LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Siyo Ukraine tu, Russia ataponaje kiuchumi?
 
Putin anashinikiza Ukraine isiwe mwanachama wa NATO ndio maana ameleta mbinu hii ya zaman,anyways kila kiongozi ana maono yake,sidhan ka Vladimir n mjinga mpk Hali hiii ipo
 
Sawa mkuu kwa hiyo udhaifu wa Russia kiuchumi ni sababu tosha ya kushindwa Vita
 
Wakati Ukraine inakuwa Bahari ya Damu Russia itakuwa salama?
 
Putin ukitaka achague mradi wa gas na nord stream 2 au ukraine asain mkataba wa kuungana na nato unahisi atachagua kipi ?

atachagua kuivamia ukraine na kuzuia mkataba.

kitu ambacho hawajui media za marekani,ufaransa,australia,ujerumani na bbc zilizo africa kwa kifupi radio mbao zote zilizopo upande wa nato hata urusi.

"""" alivyozindua avangard hypersonic missile linatoka urus mpaka marekani moja kwa moja na bomu la zurcon ambalo marekani hana" mlitangaziwa nawauliza hii habari mara mbili mbili zaidi zaidi huwa mnasikia habari za kiduku tuuu"

hizo media zinamaongezi ya kuonyesha usupa power kwa NATO countries au kuonysha kama urusi hana nguvu za kufanya lolote au wamesalender.

Nawapa taarifa lugha anayo ongea putin na uchina hamuijui kabisa ? wiki iliyopita uchina ilitoa tamko la kuiunga mkono urusi, belarus walimuunga mkono urusi na taarifa nyingi hamzipati kwa sababu "zinachujwa" ....... na kupewa zenye kuonesha urus si kitu.

Ukitaka ujue urusi ni mwanaume nitakuorodheshea mambo kadhaa hapa :…
1. Rais wa ufaransa alienda urusi kufanya maongezi ili wamtulize lakini alipigwa chini hakuonekana kitu, watu kitu ambacho hawaelewi ni kuwa BIDEN kaharibu sana .

2. Cancellor wa ujerumani kwa kiasi kikubwa ndio kasikilizwa baada ya ziara ya jana ukraine na kwenda urusi leo na putin kasema atapunguza troops kule.

3. Nchi zaidi ya 7 kubwa ikiwemo marekani, wingereza,ujerumani,ufaransa wanamuongelea urusi peke yake .

4. Hivi urusi hamjiulizi kwa nini viongozi wakubwa ndio wanamfata kwenye nchi yake lakini jamaa amewakazia mpaka cancellor wa ujerumani ndio kasikilizwa dunia nzima wanaiogopa NATO chini ya U.S.A kwa sababu ya propaganda.

halafu media za NATO zinavyoripoti et putin anatoa majeshi kama kaogopa vilee au hawezi kuvamia yani watu ni wanadanganywa na media.

kwa kifupi mimi nafatilia maneno ya putin kupita media yao ya RT .
kimachofanya asikurupuke anajua kwamba viongozi wa hii dunia ya leo hawajielewi yeye toka mwaka 2000 kaanza na bush,obama,trump anawajua vizuri hlf huyu biden.

1. BiDEN MGONJWA U.S.A
2. RAIS WA UKRAINE ALIKUA MCHEKESHAJI sio kiongozi mwenye uzto.

3. MACRON NI MTOTO bado hajakomaaa kwa maono ya putin.

KIDOGO KWA SASA ANAWEZA SEMA NA KIONGOZI WA UJERUMANI KWA SABABU VIONGOZI WAKE NI WATU WANAOJUA HISTORIA

KWA KIFUPI CANSELLOR WA UJERUMANI KATOA HOJA YA MSINGI KUWA KWA KIZAZI CHA SASA HAKITAJI VITA KAMA KIPINDI WALIVYO SHUHUDIA WAO ATHARI ZAKE NA KUELEZEA NAMNA WANAVYOTAKIWA KUFOCUS NA UWEKEZAJI.

Putin kamuelewa yule cansellor hata mimi hoja za cansellor wa ujerumani nimeziona zinastahili kupunguza jazba ya Putin.

NB : Putin ndio anaongoza kwa bomu za nuclear duniani msisahau hilo licha ya nchi saba kumtaka peke yake.
 
Hakuna vita serious vitatokea na kama itakuwepo russia ataumia sana, USA itaumia sana halafu third word countries tutalia kilio cha paka shume aliyepigwa jiwe la koo akiwa anajaribu kumeza mfupa wa samaki uliokwama.
 
Umeongea sahihi mkuu, km wanaweza Marekani na wake zake wakomboe jimbo la Cremea au Donbas iliyo chino ya waasi wanaoungwa mkono na Russia ndio vita ya 3 ya dunia ianze rasmi.
 
