Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Siku ukielewa kwa nini kuna West domination na wao ni block yenye nguvu zaidi duniani utakuwa umechelewa sana.

West wana nguvu na ushawishi mkubwa duniani kwa sababu wana teknolojia kubwa kuliko kwingine kokote duniani, hiyo teknolojia imewafanya kuwa na uchumi mkubwa kiasi cha kutoa misaada na mikopo kwa matrilioni kwa watu maskini kama nyie.

West wana ushawishi na watu wanakimbilia huko kwa sababu huko kuna demokrasia na uhuru mkubwa wa raia kuliko sehemu nyingine duniani. Ndio sababu unaona Waarabu, Wa-Irana, Warusi wanakimbilia na kuficha pesa zao huko.

West wana ushawishi kwa sababu watu wanapenda utamaduni wao kuanzia lugha, mavazi, muziki, movies, vyakula, vinywaji n.k ndio maana unaona kuna Pepsi, Coca-Cola, Starbucks, KFC, McDonald's, Burger King hadi Russia lkn huwezi kukuta kinywaji kingine cha Kirusi zaidi ya vodka huko US. Wengine hapa wanaoitukana West wako wanakunywa Pepsi baridi sasa hivi baada ya kumaliza kula supu.
Kaangalie kwenye charts za uchumi mfano tano Bora nchi nyingi ni za asia.huu ndo mwisho wa west domination
 
Russia wengi ni Wa- Orthodox, China wengi hawana dini, wengine wako na folk religions zao, wengine ni Wabudha n.k, Marekani wako watu wa dini zote kubwa duniani sasa watu wa aina hii hilo "lao moja" ni lipi??
Watu huko wako wengi wao hawana hata muda wa kuwaza huu utopolo wenu wa NWO, wako bize wanafanya kazi usiku na mchana kama mchwa kupata pesa za kuja kuwakopesha watu wenye akili ndogo wanaolia na kufikiria West domination ndio adui yao, ila Hiyo West haikuifanya Korea Kusin, Japan, Taiwan, Singapore na China kuwa mafukara[emoji16]
We unaishi dunia Gani top 5 yote ya uchumi nchi za Asia zipo 3 .nakushauri katafiti vizuri.viongozi wa huko wanaongelea Hilo Jambo kila mara na nikakupa evidence hapo juu amka.kwanini waongelee kama hamna kitu kama hicho?
 
Mnamkumbuka yule kima wa jana aliye dai Estonia inajitosheleza umeme utafikiri yeye ndie waziri wa nishati nchini humo 😂😂. Waswahili sie ni mwisho wa reli 🤗

Soma hiyo....

🇪🇪 After the Prime Minister's speech, Estonian residents rushed to buy electric generators.

Earlier, Kaya Kallas announced the possibility of power outages in the country.

"The Prime Minister is a great salesman. Today we have sold more than 100 electric generators. This is more than in the last four months," ERR quotes the words of the manager of one of the stores.

But that's not all.

Estonians have become more active in buying dry food, animal feed, personal hygiene items, flashlights and batteries.

"In other words, people started stocking up."

There are also more piquant problems. You should be ready to turn off the sewage system, said the expert of the Rescue Department Mikko Virkala.

"If need calls, then there is a solution. Take a large garbage bag purchased in advance, install it on the toilet under the toilet seat. If there is a cat at home, then you can fill the bag with cat litter. After that, you do your business in the bag and seal it with duct tape," Virkala said.
 
"The West is a series of institutions and values. The West is not a geographical place. Russia is European, but not Western. Japan is Western, but not European. “Western” means rule of law, democracy, private property, open markets, respect for the individual, diversity, pluralism of opinion"
-Stephen Kotkin
Sasa kama ni za kweli nifanyeje,niziache kwa kuwa ni za Russia?Kwa bahati mbaya taarifa zote za the West ni fake,and is by design.Cheki comment ya boss was CIA hapo chini.You cannot be more realistic than a former CIA Director.

NB:Replace American public for World Citizenry.
 
"The West is a series of institutions and values. The West is not a geographical place. Russia is European, but not Western. Japan is Western, but not European. “Western” means rule of law, democracy, private property, open markets, respect for the individual, diversity, pluralism of opinion"
-Stephen Kotkin
[emoji122]
 
NATO is supplying the Ukrainian military with huge amounts of winter uniforms.
SmartSelect_20220924_094113_Twitter.jpg
 
Professorial Rubbish,
Akili zenu ndogo ndio zinawaamisha ukiwa na mafuta tu basi unakuwa muhimu sana, hizo ni akili mgando. Dunia inatawalia na teknolojia na capital, sio rasilimali. Ndio maana unaiona Japan, Korea, Israel na Mataifa mengi sana ya Ulaya ambayo hayan hata tone la mafuta yana ushawashi mkubwa sana duniani kote.

