Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mfatilie mvamizi urusi kavamia mara ngp finland hzo mara ngp alizovamia ndzo alzopokea kpgo. Mnaleta mambo ya kijnga sn kwny hii thread kama simba na yanga. Yan mnaamin nato na marekan hawajui kuna barid kali linakuja na kwmb hawajajipanga namna ya kulisaidia jesh la ukraine? Mnadhan nato na marekan hawajui kwmb uwenda urusi anatoka hapo kherson akajpange ili aje kvngne mnadhan wao hawajui na hawajajpanga? Lakn si putin alitangaza mapema kbs wkt urusi wanavamia ukraine kwmb atakayesaidia ukraine kwa namna yoyote atapgika leo imeshndwa nn kuwapga hao nato na marekan maana mpk mnasema nato wana wanajesh wao ukraine kama wapo urusi si atimize kile alichosema sasa, achen ushabk urusi ni mkubwa haina ubish ila ni mdogo kwa nato na marekani, china n mkubwa ila n mdogo kwa nato na marekani ndo maana taiwan ipo salama.

Putin alisema atakaye jitokeza adhalani na kuleta majeshi yake wazi wazi kwamba anasaidiana na majeshi ya Zelensky kupigana na Urusi - mpaka sasa hakuna Taifa lolote limejitangaza kwamba limengia vitani kusaidiana na jeshi la Zelensky ili kupigana vita na Urusi - hakuna.

Sana sana majeshi ya NATO/US wanajificha nyuma ya pazia ya jeshi la Ukraine, wanavaa uniform za jeshi la Ukraine na kwenda front line - wameuwawa wengi lakini Serikali zao wako kimya kabisa.

Sasa mlitaka Putin afanye nini akurupuke tu na kushambulia mataifa ambayo hayajajitokeza wazi wazi kwamba yanataka kupigana na jeshi la Urusi - hizi dhana zilizo jengeka humu kwamba eti sijui jeshi la Urusi lina ogopa jeshi la NATO/US kitu gani kinawafanya muwe na imani kwamba mnacho kifikiria mko sahihi kabisa - lini NATO iliwahi kupigana na a military powerful Nation kama Urusi, China au North Korea lini, sana sana NATO imezoea kuonea nchi ambazo ni weak kijeshi mfano: Iraq, Yugoslavia, Libya,Afghanistan,Syria etc.

Halafu watu wanakuja hapa na maoni ya ajabu ajabu eti Urusi haina lolote sana sana inajivunia missiles zake za thermonuclear basi, as if Amerika haina silaha za nuclear au Urusi kuwa na missiles mabom ya nuclear ni dhambi!!!

Sasa kama mnafikiri NATO/US wana uwezo mkubwa kijeshi kwa nini hawajiingizi kwenye mapigano ya Ukraine moja kwa moja moja badala yake wanaishia kwenye makongamano na maazimio lukuki vitisho tisho vya kitoto na sanctions chungu mzima, mpaka uchumi wao una fikia hatua ya kuyumba - mwisho wa siku wanakwenda kumbbeleza Putin yaishe kwa kupitia mawaziri wao wa ulizi -alianza waziri wa Ulinzi wa Merokani, juzi juzi kafuatia waziri wa Uingereza ambaye mwaka jana alikuwa anajifanya kifaru mwenye uwezo mkubwa wa kumumaliza Putin na jeshi lake - sasa kiko wapi na mikwala yao - wajaribu basi kuivamia Urusi kwa lengo la kumsaidia Zelensky halafu tuone kutatokea nini??
 
Kwamb vita inapigana Urusi ? hoja nyingine ni vichaa ndo wataamini , Ukraine na Urusi wanafanana karibu kila kitu na uzuri vita inapiganwa Ukraine sehem ambapo wenyej wanaish kila siku na wamepazoea
Kwa fikra zako ndogo, unadhani ni kwanini kumekuwa na mashambulizi kwenye miundombinu muhimu ya nishati hapo Ukraine...?? Unadhani ni kwanini hivi karibuni serikali ya Ukraine iliwaonya raia wake kuhusu hali ya baridi inayokuja...??? Unadhani hadi kufikia sasa Ukraine wanamiundo mbinu imara itakayoweza kuwasaidia wananchi wake kipindi cha baridi..?? Hasa miundombinu ya nishati ya gas na umeme iliyofanyiwa uharibifu mkubwa na Urusi..
 
Teh umerudi... Haya tuendelee ila hakikisha uko na data karibu pia make sure katika majadiliano 'A' ibaki kua 'A' na 'B' iendelee kua 'B'. I mean kusiwe na double standard ya hiki ama kile.

Tuanze rasmi!
Kuhusu Soko la Ulaya la Gas...
Hapa sikwambii nani ila nataka kukupa data uzitafakari!

Before 24th Feb, Russia ni top Natural Gas Exporter to "EU", akiwa ana account for more than third ya wote! Russia Natural Gas ni Cheap by 1/4th kuliko ile ya US na ni safe zaidi kwa climate compared ya ile ya US.

