Kama Ukraine akikubali kushindwa Leo hii,maana yake vita itaishia hapohapo.
Urusi haitaendelea kusonga mbele kijeshi.
Wala haitayaachia maeneo iliyoyashilikilia,na ndio kushindwa kwenyewe kwa Ukraine huko.
Ukraine itabidi ikubali kutojiunga na NATO,ndio kushindwa kwenyewe huko.
Ifahamike kuwa silaha za Ukraine kabla ya OP hii kuanza zote zulishaliwa na Urusi,hizi walizonazo Sasa hivi ni kutoka Kwa NATO.
Ikumbukwe kwamba NATO nao wanapunguza silaha zao kwa kiasi kikubwa mno,nao wanaishiwa silaha.
Kwa maana hiyo NATO wako vitani na Urusi kwa kuwatumia wapiganaji kutoka Ukraine.
Kama Zelensky akishupaza shingo askari wake wengi wataendelea kufa na silaha za NATO zitaendelea kuliwa.
Mwisho wa siku hata NATO wakiamua kuingia vitani na Urusi hawatakua na nguvu kama Ile ambayo wangekua nayo kabla ya kuanza kuiunga mkono Kijeshi Ukraine.
Urusi wanapunguza akiba Yao ya silaha na NATO pia wanapunguza.
Tumeshuhudia Canada,Poland,USA,UK na wengine wakilalamika kua akiba zao zimepungua,zimebaki kwa ajili ya ulinzi wa taifa lao TU.
Kadri wanavyoongeza kuipa silaha Ukraine ndivyo Urusi anavyoongeza ukali wa mashambulizi,toka makambi ya kijeshi Sasa ni miundombinu inayoiwezsha majeshi kupigana.
Huu ni uharibifu utakao ilazimisha Ukraine na NATO kuweka silaha chini na wakubali kuja mezani.
Kuna watu wanasema,silaha anazipewa Ukraine ni mkopo atalipa,lakini Ukraine sio wa kulipa Leo wala kesho,itaichukua Ukraine miaka mingi sana kuanza kulipa madeni hayo.