LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Huu uzi mzuri Kama unanpenda hbr za kimataifa adhari za Vita kwa africa Ni zipi ikiwa afrca Hana maslai na kundi lolote hap.
Majibu plz kwa wataalam. Ahamed rajabu Ni mchambuzi mzuri San embu ajitokeze
 
Aivamie Ukraine akose mradi wa gas wa Nord Stream 2?..NATO walishamwambia Putin very clear,hawezi pata vyote,achague kimoja,aivamie Ukraine akose Nord Stream 2 au aachane na Ukraine inversion abakize Nord stream 2.
Unafikiri Putin ni mjinga hivyo akose mradi utaofaidisha genereations sababu ya vita Ukraine.
Kila kitu ni leverage boss sio ubabe wa kijinga mnaoupigania huku usio na kichwa wala miguu.
Leo Sergei Lavrov amesema baadhi ya wanajeshi waliokuwa mpakani Ukraine wameanza safari ya kurudi kambini,Hata satellites za Marekani wame confirm movements za wanajeshi ku withdraw..
Vita sio lelemama aisee
Pia usisahau raisi wa Ukraine ameamua kutafakari upya suala la kujiunga NATO
 
Mkuu yale majimbo yapo chini ya majeshi ya Russia tayari,na si kwamba Ukraine haipigani litakimbia, tayari kuna Jimbo la Donetsk lipo mikononi mwa Serikali ya Ukraine.
Sasa Russia kama ana nguvu kwanini na yeye anashindwa kuiwekea vikwazo US?
This means yeye bado ni Bwana mdogo tu,na ukichapwa vikwazo utawezaje kushinda Vita?
Kwa sababu vita inahitaji Uchumi Bora
Donesk gani iyo mkuu ambayo ipo chini ya serikali?
 
Huyo Hitler alipigwa na Warusi na siyo taifa lingine kamaulikuwa hujui sasa ujue
Urusi akitumia taarifa za kiintelijensia za baba mzazi wa computer Allan turring...bila hivyo huenda matokeo ya Vita yangekua tofauti
 
Nitajie ni lini Ukraine imetishia raia wa Urusi?..
Ukraine anataka uhuru wa kuchagua rafiki bila kupangiwa na mtu,maana ni nchi huru,labda useme hapa Ukraine sio nchi huru na utoe vigezo.
Marekani sio tu anaowapigia Russia kelele dunia yote inamuona mrusi ana sababu za hovyo kutaka kuivamia Ukraine,,strategic area zote kama eastern Ukraine na Crimea ambapo ni door to black sea fleet na baltics Russia ndio anazitawala,leo anataka ku bomb Kyev aue raia wasio na hatia in what grounds??
Kingine shida ni kujiunga NATO sio?,,Ronania,Lithuania,Wazirstan wote hawa walikuwa Soviet members na wamejiunga na NATO,mbona Russia hakuwavamia kwa kigezo hicho hico unachokiita kuhatarisha raia wake?...Tuache kushabikia mauaji kishabiki shabiki
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.

Russia imepeleka zaidi ya wanajeshi 130,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na wakati wowote wanasubiria amri ya Rais Putin Kuivamia Ukraine.

Baada ya Russia kuimega Crimea na Dunia kukaa kimya,Putin alidhani itakuwa rahisi pia Kuivamia Ukraine na kufanya lolote sasa mambo yamekuwa Tofauti.

Uingereza imepeleka shehena kubwa mno ya silaha mbalimbali Ukraine na makomandoo wa kikosi maalumu cha SAS.

Canada nayo imesema haitaiacha pekee yake Ukraine itaipa misaada yote ya kijeshi dhidi ya uvamizi wa Russia. Kwa hiyo Russia inafikia hatua wanaogopa wakijua wazi kwamba kushinda vita kwao itakuwa ngumu mno.

Na hakika Russia ikijaribu kuivamia Ukraine haitashinda hii vita zaidi ya kuharibikiwa kiuchumi. Russia ni nani hasa hata ashinde vita dhidi ya Marekani, Uingereza,Canada na mataifa mengine mengi ambayo yanaisaidia Ukraine bila kuitangazia Dunia.

Mengine yabakie ushabiki tu, lakini Russia haitashinda hii vita na wao wameshaliona hilo.

View attachment 2119949

Huenda nikweli naungana na wewe.

Putin amesema wazi kwamba hataki Ukraine wajiunge na NATO.

Jana wakati anaongea na waandishi wa habari yeye na kiongozi wa ujerumani alisema inaonekana kama amepuuzwa katika hojayake ya kuitaka Ukraine isijiunge NATO.
Kwasababu inchi za ulaya na mshirika wao US wamejiingiza kwenye huo mzozo mazima kwa kupeleka wanajeshi Ukraine na kutoa mafunzo ya kijeshi na vifaa.
Kwa maana hiyo in other way around, Ukraine nikama tayari wapo nato nandio maana NATO wanaungana nae.

