Petrodollar ni kitu kimoja Tu na hiyo ni kama tone la bahari , kuna vitu vingi vinavyoendelea kuipa thamani na nguvu pesa ya dollar ($) kuendelea kuwa kama international standard currency ya miamala . Na uzuri umetaja kimoja wapo kwamba ni kwamba central banks zote dunia hii reserves zao ni inform of USD ukiachilia bullions kama gold na silver na hii ilitokana na ule mkutano WA bretton woods ambapo central bankers dunia nzima walikutana ili kutafuta currency ambayo inaweza kutumika kama standard currency kwenye miamala duniani ili kuweka stability katika mifumo ya kifedha duniani hii ndio mkutano ndio ilioipa nguvu dollar kutumika kama inavyotumika mpaka leo hii .
Na kuna sababu why USD dollar ilikuwa selected out of those many currencies , haikuwa voodoo magic au ajali Kwa USD currency kuemerge kama dominant currency mpaka leo .
Sababu moja wapo ni kwamba USD currency ilikuwa backed by gold ( gold standard ) Kwa wachumi Kule USA wanaita hivi ,kinyume na sarafu nyingine ambazo zilikuwa basically ni pieces of paper au fiat currency /currency backed by nothing ,nikiwa na maana kwamba United States central bank ndio ilikuwa ina reserve kubwa zaidi ya dhahabu na dollar 35 zilithaminishwa na ounce 1 ya gold / dhahabu , hivyo kila dollar moja ya kimarekani iliyoexist kwenye mzunguko WA kifedha au kuchapishwa na kuingizwa na central bank ya Marekani ilithaminishwa na kiasi cha ounces kadhaa za dhahabu ambazo zilikuwa Chini ya umiliki WA benki kuu ya Marekani .
Ingawa pia mwaka 1971 Richard Nixon alikuja kuondosha hii gold standard Kwa kutoa sababu kwamba ilikuwa kupambana na international money speculators waliotoshia stability au uthabiti WA sarafu ya dollar ya kimarekani . Na ndio Hilo suala linaloleta mjadala mpaka sasa hata Kwa wachumi na wanasiasa pale Marekani kwamba kitendo cha Richard Nixon kingesababisha watu na nchi nyingine kukosa Imani na sarafu ya kimarekani siku za mbele kwa kuwa kuondoa gold standard kungeifanya USD kuwa kama fiat currencies nyingine ambazo hazijawa backed na anything na hivyo serikali za hizo nchi zinaweza chapisha hizo currencies na kuziweka kwenye mzunguko bila kujali na kusababisha epic inflation na matatizo mengine ya instability katika mifumo ya kifedha nadhani kilichotokea Zimbabwe na Venezuela kila mtu anaelewa ,wale baada ya kubanwa na vikwazo wakaanza kuchapisha pesa kama vichaa na kuziweka kwenye mzunguko inflation na total collapse ya sarafu hizo na uchumi kila mtu nadhani anajua .
Pia kitu kingine muhimu kinachoendelea kuipa dollar nguvu ni Trust ya watumiaji WA dollar ya kimarekani na namba kubwa ya watumia WA USD katika mifumo ya kifedha na miamala hila kusahau mifumo na miundombinu ambayo imeshakuwa established ,mfano hizo visa card ,master card , swift NK ingawa kuna options zake nadhani wachina na warusi wanazo pia versions zao Ila hazijapata trust na ushawishi kuwa na watumiaji wengi so
So conclusion ni kwamba USD itaanguka na kupotea kabisa kama siku moja tutaamka central banks zote /nyingi dunia hii zimedump USd ,pia wananchi na taasisi za kifedha dunia nzima WAache kutumia USd au waloose confidence na USD .Kitu ambacho sidhani kama kitatokea atleast in our lifetime .labda Kwa vitukuu WA vitukuu wetu huko Maana hata hizo nchi za BRICS mfano China ,Russia na wenzake ndio holders wakubwa WA United States treasury bonds / dhamana za hazina ya serikali ya Marekani na hizo dhamana ziko interms of USD kitu ambacho hata wakiamua kuzidump tena Kwa wakati mmoja si rahisi hata kidogo .