It's cheap Russian Gas inayoiweka EU kua competive kwenye soko la dunia in term of uzalishaji. Hivyo utaona issue ya Tax around Europe ni high ila corporates nyingi ziko hapo due to low cost of production ambayo chanzo kikubwa ni cheap energy. Of course ni cheap kutoka Russia!

So what does it mean by replacing Russian NG with others suppliers.

Jibu ni simple, It's High cost of energy ambayo itapelekea high cost of production. High cost of production will sky rocket EU products na kuzifanya kua uncompetitive sokoni. Which in turn will account kwa collapse of EU economy as many companies will head towards countries ambazo watakuwa assured kua na low cost of production hivyo kuweza ku'maximize their profits.

Hiyo ni general view of the situation.

Now tuje in term of figures!

As data nilizo kuonesha juu... Russia ana account more than 3rd, its 43%. while that of US ni less than 8%.

Tufanye mahesabu mepesi kiutu uzima.

Lel say total amount consumed by EU ni 1,000.
[emoji95] Total inayotolewa na Russia peke ake 43% maana ake ni 430.
[emoji95] Total inayokua supplied by US less than 8% ambayo tunaweza sema ni approximately kama 80 hivi kwa mfano wa 1,000 niliotoa.

So US ku'replace Russia hapo EU will need to supply over '510'. That's over 6 times of the current supply anayotoa US kwa Europe!

Maswali unayopaswa kujiuliza.
1. Is that possible? If yes how?
2. What's current production of Natural Gas by US? And how hiyo '530' will be added in current production to satisfy the demand?
3. How big is natural gas reserves anayo US? Will it be secured for a long term?
4. What's current consumption of Natural Gas by US? Je atakuwa na surplus ya zaidi ya kuweza kuendana na hilo Gap la Russia?
5. How about means of delivery from US to EU compared to Russia to EU? Will it be secure and safe to such large amount of Natural Gas required kumtoa Urusi sokoni?

Hayo ni machache maswali ya kujiuliza.

Digest some hints below!

Unajua kwanini inaitwa LNG?
Jibu la hili swali itakupa muongozo wa swali la 5 hapo juu.

Unajua how LNG is transported and stored? Na je hizo resources za kutunzia Gas to such amount zipo EU? Do you know why Russia Natural Gas is cheaper kwa EU compared na wengine? Jibu la swali hili litakupa mwongozo wa swali la kwanza hapo juu.

Je wajua kama US despite being among top Natural Gas producer ila ni miongoni mwa Importes wakubwa wa Natural Gas nchini mwake? Yes cause anatumia zaidi kuliko anacho zalisha.

Na kuweka maelezo sawa kitakwimu ni kua US na China (Each of them) wanatumia higher amount of Natural Gas kuliko collective EU yote.

Najua utajiuliza kama yeye anapeleza kwanini anaenda kuuza huko EU. Yes that's business you sell where it fits your interest! Anauza EU kwa bei mara 4 zaidi ya anayouza nyumbani.

So ana import kutoka Canada, Australia kwa bei chee... Kiasia anabeba anapeleka kuuza EU kwa bei mara 4 zaidi... Why? EU kuna liberal market of energy! Its market that determines price ya energy kwa ujumla. (Kwa jicho pana) tunasema liberal markets are easy to manipulate by imperialists who focus much on profit kuliko service yenyewe!

Sooooooooo... Russia hakosi kitu kwa EU as her Natural Gas are cheap. Hivyo soko lake ni easy na liko on demand! That's why even EU wenyewe wanapigana vikumbo kuikwepa. Up to date keshafanya diversity ya kile kilicho kua kikitumika EU now kipo kinatumika Asia.

Anayekosa au kuharibikiwa ni allies wa US sio Russia. Hata logic ya kawaida tu unasusa wengine wanakula... Utakufa njaa wewe usie jua kupika na usie na jiko.

Russia ana make strategic alliances, Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Just China na India ni soko almost two times ya kile kinachotumika ama kilichopo EU.

So tuzungumze kwa data mkononi!

Huo ni just muhtasari wa kipengele cha kwanza cha swali lako.

Kama umeelewa poa kama hujaelewa poa pia now tukubaliane kuto kukubaliana kabla hatujaingia kipengele cha pili.
Heshma yako MKUU
 
Fatilia vita ya russia na finland nyakat za baridi uone finland alivyomtandka urusi, unadhan ukraine hawaujui huo ukanda wao yan kwmb urusi kwny huo ukanda ndiye mtaalam wa kupgana kwny mabarafu na barid kali au siyo?

Russians waliumbwa na sifa za kipekee za kuhimili baridi?

kwamb Baridi lilipigana vita ?
... hoja murua kabisa. Kuna members humu wana-post utumbo hadi unashangaa huyu ni binadamu au zombie!
 
