Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Drones za Uturuki hazijapungua ufanisi bali waliamua kutotoa clips zake zilizokuwa zinavujishwa na operators kinyume na amri za kijeshi. Video nyingi za Bayraktars zilikuwa hazitolewi kwa ruhusa. Mpaka sasa Ukraine imedhihirika imepoteza drones 8 wakati Russia imeharibu nyingi kuliko zilizopo.

Marekani ilipeleka Switchblade chache. Hilo la Iran kupeleka silaha kwa makundi nalijua, ila advanced drones za Iran hazitoi. Hao Houthi na Hezbollah wanafanya pia production wenyewe. Sio hivyo tu, hata Alibaba kuna UAV zinanunuliwa na Ukraine na zinatumika kwenye mashambulizi tena ndani ya ardhi ya Russia
 
Mbna hamna kulialia MKUU hapo pakutaka tuone ndio muda huu sasa tunaona
IRAN tayar anatamba huko kuliko hao ambao uliwaeka mbele yako hapo awali kama hao TURKEY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nilikuwa nasoma kitabu cha Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama kiitwacho A Promised Land nikashangaa kuona kumbe mfumo wa usalama wa makombora ya nuclear ya Urusi umejengwa kwa masaada wa USA na wameshiriki katika ujenzi wa mfumo huo. Kama hiyo haitoshi viongozi US na maafisa mara kadhaa mamekuwa wakitembelea sehemu yalipo fichwa makombora hayo. Kwa hilo tu nafikiri vita ya nuclear haiwezi piganwa ndani ya kalne hii.
 
Sasa wanatengenezaga ya nin kama wanaogopana hivo
 
Kuna asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania ni jobles....Hayo makampuni ni bora yaje tu na huku.....hawa panya road wote hawa...kuna vijana waliopitia JKT wanazurula tu mitaani huku jobles...bila shaka kwa hii manpower isiyotumika Tz...makampunu yaanzishwe tu....kama ambavyo kuna utitili wa kampuni za ulinzi siku hizi....
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Patamu hapo

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Hii dunia ina siri nyingi sana brother, huwezi amini pamoja na vita inayoendelea lakini bado vikao vya kila wiki kati ya Pentagon na jeshi la Rusia vinaendelea kama kawaida wanakunywa ma kahawa pamoja
Tafuta movie inayoitwa "Thirteen days" inayoelezea mgogoro wa Cuba wa US dhidi ya Soviet (Russia) hadi kufikia hitimisho la kidiplomasia la kuondoleana silaha za nuclear mipakani mwao.

Hii movie ni ya US wenyewe! Ukiitizama hii movie kwa hatua inayofikia ya mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi kufikia pahala kwa hatua chache watangaziane vita ni suala gumu na linalotisha mno!

White house wanapoteana, Pentagon wanapoteana na vyombo vyengine vya usalama wanapoteana! Na kwenye hiyo movie wankuonyesha kwa nini wanapoteana! Kwa sababu mpinzani unaetutumuliana misuli naye si kwamba utamuadhibu bali mtaadhibiana ya kwamba: Tukiishambulia Soviet(Russia) US haitobaki salama na Soviet (Russia) ikiishambulia US nayo haitobaki salama na inayozungumziwa hapa ni nuclear.

Hatua ambayo iliyofikia Soviet ikawa haijibu suala lolote kupitia balozi yake US wala Kremlin; taarifa hazitoki kwa wakati Taifa jengine linashindwa lichukue maamuzi gani! Tuangie kwenye vita ama la! Lakini jawabu linabakia palepale ni nuclear! Kwenye hii movie inaonyesha haya mataifa makubwa yanapoona usalama wa nchi yake upo hatarini watakuja kufanya maamuzi magumu Sana na kwa misingi hiyo ni vizuri waheshimiane kwa misingi ambayo kwa kila mmojawapo ataona yupo salama kwa Taifa lake.

Kwa bahati mbaya US na NATO na EU wanajaribu kuuvuka huu mstari kwa Russia. Inatambulika na kufahamika Ukraine niTaifa huru. Lakini kuutumia Uhuru na demokrasia ya Ukraine kwa ajili ya kupambana na Russia ni uchochezi. Huu mtanange kwa Russian ni kufa na kupona kwao wanaona ni kutetea na kulinda Taifa lao. Kwa namna yoyote ile ikiwa ni mchezo wa hatari sana.

Na ndiyo maana wasomi wa US wanawaasa wanasiasa wao hususani wa sasa hivi wasome historia.
 
Ni upuuzi gani huu umeandika [emoji848]
 
Walizibeza lakini sasa hivi zinawapeka mputa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…