Hakuna watu waliokaa chini mafichoni wakatengeneza vita au vurugu kati ya Waarabu au jamii za Mashariki ya kati eti kwa sababu ya mafuta, ni ujinga wa kiwango cha lami kufikiri hivyo kwa sababu Lebanon wala hakuna mafuta ila kila siku ni kutwangana, Afghanistan ambapo Taliban na Al Aqaeda wanachinja watu hakuna mafuta. Yemen na Syria kuna vimafuta vya kwasha vibatari tu.

Kama US angekuwa ndio chanzo cha hivyo vita vya waarabu kwa sababu ya mafuta nchi ambazo zingepaswa kuwa vitani leo hii ni Saudi Arabia, Kuwait, Qatar na United Arab Emirates.

Halafu kwa nini US asilete hiyo migogoro Mexico au Canada zilizojaa mafuta pia na ambazo ziko pua na mdomo??! Jaribuni kutumia akili zenu kufikiri badala ya kuvukia barabara tu.
Mkuu Ulichosema ni kweli kabisa, kingine Cha kuongezea huyo mtoto Yoda akafanye research pamoja na wenzake pro USA/NATO/UKRAINE katika hii issue ya BILDERBEGS ARC OF CRISIS.

Ilikuwa mwaka 1979 mkutano ulifanyika Austria huu ulikuwa mkakati wa kuhujumu mataifa ya Mashariki ya kati(hasa ya kiarabu) pamoja na Eurasia ( ulaya Mashariki na Asia ya Kati na Kusini) kwa malengo ya kuyacontrol mafuta na kuishughulikia urusi. Hapa unakutana na mwanasiasa shetani kabisa ambaye Leo hii ni Mzee kabisa bwana HENRY KISSINGER.

Humo unaona ni jinsi gany mwarabu anavyoshughulikiwa kwa mafuta na dini yake ambapo na urusi anadhibitiwa kupitia majirani zake na wateja wake wa natural resources Kama mafuta. Ambapo hii ni mipango ya nyuma na Leo yanatokea kabisa.

Watu wakiona kwamba tunapinga mambo yanayofanywa na marekani na washirika wake wanafikiria sie tunamatatizo kumbe wao ndio wanashida vichwani mwao either kwa kutokujua ukweli au kuujua na kuikataa kwa makusudi. Kingine kwa wale wanaomini China ni adui wa marekani nawaonea huruma sana huko China kuna familia moja inaitwa li bloodline wale wanaofatilia mambo wanajua what I mean napia uchumi wa China muuangalie sana kwa jicho la tatu, ngoja niishie hapa mambo yasiwe Mengi na kuharibu lengo la hii thread.
 
Mnamkumbuka yule kima wa jana aliye dai Estonia inajitosheleza umeme utafikiri yeye ndie waziri wa nishati nchini humo 😂😂. Waswahili sie ni mwisho wa reli 🤗

Soma hiyo....

🇪🇪 After the Prime Minister's speech, Estonian residents rushed to buy electric generators.

Earlier, Kaya Kallas announced the possibility of power outages in the country.

"The Prime Minister is a great salesman. Today we have sold more than 100 electric generators. This is more than in the last four months," ERR quotes the words of the manager of one of the stores.

But that's not all.

Estonians have become more active in buying dry food, animal feed, personal hygiene items, flashlights and batteries.

"In other words, people started stocking up."

There are also more piquant problems. You should be ready to turn off the sewage system, said the expert of the Rescue Department Mikko Virkala.

"If need calls, then there is a solution. Take a large garbage bag purchased in advance, install it on the toilet under the toilet seat. If there is a cat at home, then you can fill the bag with cat litter. After that, you do your business in the bag and seal it with duct tape," Virkala said.
😄😄 wanye kwny mifuko tu hamna namna tena.
 
Wewe nipe kwanza ushahidi hakuna Sungura anayezungumza kama yule wa kwenye hadithi za Abunuwasi.

Hakuna siku dunia ya watu bilioni 8 wengine wenye akili fyatu kama nyie Pro-Russia itakuwa chini ya dini moja au serikali moja.

Hakuna kiongozi, tajiri au mwanasayansi yeyote wa Magharibi ambaye anafikiria huo utopolo wenu. Watu huko wanaumiza vichwa na kuchakarika kuwaletea Google muendelee ku google vizuri utopolo wenu, muziki, movies, vitabu, Stralink, magari, meli, dawa, chanjo soda, vifaru, na kila kitu ambacho mnatumia huku mkipayuka na kudanganyana kizombi kwamba mnataka kumalizwa nyie mafukara.
Kuhusu dini ni ngumu sababu ni suala la imani,ila serikali moja inawezekana. Kama miaka ya nyuma palikuwa na vieneo vidogo vidogo vya machief na falme na sasa tuna serikali basi huko mbeleni uwezekano upo wa kuwa na serikali zinazowajibika kwa serikali moja. Na teknolojia inavyokua ndivyo urahisi unavyoongezeka. Ni suala tu la wenye nguvu kutoka nchi kubwa kubwa kuamua kula keki ya dunia kwa pamoja badala ya kuwagawana vipande vinavyoitwa nchi. Hapo unakuta watu watachangamana sana na kuzaliana bila kujali huyu ni mchina, mhindi au mzungu sababu suala la mipaka halitakuwa ishu.