Treasury bond ni kama kuikopesha serikali pesa .Sasa central bank of China ni holder mkubwa WA hizo treasury bonds za United States government sasa hawezi kuzidump Kwa wakati mmoja ni kama atakuwa kaloose billions of USD kwenye reserve yake mwenyewe na kuua uchumi wake sasa ni kama kujipiga risasi miguuni mwake na si Chinese central bank anayemiliki hizo treasury bonds za serikali ya Marekani tu,ni benki kuu karibia zote dunia hii yanahizo US government treasuries bond katika reserve balance sheet zao sasa imagine siku waseme wanazidump hizo US government treasuries bond ,hiyo itakuwa chaos na economic collapse kwenye nchi zao pia .Ukiachilia benki kuu ,kina mamilioni ya watu individuals wanamiliki hizo US government treasuries ina Maana nao ni lazima wazidump kitu ambacho si rahisi ,Kwani hizo ni life time savings na mitaji Yao
Na huo ni mfano Tu kukuonyesha jinsi hili jitu linaloitwa US dollar lilivyo kubwa na kutisha . So huu mfumo waliousuka waliangalia probably millennium nzima kabisa ijayo na hizo dynamics zote walishacalculate Kabla hawajasuka Huu mfumo .
So USD bado itaendelea kudominate kama global currency miaka na miaka
[emoji106] thumb up!
Kwa kusummarise USD ina nguvu sasa hv kwa sababu ya vitu takriban vitatu (kwa nlivyoyaelwa maelezo yako pia)
1. Trust for trade. Nchi nyingi still bado zina imani na usd licha ya kuanguka kwa gold std. Hii inawezesha hata nchi mahasimu kufanya biashara bila kuogopa kufanyiana hiyana.
2. USD can buy oil. Hii km sikosei mfalme wa saudia aliwekeana mkataba na FDR 1945 kwamba saudia watauza mafuta kwa dollar in return usd itaipa ulinzi saudia. So demand ya dollar inakwenda sambamba na demand ya mafuta.
3. Kwa ajili ya swift network Excess forex reserves za mataifa mengi zipo in dollar na pia zipo invested in US economy. Hii ni advantage anayopata us kwa mfano by sept 2021 kulikuwa na zaidi ya tr usd 7 reserves za mataifa mbalimbali ambazo wameziinvest us kupitia treasury bonds.
Though sio rahisi lkn mpango wa mchina na mrusi kuiondoa dollar kwenye nafasi yake ni doable. Kuna video mahali nimeona wanazungumzia hili.
1. Urusi ameshaanza kuuza gesi yake na mafuta kwa ruble. Hii kwa kiasi chake imepunguza demand ya dola na kuongeza dd ya ruble kwa baadhi ya nchi (unfriendies) zinazonunua hizo bidhaa kwake.
2. China anatoa mikopo mingi sana kupitia Bri na mpk ss 14% ya mikopo hiyo ameitoa kwa yuan. Experts wanasema anaweza kulazimisha wadeni wake wamlipe kwa yuan kwa kuwapa discount kwenye interest. Bila kusahau wengi wa washirika wa china kwenye bri wanafanya biashara na china so km wakishift kwenda kwenye yuan itakuwa na impact kwa dollar. Pia China kupitia Bilateral currency swap ameshaingia mikataba worth 3 tr yuan na nchi mbalimbali km engereza, south korea, singapore, hongkong, ulaya, russia etc ambazo zitawawezesha kufanya biashara bila kuhitaji dollar.
4. Saudia anafikiria kuanza kuuza mafuta yake kwa yuan pia.
Hizo zote ni dalili kukuonesha kuwa yanawezekana japo sio rahisi jaribu kufuatilia usd kwenye market share imepungua kiasi gani. Of course US hawezi kukubali kirahisi na pia kuna ugumu mwingi. Michezo ya china kudevalue hela yake itamgarimu pia nchi nyingi zina imani zaidi na us kuliko china.
Multipolar world wanayoihubiri mchina na mrusi haitamake sense km still dunia itakuwa na single dominant currency. So nafkiri wanamaanisha multipolar in everything. Tutaona mengi as time goes kushindawa na kushindwa kunategemea na nani mwenye kusukuma kete zake vizuri