoendesha operesheni za kijeshi huko Ukraine.
 
Huwa nakaa nawaza sana kuhusu hizi silaha za nyuklia.

Lengo mama la uundwaji wa silaha za nyuklia ni nini kama kwa sasa dunia yote inamhofia Putin kutumia hayo mabomu.
Binafsi nitamuelewa Putin akiamua kutumia nyuklia endapo ikitokea akazidiwa na NATO + USA.

Kama uundwaji wa hizi silaha ni hatari kwa usalama wa uhai hapa duniani,kwa nini bado tunashindana kuzimiliki kwa wingi wakati tunajua hakuna adui mwingine tofauti na mwanadamu tunapokusudia kwenda kuzitumia? Kwanini tusionyeshane umahiri wa kivita kwa mbinu mbadala kuliko haya madude yanayotishia uwepo wetu?

Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo nyuma kwamba taasisi nyingi za kimataifa ni vibaraka wa USA na NATO,ndio ilivyo UN pia. Baada ya hii vita UN asimamie uteketezaji wa silaha za nyuklia ili wanadamu tusiishi kwa hofu kubwa kama ilivyo sasa.
 
Na bado,tuliwaambia hapa wakatoa povu wakati yeye anatumia maguvu wenzie wanatumia akili zaidi wanabofya kitufe cha sanctions huku wanaendelea kupop champagne.Warusi wa JF wamekazania "Putin ni noma".
Umekuja ku test mitambo!?
 
Na bado,tuliwaambia hapa wakatoa povu wakati yeye anatumia maguvu wenzie wanatumia akili zaidi wanabofya kitufe cha sanctions huku wanaendelea kupop champagne.Warusi wa JF wamekazania "Putin ni noma".
Kwanza BBC na Nyamizi nyie wote mnajitekenya na kucheka wenyewe. Urusi anakila kitu kwenye dunia hii endeleeni kumwombea mabaya ila sisi tupo pamoja na yeye.
 
Daaaah!! Naona Putin anavyopasua Vichwa vya wakubwa wenzake huko. Naona shirika la nguvu za Atomic ghafla limekaa kujadili nuclear site iliyovamiwa na Russia, sijakaa sawa naona Marekani na EU wanaliongelea.

Kweli nuclear inatisha
 
sorry mkuu unasema ulifika marekani . VP umewah fika na Russia?.
Ha ha ha,Russia aende kufanya nini,akiambiwa achague aende wapi hata sasa atakimbilia US.Wakiwa hapa JF wanaiponda US lakini ndiyo hao hao wanakuja kututambia humu kuwa wameshafika Marekani,sasa sijui kila mtu akianza kusema sehemu alizofika au anapoishi sijui hapa patakuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…