Sasa najiuliza kama Putin amesha jua hivyo anasubiri nini kushusha kipondo!!.

Nadhani anawaogopa Us tu hapo vinginevyo angesha fyatua risasi.

Us kuna kitu kinacho watia kiburi ndio maana wanajiaminisha kiasi cha kwenda nchi za mbali kuzuiya mipango ya watuwengine,maana kutoka Marekani mbaka Ukraine nimbali na unavuka nchi nyingitu.

Putin knows what's gonna happen once akiingia kwenye vita na US.
 
Naona walalahoi wa US na Urusi mnatupiana maneno tu bure hapa akati mradi wa umeme wa maji umejengwa chini ya kiwango huko. ( kwamujibu wa mb Msukuma)

Endeleeni kushabikia vita alafu yakwenu yanakwenda hovyo.
 
Wala hauhitaji warheads 5,000 au zaidi kuipiga nchi kama Urusi. Ushindani wa kuwa na mabomu mengi ulikuwa ukifanywa enzi hizo za Cold War kwa sababu teknolojia ilikuwa hafifu.

Unachohitaji kwa sasa ni mabomu machache lakini yenye uwezo mkubwa wa kupeleka madhara kwa adui (high precision). Ukiwa nayo, unapeleka mashambulizi katika maeneo ya kimkakati zaidi yakiwemo majiji makubwa.
Russia anavyo vyote uwingi wa mabomu ya nuclear na mabomu hatar zaid duniani ! Na sio mabomu tu na silaha hatar zaid ya kutosumbuliwa duniani.

Kwanini Iran hawataki amiliki mabom ya nuclear ? Biden aliwaambia american citizen waondoke Ukraine kabla uvamizi haujatokea sababu hatopeleka even a single mwanajeshi kuwa evacuate raia wake na akawaambia being there na tukajibizana risasi na mrusi ina maanisha ni world war tayar.

Do you think Russia ni china kwenye umiliki wa silaha ?
 
Mkuu, siyo kila kitu Marekani inaitangazia Dunia juu ya uwezo wake kijeshi, Kama Russia inaogopa vita kwa sababu za kiuchumi basi huo ni udhaifu tosha wa kushindwa kabila ya kushindwa,ulishawahi kusikia kuwa Marekani inaogopa vita kwa sababu ya Uchumi?
Ndo ujue kuwa Marekani ni Baba lao Duniani [emoji16]
Russia ame suffer enough kwenye uchum na hawez ku risk zaid ya hapo. Vikwazo vingi alivowekewa vimemfanya asiwe na makali kwenye uchumi lakin kwenye uwanda wa vita mkuu yule jamaa si mchezo.
Marekani anatudanganya na propaganda nying ukion analazimisha kitu ujue anataka afaidike yeye.
 
Putin ukitaka achague mradi wa gas na nord stream 2 au ukraine asain mkataba wa kuungana na nato unahisi atachagua kipi ?

atachagua kuivamia ukraine na kuzuia mkataba.

kitu ambacho hawajui media za marekani,ufaransa,australia,ujerumani na bbc zilizo africa kwa kifupi radio mbao zote zilizopo upande wa nato hata urusi.

"""" alivyozindua avangard hypersonic missile linatoka urus mpaka marekani moja kwa moja na bomu la zurcon ambalo marekani hana" mlitangaziwa nawauliza hii habari mara mbili mbili zaidi zaidi huwa mnasikia habari za kiduku tuuu"

hizo media zinamaongezi ya kuonyesha usupa power kwa NATO countries au kuonysha kama urusi hana nguvu za kufanya lolote au wamesalender.

Nawapa taarifa lugha anayo ongea putin na uchina hamuijui kabisa ? wiki iliyopita uchina ilitoa tamko la kuiunga mkono urusi, belarus walimuunga mkono urusi na taarifa nyingi hamzipati kwa sababu "zinachujwa" ....... na kupewa zenye kuonesha urus si kitu.

Ukitaka ujue urusi ni mwanaume nitakuorodheshea mambo kadhaa hapa :…
1. Rais wa ufaransa alienda urusi kufanya maongezi ili wamtulize lakini alipigwa chini hakuonekana kitu, watu kitu ambacho hawaelewi ni kuwa BIDEN kaharibu sana .

2. Cancellor wa ujerumani kwa kiasi kikubwa ndio kasikilizwa baada ya ziara ya jana ukraine na kwenda urusi leo na putin kasema atapunguza troops kule.