Nadhani ni mkopo siyo msaada na ndiyo maana hii vita ni ngumu kuisha, maana EU na US hawatakubali kirahisi Urusi ashinde. Mikoa yenye mali nyingi kaibeba, hapo wanawaza hela zao zitarudi VP.
Ule hata mie naamini nimkopo nandio ugumu wa vita kama usemavyo

Niwazi Elensky akitii matakwa ya RUSSIA bila kuamuliwa na mabwana zake itakua pigo kwa mabwana zake maana wameweka kiasi kingi watakua looser

Maana sidhanii kama watalipwa tena kiukweli jamaa wanamuhitajia Elensky kwakulipwa deni lao

Ila hem acha tuone khatma ya hili jambo litamalizaje
 
I am sorry to bring this:

RISHI SUNAK

His father was born and raised in the Colony and Protectorate of Kenya (present-day Kenya), while his mother was born in Tanganyika (which later became part of Tanzania). His grandfathers were born in Punjab province, British India, and migrated from East Africa with their families to the UK in the 1960s
 
Kwa maoni yangu ni kwamba Kiev anakopeshwa either kwa kujua au kutokujua! Maana hata wakati wa Vita yetu na Uganda miaka iyo Siraha tulipewa lakini mpaka leo madeni yapo.
Nashukuru MKUU

Nahaya sio maoni yako ndio uhalisia wenyewe huu

Sasa unaposema US anaongoza kuuza silaha kupitia mgogoro wa UKRAINE va RUSSIA unakua unakosea sana kwa hio kauli yako hapo juu nauhalisia

Yaani hapo ukweli nikwamba US nawenzake wamewekeza mabilioni ya $ kwa UKRAINE kupitia mkopo kwamana hio wanauza silaha ila hawapati faida kwanza kwamuda huu

Faida ya US inategemeana na mwenendo na khatma ya huu mzozo hapa akishinda UKRAINE inakua wazi US na NATO yake watafaidika na zile silaha walizotoa mkopo kwa Elensky (hapa kwenye silaha US kacheza kamari ) na anaomba UKRAINE washinde warejeshe chao

Ikitokea RUSSIA akashinda hii OP inakua hasara kubwa sana sana sanaa kwa US na shost zake maana wanakua wametupa pesa maana wamewekeza ila hawakupata walichotarajia

RUSSIA tayar hapo UKRAINE anavuna faida za SMO maana anazuia maeneo yrnyr rasilimali nyingi na faida nyingi mfano ukanda ule ana kamatia bahari huku MAURIOPOL anakamatia eneo kubwa lenye viwanda vya chuma na kuna kipindi walikua wanasema RUSSIA washaanza peleka kwao sijui kama kweli ama laa ila faida tayar tukienda kule DONBAS jamaa wanajibebea NGANO SHAIRI nk
Kiufupi mpaka sasa RUSSIA kashaanza kula matunda ya SMO ila kwaupande wawest wao wanawekeza wanasubiria final itakuaaje acha tuone


Mwisho :-kwamaoni yangu kupitia hili la silaha US na wenzie bado hawajaanza kufanikiwa nakuvuna pesa kama uliposema kule awali hapa faida ya US na wenzake wataiona baada ya hii vita nabaada yenyewe niwategemee UKRAINE aibuke mshindi la sivyo imekula kwao
 
Baada ya Urusi kushambulia miundombinu ya umeme katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, mji huo na meneo mbalimbali ya nchi hiyo yamelazimika kuingia katika mgao wa umeme huku hatua kali za udhibiti wa matumizi ya umeme kama vile kuzima taa za barabarani zikichukuliwa.

Picha:

IMG_5618.jpg


IMG_5619.jpg

IMG_5620.jpg

IMG_5623.jpg

IMG_5625.jpg

IMG_5626.jpg

IMG_5630.jpg

IMG_5629.jpg

IMG_5627.jpg


Ratiba:

IMG_5624.png
 
Mkuu, sina uhakika kama kuna mpango maalum. Hao wanaotukana wengine kwa maneno kama shoga, senge, mpumbavu, "mazafaka" labda ni watu wanaofurahia kutumia hapa maneno ambayo walikataliwa kuyasema walipokuwa watoto; sasa wanajisikia nafuu wakitumia nafasi hapa ambako wanaweza kuficha majina yao... Kuna therapy kwa matatizo hayo ila si hapa online. Ningefurahia kama Jamiiforums ingesimamiwa kidogo na mtu anayetumia matusi anhepigwa ban haraka. Ila sioni usimamizi huo. Basi tuvumilie, tujaribu kuwakemea bila kutumia lugha yao, menginevyo hatuwezi kuepukana na balaa fulani maishani mwetu.
Umeongea la maana ndugu yangu. Binafsi nimeshalisemea sana hili na hata kuliripoti kwa hao moderators. Katika platforms nyingine kama yahoo, comments mbovu zote hufutwa. Kwa hili la matusi, ni wazi jamiiforum wamelala.
 
Back
Top Bottom