We jamaa bado hujaelewa hizi siasa za dunia hii zinavyoenda. Hivi hali ilivyo ni muda wa kutaka kukomboa majimbo ili umpe Urusi nafasi ya kupata kisingizio? Marekani hawezi ingia vitani moja kwa moja kwani manufaa yake kwenye hivi vita ni kidogo.
 
Tatizo mkuu ume amuwa kujitoa akili badala yake umeamuwa kuongozwa na mihemko na chuki dhidi ya Russia.

Hapa kinacho angaliwa siyo huo urafiki bali ni lengo la huo urafiki ndicho kinacho iogopesha Russia na ina haki ya kuwa na hofu hiyo.

Ndio una haki ya kuwa na rafiki unaye mtaka ila nikigundua huyo rafiki anataka kukutumia kunidhuru mm na familia yangu sinta jiuliza mara mbili nitakuteketeza mara moja.

Na ukitaka kulitambua hilo leo hii Mexico imkaribishe china au Russia waanzishe ushirika wa kijeshi tuone kama Marekani atasikiliza uho uharo wenu wa sijui Mexico ni taifa huru na lina uhuru wa kuchagua rafiki anaye mtaka.

Eti dunia nzima inapinga?
Nitajie ni nchi gani inayo piga kekele zaidi ya USA na vibaraka wake.

Hata Turkey ambayo ni mwana chama wa Nato emewataka viongozi wa Ukraine kutumia busara maana vita ikitokea atakaye poteza ni Ukraine na si USA na maswahiba wake wanao mjaza upepo.
Mkuu punguza mihemko .
 
We jamaa bado hujaelewa hizi siasa za dunia hii zinavyoenda. Hivi hali ilivyo ni muda wa kutaka kukomboa majimbo ili umpe Urusi nafasi ya kupata kisingizio? Marekani hawezi ingia vitani moja kwa moja kwani manufaa yake kwenye hivi vita ni kidogo.
Sasa mkuu unacho pinga nn na unacho kubali ni kipi?
Maana kwa hoja yako tiyari umesha unga mkono mawazo yangu.
Na ndio maana nikataa hoja yake ya kwamba Urusi ina ogopa kuivamia Ukraine kwa sababu ina ogopa kupingwa na Marekani.

Nilicho taka kumaanisha ni kwamba Marekani hawezi kuweka mamilioni ya raia na uchumi wake rehani eti kwa ajili ya kuitetea Ukraine kwa sababu hana sababu na maslahi ya kufanya hivyo zaidi ya kupeteza.
 
WAAMUZI KTK UBORA WENU

Wengine humu hata mlio wa risas hamuujui, si ajabu bomu kuliona kwa macvo hujawai zaid ya kuona ktk Hollywood movies.

Sas hayo makelele ya kushadadia sjui taifa fulani lina nguvu kulko taifa fulani, unapata wapi hiizo nguvu?

Ktk vita hakuna mshindi, hususan vita vya mataifa makubwa yanayohusisha siraha kubwa za maangamiz.

Acheni ushabik uchwara
 
Vita yoyote itakayohusisha Kati ya USA China au Russia Itakuwa ni ya muda mfupi Sana kuliko inavyofikiria. Sbabau hakuna atakaye poteza mda na visilaha vidogo wapoteze miezi au miaka wanapigana. Mtalala usiku kama wa Leo kesho asubuhi mnasikia Kuna mtu kamwagiwa NYUKLIA NUSU YA NCHI...........Atakayeanza kulimwaga ndio mshindi
 
hao walojiunga hawakua kitisho kama KIEV nandio maana MOSCOW wamekua wazi kabisa kwamba kama KIEV itajiunga na NATO watapigwa tuu
nahata mimi sisapoti VITA ila wakijiunga wapigwe tu tena wapigwe kipigo chakuchakaza
 
We jamaa bado hujaelewa hizi siasa za dunia hii zinavyoenda. Hivi hali ilivyo ni muda wa kutaka kukomboa majimbo ili umpe Urusi nafasi ya kupata kisingizio? Marekani hawezi ingia vitani moja kwa moja kwani manufaa yake kwenye hivi vita ni kidogo.
hrheher
kwakua haya majimbo yalitekwa mwaka jana ama
 
Japo napenda kumbukizi ya vita baridi "cold war" ya miaka ileee..
Na ni kweli iliweza kuleta balance of power.....
Na ninapenda iwepo nchi kama USSR iliyokuwa inamuweka US kwenye "check mate and balance"
Kwa sasa Russia ni "Riot Country" na anajijiua kiwango chake cha nyodo kina ukomo.....
Haya sasa anarudisha majeshi nyuma.....
Mjini Hela....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…