3. Nchi zaidi ya 7 kubwa ikiwemo marekani, wingereza,ujerumani,ufaransa wanamuongelea urusi peke yake .

4. Hivi urusi hamjiulizi kwa nini viongozi wakubwa ndio wanamfata kwenye nchi yake lakini jamaa amewakazia mpaka cancellor wa ujerumani ndio kasikilizwa dunia nzima wanaiogopa NATO chini ya U.S.A kwa sababu ya propaganda.

halafu media za NATO zinavyoripoti et putin anatoa majeshi kama kaogopa vilee au hawezi kuvamia yani watu ni wanadanganywa na media.

kwa kifupi mimi nafatilia maneno ya putin kupita media yao ya RT .
kimachofanya asikurupuke anajua kwamba viongozi wa hii dunia ya leo hawajielewi yeye toka mwaka 2000 kaanza na bush,obama,trump anawajua vizuri hlf huyu biden.

1. BiDEN MGONJWA U.S.A
2. RAIS WA UKRAINE ALIKUA MCHEKESHAJI sio kiongozi mwenye uzto.

3. MACRON NI MTOTO bado hajakomaaa kwa maono ya putin.

KIDOGO KWA SASA ANAWEZA SEMA NA KIONGOZI WA UJERUMANI KWA SABABU VIONGOZI WAKE NI WATU WANAOJUA HISTORIA

KWA KIFUPI CANSELLOR WA UJERUMANI KATOA HOJA YA MSINGI KUWA KWA KIZAZI CHA SASA HAKITAJI VITA KAMA KIPINDI WALIVYO SHUHUDIA WAO ATHARI ZAKE NA KUELEZEA NAMNA WANAVYOTAKIWA KUFOCUS NA UWEKEZAJI.

Putin kamuelewa yule cansellor hata mimi hoja za cansellor wa ujerumani nimeziona zinastahili kupunguza jazba ya Putin.

NB : Putin ndio anaongoza kwa bomu za nuclear duniani msisahau hilo licha ya nchi saba kumtaka peke yake.
Hawafuatiliii hizi mambo wako wanasikiliza sana sky news, cnn, wion na nyingine nying lakini hawasikilizi habari pia za upande wa pili.
Ku engage in a war with russia kwa sasa ni kuiweka ulaya yote mashakani kuliko hizo propaganda channel za western bloc zinavyodai. Marekani yuko far huko.
Croatia ashagoma, German mwenyewe mguu ndan mguu nje, hungary ashagoma na nchi kibao zinaona hakuna haja ya kutaka kuingia kwenye vita ambayo waathirika wakubwa ni wao.
 
Huyo Hitler alipigwa na Warusi na siyo taifa lingine kamaulikuwa hujui sasa ujue
unajua back up ya mrusi kumpiga Hitler aliipata wapi?.
acheni ushabiki wa kishamba US ndiye alitia nguvu upande wa Urusi ndiyo maana habari inasomeka hivyo, asingelifanya hivyo habari ingelikuwa kinyume chake.

unajua Japan aliwai Kalia eneo Urusi kimabavu wakati huo anatawala China, ufiripino, Siberia, Taiwan, Hong Kong,Manchuria.

Japan ndiyo mtabe wa huo ukanda, sio hao wazungu njaaa na wauza Vodka.. Japan ikiwa katika ubora wake akakutana jinamizi...
sasa kamuulize Japan nini kilimfanya asiwe interested na vita hadi LEO? na wana siku mahalum ya kusikitika nchi nzima.
sasa hayo yametokea enzi hizo wakati baadhi ya wazungu wa Urusi wanatumia vibatali majumbani mwao unless uniambie toka wakati huo US walisimama kudeal na sayansi ya nyuklia na mabomy yote kwa ujumla ndiyo nitakubaliana na madai yako kua US ni mchumba tu kwa Urusi.
 
Watu wametengeneza silaha nyingi na za hatari lakini kiuhalisia hawatazitumia na badala yake migogoro itasuluhishwa mezani.

Katika dunia ya leo vita ni ghali sana na unapopigana kisha vita vikiisha na uchumi wako unakuwa umesambaratika kabisa na kuujenga tena ni kazi ngumu kushinda vita vyenyewe na haijalishi kama ulishinda hivyo vita au la.

Hiyo scenario ndio kila nchi inajaribu kuepuka bila kujali nchi ni kubwa au ndogo na inapofika hapo ndio maana hata Russia leo hii nimesikia wameanza kuondoa wanajeshi wao kutoka kwenye mpaka wao na Ukraine.

Russia wameona isiwe shida kwani wakiwekewa vikwazo wameona hawana dawa ya vikwazo na wanafahamu athari ya vikwazo vya kiuchumi ni mbaya kuliko kuikalia ardhi ya Ukraine kwa nguvu hivyo naona wanaelekea kukubali yaishe.
 