Mfano TZ sasa hivi makabila tumeshachanganyika kwa kiasi fulani, tunapoelekea hata lugha za makabila watoto hawajui. Miaka ya nyuma haikuwa raisi mgogo kwenda uchagani na kutwaa mke.
 
Leo nilikuwa naangalia BBC news walikuwa wanafanya mahojiano na jeneral mmoja wa jeshi la Israel alisema tatizo la Urusi ndani ya Ukraine ina upungufu wa Askari na Urusi imelitambua hilo ndio maana wameamuwa kupeleka jeshi la akiba ili kutatua tatizo hilo.

Anasema mpaka sasa Urusi ina wana jeshi 150,000 tu ndani ya Ukraine wakati imeteka eneo kubwa ambalo ukubwa wake ni nchi kama Ureno au Hangary akaongeza kusema eneo lenye ukubwa wa namna hiyo hauwezi kulidhibiti kwa idadi hiyo ya Askari ni wachache.

Akatoa mfano wa shambulizi la ghafla lililo fanywa na Ukraine kwenye mkoa wa karkiv akasema wanajeshi wa Urusi kwenye mkoa huo walikuwa 2500 wakati wanajeshi wa Ukraine walikuwa walikuwa zaidi ya 15,000 kwa hiyo wana jeshi wa Urusi hawakuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyuma maana wangeamuwa kupambana wangezungukwa na hii ingekuwa hasara kubwa ya kimkakati.

Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa Ukraine inanufaika na wingi wa wapiganaji.

Alipo ulizwa ni kwa nini Urusi imeamuwa kutuma wana jeshi wa akiba badala ya kutuma wanajeshi kamili, akajibu ya kwamba Urusi inalinda nguvu zake za kijeshi maana ina mpaka mikubwa inayo hitaji ulinzi, na bado ina maadui wengi ,kwa hiyo hauwezi kuelekeza nguvu zake zote ndani ya Ukraine.
Alafu akamalizia kwa kusema kuwa Urusi bado maghara yake yamejaa siraha za kumuwezesha kupigana kwa muda mrefu.
T14 Amarta ni zaidi ya huyo Gen wa Israel.
Ambae kwangu Mimi amaweka ukweli usio na punje ya uongo.
Watu wenye akili tunajua hilo,ila tunawaacha makamanda wa NATO base ya Jf waseme Yao.
 
Bila counteroffensive saivi Kharkiv pia ingekuwa ktk huu wizi unaoendelea huko donbass kherson na kwngneko kunapokaliwa na mvamizi
Kwani HIMARS na NASMS hazikusaidia kuzuia huo wizi
Si zilikua zinashambulia sana au zilikua kelele tu za media zenu uchwara MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumezoea kuona vibaka wakikwapua mikoba na simu za watu na kuwatishia visu ama bisibisi wahanga, putin nae anafanya vivyo hivyo wafanyavyo vikibaka, anakwapua Ardhi ya watu na kuwatishia nyuklia.
Dunia isimame kupinga udharimu wa Putin.. Hatupo katika dhama za akina Neo.
Mnaanza kuionea huruma sasa UKRAINE eeeh
DUNIA si mlisema iliungana kuiekea vikwazo RUSSIA ama kuna dunia nyengine mnayoitaka iungane
DUNIA pia iliungana kupeleka HIMARS JAVELINE STINGERS cjui namadudu gani mengine bado mnataka DUNIA ipi tena iungane
Tulikua na tunaendelea kuwaambia njia pekee ya UKRAINE na shost zake kumshinda RUSSIA nikuungana na kuingia direct vitani na RUSSIA hapa nazungumzia NATO au UKRAINE akubali matakwa ya RUSSIA
Huku kulalamika lalamika hakutasaidia kitu mzeee kikubwa akimaliza huku atatafta kwengine ili aoneshe UKUU wake ulivyo
Aliushiwa chakula akaishiwa silaha akaishiwa morali bado mnalalama
Hatupendi vita na tunajua UKRAINE anaonewa ila tunajua RUSSIA dude kuuubwa sana
Sema acha UKRAINE wapigwe wali wameyataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujaelewa, basi uwezo wako hauruhusu, na siwezi kukusaidia kitu chochote.

Yes angalau wewe, ingawa ni chongo, alas tutaenda hivyo hivyo. Kuna term deterrence kaifwatilie. Kutokusaidiwa kwa Mexico kuwaonyesha uimara.
Hujajibu swali
MEXICO alipewa msaada nanani MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom