Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Okay, njoeni tuongee scenario ambapo mrusi kapiga bomb ya Nyukilia wananchi wa nchi gani wataumia zaidi. Nikisema nchi gani, namaanisha nchi zote zinazopatikana hapa Duniani. Kwanza nchi ambazo zina public bunker nyingi ni Usa, Russia na ulaya pia wananchi wake walishapewa mafunzo nini cha kufanya pale vita vya nyuklia vitakapoanza, hivyo tunahitimisha kwa kuona wananchi wa hizi nchi watakuwa na nafasi ya kupenya chujio la nyuklia tofauti na nchi nyingi za Afrika na Amerika kusini.

Wote tunajua ubora wa public service ulivyo, hivyo bunker za public ni za kiwango cha chini sana hivyo hizo ni kwa wananchi wa kawaida. Wenye pesa nyingi hasa hizi nchi za kibepari wao wana bunker zao special, tena sio bunker bali ni luxury bunker. Na kampuni zinauza room zikijinadi kwamba kuwa tenant kwenye bunker yao basi utakuwa miongoni mwa watu wa mwisho kabisa kufariki endapo janga kubwa likiikumba dunia, kama vita vya Nyuklia. Kwenye hii point tunaona raia wa west wengi wataishi kwa luxury kuliko hata raia Oligach wa urusi wakati WEWE NA MIMI tukisaga meno.
Kwa wananchi wa Marekani, kwanza kuna jamii kabisa wanajiita prep wenyewe wanajiandaa na janga, kama likitokea unakuta mtu ana akiba ya msosi na mahitaji muhimu mpaka miaka mitano. Mbali na hivyo kuna makampuni mengi ya kujenga bunker kulingana na fedha zako tuu pua kuna course kibao za survival raia wanajifunza. Hivyo hii jamii wataishi normal.

Tuje kwetu Africa na wale waunga mkono putin. Ivi wewe mwafrika mwenzangu utaenda bunker ipi kujificha from radiation fall out, embu niambie wapi utapata mask kuchuja radiation practical pale upumuapo? Kama hutambui jua ya kwamba tokea test ya mabom ya nyukilia yaanze, viumbe hai wote tuna a very very small doze ya radiation practical, na wanasayansi wanaweza kujua huyu alikuwa before nyuklia bomb or after kwa sababu tuna trace za hizo practical. Wenzetu angalau wanaweza ata ingia underground railroad na kutulia, sisi je? Ivi mnajua bunker ya putin ina supply mpaka za mwaka gani ? Au mnashupaza tu shingoo zenyu? Ivi kwa nini uzurike wewe kwa manufaa ya watu wengine? Ndio maana west wanasema kutumia card kwamba nina mabom ya nyukilia inaonyesha hauna utimamu wa akili, yaani ujeruhi watu wengi kisa tu hupati unachotaka? Kwani ni binadamu gani kapata vyote anavyotaka kwenye huu ulimwengu? Jee kila mmoja angechukua maamuzi kwa kuwa kakosa alichotaka tungeishi kweli?

Unakuta mwafrika anaweka twakwimu za kombora za nyuklia kati ya urusi n west alafu anafurahia urrusi kuwa nayo mengi, MWANAWANE mrusi akipiga ata nusu tuu utajificha wapi?
 
2 Millions Barrels per day mbona ni parefu sana aiseee.

Hii sasa ni hali ya hatari mbona.
Jamaa wanataka Marekani atoe Mafuta yake ya reserve yaingie mtaani(kuwauzia EU na dunia),US nayo haitaki reserve yake kuguswa.

To be an enemy of America can be dangerous, but to be a friend is fatal.”— Henry Kissinger
 
Russian Deputy Prime Minister Novak arrived at the OPEC secretariat in Vienna, where the OPEC + alliance negotiations on an oil deal will be held - the possibility of a new production cut is being discussed
Wanasema tu ,Hii vita imekuja wakati sahihi .After two years mtashangaa Ulaya itakuja na solution na ndipo hizo nchi zitakapoanza kulia.Hulka ya binadamu akishajua tatizo hulitatua na kuachana na cha mwanzo.
 
Kwani hii sio Vita kamili?....

Kuna 'special operation' inayochukua miezi 7 inayohusisha mpaka 'recruitment' ya jeshi la akiba ?

miss ngaboru
Kwa mujibu wa wenyewe russia hii ni SMO. ndio maana hata mkuu wa majeshi anapotoa taarifa anaanza kwa kusema .......continue with special military operation in kherson.....

Kama ulimwelewa @qub
Mkuu Mag3 i have much respect kwako mkuu. Nakujua vizuri kupitia hapa jukwaani. Una uelewa mkubwa wa mambo. Lakini hili la Special Military Operation inayoendeshwa na Russia kule Ukraine mzee unaonyesha mahaba zaidi ya uhalisia. Labda kwa sababu unaishi huko. Us babby😁

Hii SMO kiukweli haikwenda kama ilivyotarajiwa. Na naamini Russia walitegemea kuwa nyepesi, lakini ikawa kinyume chake. Ndio maana Majeshi ya Russia yalianza moja kwa moja msafara wa kwenda kiev wakiamini kabisa hawatakutana na upinzani mkubwa. Hii lilikuwa kosa kubwa. Sasa baada ya kujiondoa kule kiev na kurudi kule donbass kwenye majimbo ya Lughansky, Donesky, na kherson wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa japo wanapata upinzani haswa baada ya introduce ya HIMMARS. Lakini pamoja na upinzani russia wanaopata nakuakikishia kwa 500% Ukraine hawezi kushinda na siku ya mwisho russia ataibuka mshindi. No matter how long hii operation itachukua.
Mwisho kabisa itakuwa hivi.

Ukraine will not remain the same before SMO
Ukraine itaongozwa na viongozi watakao wekwa pale na Moscow. Watafanya kile Nini Moscow wanataka.
EU itakuwa imevurugwa. Haiwezi kuwa kama hii iliyopo sasa.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa litafanyiwa mabadiliko makubwa.
 
mmeamua kucopy hadi kirusi kabisa
Naambiwa walisomea Urusi kama yule Dr. Shika (RIP) Hivi Inakuwakuwaje hadi kijana anaamua kwenda kusoma Urusi? Ili iweje? Ili uwe translator? Halafu wanadai wana analytical minds, really? By copying and pasting Russian propaganda? In Russian? On the contrary that is called synthetical mind!
 
Kwa mujibu wa wenyewe russia hii ni SMO. ndio maana hata mkuu wa majeshi anapotoa taarifa anaanza kwa kusema .......continue with special military operation in kherson.....
SMO indeed! Hivi hiyo SMO inatakiwa ichukue muda gani ama ni mpaka washinde? Kumbuka huu ni mwezi nane toka watangaze SMO. The guy played his card wrong, alidhani na safari hii yatakuwa yale yale ya Crimea! Alionja asali akaamua kuchonga mzinga. Please take my writings with a light touch maana saa hizi kuna watu wanasonya wakisoma haya...the Putin apologists!
Don't get me wrong dear, siyo mahaba yangu kwa USA, hapana, there you are wrong. Ni chuki yangu dhidi ya wannabe dictators like Putin. Kiongozi gani hutaki mawazo mbadala, unataka wewe tu usujudiwe? Uko tayari hata kumuua aliye na ujasiri wa kukukosoa!

I hate authoritarians wherever they may be and in whatever form. Niliwahi kuishi na rafiki yangu, Mrusi wa kuzaliwa aliyelazimika kuikimbia kwa sababu ya Putin. Alinisimulia why he had to disagree with his own parents and disown them. Mbona nilitoa machozi!

HItler alianza hivi hivi, akamega hapa na mara kamega pale na baada ya kunogewa akataka aimege dunia nzima. Kwetu hapa Idi Amin Dada wa Uganda alimega Kagera na mara akataka kumega na Mwanza. Alivurumishwa kama Putin anavyovurumishwa.

Jioni njema ndugu yangu.
 
Ukraine will not remain the same before SMO
Ukraine itaongozwa na viongozi watakao wekwa pale na Moscow. Watafanya kile Nini Moscow wanataka.
EU itakuwa imevurugwa. Haiwezi kuwa kama hii iliyopo sasa.
Ukraine hii ya Zelensky iliyomzuia Putin kuteka Kyiv au unaongelea hayo majimbo yaliyokwisha kumegwa ?...

Kumbuka hata hayo majimbo yaliyomegwa hayapo kwenye udhibiti wa asilimia 100 na Moscow

na Kwa counter offensive hii inavyoenda huku misaada ya silaha ikizidi kuongezeka kwa Ukraine, utawala wa Moscow kwenye hayo majimbo utakuwa mgumu mno.
 
OP inakwenda kumalizwa na matukio makubwa. Tukio kubwa la kutisha litarudiaha akili za wanadunia na Op itaisha.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Duh...aisee...hii comment ya ajabu kwelikweli...Kama ulikuwa hujui elimu ya Russia ni miongoni mwa elimu Bora kabisa duniani...Russia inaongoza kwa elimu ya sayansi na hasa physics na mathematics..kwa philosophy pia iko juu....
Elimu ya West nayo ni 'Nzuri' 😂😂 na hasa kwenye maeneo Kama Mt. Kilimanjaro ulivumbuliwa na mzungu...USA ndiyo leader wa demokrasia🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…