Taifa la Ukraine ni miongoni mwa nchi zinazomiliki silaha za Nyuklia na makombora ya masafa marefu

Ni taifa kubwa tu la watu milioni 45 kulingana na takwimu za mwaka 2020

Jamaa wana silaha za kila aina lakini wanapigwa biti na mrusi wanaufyata

Kila mtu anaijua nguvu ya Putin na Urusi,lakini nachotaka kusema hapa ni kuwa, kama nchi nyingine tusiwe kama Ukraine

Hata kama ni Russia na manguvu yote ukraine alitakiwa akitishiwa kuvamiwa naye aonyeshe misuli ya umwamba

Taifa la watu milioni 45 sio taifa dogo wakuu ni taifa ambalo linaweza kuwa na uwezo wa kutunisha misuli kwa taifa hata lenye watu milioni 300

Sasa wapo milioni 45 wanakua waoga hivyo na wanaonyesha udhaifu mkubwa,jee wangekua milioni 3 au 4 jee?

Taifa la watu milioni 45 mkiamua kuwekeza kwenye jeshi na uwezo mkubwa mnauwezo wa kulitunishia misuli dola lolote hapa ulimwengu, milioni 45 inakutosha kuwa superpower nawe ukatunisha misuli

Na silaha za nyukilia wanazo lakini wamekua watu waoga hivyo?Vita ikitokea Ukraine wakijipanga wakipigana na Russia hata kama mrusi atashinda lakini wangemuachia russia makovu fulani au kumporomosha kiuchumi,kwamba vita viww virefu vya kufa na kupona.

Ukraine anapitwa hadi na nchi kama Israel ambayo ina idadi ndogo lakini wanatunishia misuli madola makubwa,kila kitu ni kujipanga,Israel sio wengi ni nchi ndogo lakini kijeshi wanajitahidi vipi hao ambao wapo milioni 45 na wamejionyesha dhaifu hivyo

Una makombora ya masafa marefu yanayofika Moscow halafu unatishiwa kuvamiwa?Kwanini usitamke wazi kabisa kwamba ukivamiwa utaishambulia Moscow kwa makombora ya masafa marefu?

Hii nchi ni ya ajabu sana. Mimi kwa hili nasimama na Urusi katika huu mgogoro lakini Ukraine wanafeli sana masilaha yote hayo lakini wameshindwa hata kupiga mkwara tena watavamiwa na hawatafanya kitu,hawa jamaa ni useless kabisa

Ukraine hawafai kuigwa
 
Ukizidisha sana ubabe wapenda amani wanachange mind zao wanaona its time ya kummaliza mbabe so Russia anatumia mfumo wa Hitler ambao ulichokwa mno so Russia inaweza kuwa ndio mwisho wa ubabe wao forever... tena ikija vita basi usimamishwaji wake crimea itakuwa sharti irudishwe Ukraine so ni pata potea kwa Russia
 
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.

Russia imepeleka zaidi ya wanajeshi 130,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na wakati wowote wanasubiria amri ya Rais Putin Kuivamia Ukraine.

Baada ya Russia kuimega Crimea na Dunia kukaa kimya,Putin alidhani itakuwa rahisi pia Kuivamia Ukraine na kufanya lolote sasa mambo yamekuwa Tofauti.

Uingereza imepeleka shehena kubwa mno ya silaha mbalimbali Ukraine na makomandoo wa kikosi maalumu cha SAS.

Canada nayo imesema haitaiacha pekee yake Ukraine itaipa misaada yote ya kijeshi dhidi ya uvamizi wa Russia. Kwa hiyo Russia inafikia hatua wanaogopa wakijua wazi kwamba kushinda vita kwao itakuwa ngumu mno.

Na hakika Russia ikijaribu kuivamia Ukraine haitashinda hii vita zaidi ya kuharibikiwa kiuchumi. Russia ni nani hasa hata ashinde vita dhidi ya Marekani, Uingereza,Canada na mataifa mengine mengi ambayo yanaisaidia Ukraine bila kuitangazia Dunia.

Mengine yabakie ushabiki tu, lakini Russia haitashinda hii vita na wao wameshaliona hilo.

View attachment 2119949
Are you kidding me Putin was KBG director .Huyo ana create story Ukraine started watch Putin
 
Are you kidding me Putin was KBG director .Huyo ana create story Ukraine started watch Putin
kuwa KGB hakufanyi Putin asiwe wa kubebeka, hata Gharib bilali kasomea utengenezaji wa mabomu ya nyukilia ila sasa kaanzisha Ufugaji wa kwale.

kutaja taja majina KGB sijui nini nini vile kusiwatiwshe.
 
Back
Top Bottom