Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Putin alisema atakaye jitokeza adhalani na kuleta majeshi yake wazi wazi kwamba anasaidiana na majeshi ya Zelensky kupigana na Urusi - mpaka sasa hakuna Taifa lolote limejitangaza kwamba limengia vitani kusaidiana na jeshi la Zelensky ili kupigana vita na Urusi - hakuna.

Sana sana majeshi ya NATO/US wanajificha nyuma ya pazia ya jeshi la Ukraine, wanavaa uniform za jeshi la Ukraine na kwenda front line - wameuwawa wengi lakini Serikali zao wako kimya kabisa.

Sasa mlitaka Putin afanye nini akurupuke tu na kushambulia mataifa ambayo hayajajitokeza wazi wazi kwamba yanataka kupigana na jeshi la Urusi - hizi dhana zilizo jengeka humu kwamba eti sijui jeshi la Urusi lina ogopa jeshi la NATO/US kitu gani kinawafanya muwe na imani kwamba mnacho kifikiria mko sahihi kabisa - lini NATO iliwahi kupigana na a military powerful Nation kama Urusi, China au North Korea lini, sana sana NATO imezoea kuonea nchi ambazo ni weak kijeshi mfano: Iraq, Yugoslavia, Libya,Afghanistan,Syria etc.

Halafu watu wanakuja hapa na maoni ya ajabu ajabu eti Urusi haina lolote sana sana inajivunia missiles zake za thermonuclear basi, as if Amerika haina silaha za nuclear au Urusi kuwa na missiles mabom ya nuclear ni dhambi!!!

Sasa kama mnafikiri NATO/US wana uwezo mkubwa kijeshi kwa nini hawajiingizi kwenye mapigano ya Ukraine moja kwa moja moja badala yake wanaishia kwenye makongamano na maazimio lukuki vitisho tisho vya kitoto na sanctions chungu mzima, mpaka uchumi wao una fikia hatua ya kuyumba - mwisho wa siku wanakwenda kumbbeleza Putin yaishe kwa kupitia mawaziri wao wa ulizi -alianza waziri wa Ulinzi wa Merokani, juzi juzi kafuatia waziri wa Uingereza ambaye mwaka jana alikuwa anajifanya kifaru mwenye uwezo mkubwa wa kumumaliza Putin na jeshi lake - sasa kiko wapi na mikwala yao - wajaribu basi kuivamia Urusi kwa lengo la kumsaidia Zelensky halafu tuone kutatokea nini??
 
Kwamb vita inapigana Urusi ? hoja nyingine ni vichaa ndo wataamini , Ukraine na Urusi wanafanana karibu kila kitu na uzuri vita inapiganwa Ukraine sehem ambapo wenyej wanaish kila siku na wamepazoea
Kwa fikra zako ndogo, unadhani ni kwanini kumekuwa na mashambulizi kwenye miundombinu muhimu ya nishati hapo Ukraine...?? Unadhani ni kwanini hivi karibuni serikali ya Ukraine iliwaonya raia wake kuhusu hali ya baridi inayokuja...??? Unadhani hadi kufikia sasa Ukraine wanamiundo mbinu imara itakayoweza kuwasaidia wananchi wake kipindi cha baridi..?? Hasa miundombinu ya nishati ya gas na umeme iliyofanyiwa uharibifu mkubwa na Urusi..
 
Heshma yako MKUU
 
Fatilia vita ya russia na finland nyakat za baridi uone finland alivyomtandka urusi, unadhan ukraine hawaujui huo ukanda wao yan kwmb urusi kwny huo ukanda ndiye mtaalam wa kupgana kwny mabarafu na barid kali au siyo?

Russians waliumbwa na sifa za kipekee za kuhimili baridi?

kwamb Baridi lilipigana vita ?
... hoja murua kabisa. Kuna members humu wana-post utumbo hadi unashangaa huyu ni binadamu au zombie!
 
Nadhani ni mkopo siyo msaada na ndiyo maana hii vita ni ngumu kuisha, maana EU na US hawatakubali kirahisi Urusi ashinde. Mikoa yenye mali nyingi kaibeba, hapo wanawaza hela zao zitarudi VP.
Ule hata mie naamini nimkopo nandio ugumu wa vita kama usemavyo

Niwazi Elensky akitii matakwa ya RUSSIA bila kuamuliwa na mabwana zake itakua pigo kwa mabwana zake maana wameweka kiasi kingi watakua looser

Maana sidhanii kama watalipwa tena kiukweli jamaa wanamuhitajia Elensky kwakulipwa deni lao

Ila hem acha tuone khatma ya hili jambo litamalizaje
 
I am sorry to bring this:

RISHI SUNAK

His father was born and raised in the Colony and Protectorate of Kenya (present-day Kenya), while his mother was born in Tanganyika (which later became part of Tanzania). His grandfathers were born in Punjab province, British India, and migrated from East Africa with their families to the UK in the 1960s
 
Kwa maoni yangu ni kwamba Kiev anakopeshwa either kwa kujua au kutokujua! Maana hata wakati wa Vita yetu na Uganda miaka iyo Siraha tulipewa lakini mpaka leo madeni yapo.
Nashukuru MKUU

Nahaya sio maoni yako ndio uhalisia wenyewe huu

Sasa unaposema US anaongoza kuuza silaha kupitia mgogoro wa UKRAINE va RUSSIA unakua unakosea sana kwa hio kauli yako hapo juu nauhalisia

Yaani hapo ukweli nikwamba US nawenzake wamewekeza mabilioni ya $ kwa UKRAINE kupitia mkopo kwamana hio wanauza silaha ila hawapati faida kwanza kwamuda huu

Faida ya US inategemeana na mwenendo na khatma ya huu mzozo hapa akishinda UKRAINE inakua wazi US na NATO yake watafaidika na zile silaha walizotoa mkopo kwa Elensky (hapa kwenye silaha US kacheza kamari ) na anaomba UKRAINE washinde warejeshe chao

Ikitokea RUSSIA akashinda hii OP inakua hasara kubwa sana sana sanaa kwa US na shost zake maana wanakua wametupa pesa maana wamewekeza ila hawakupata walichotarajia

RUSSIA tayar hapo UKRAINE anavuna faida za SMO maana anazuia maeneo yrnyr rasilimali nyingi na faida nyingi mfano ukanda ule ana kamatia bahari huku MAURIOPOL anakamatia eneo kubwa lenye viwanda vya chuma na kuna kipindi walikua wanasema RUSSIA washaanza peleka kwao sijui kama kweli ama laa ila faida tayar tukienda kule DONBAS jamaa wanajibebea NGANO SHAIRI nk
Kiufupi mpaka sasa RUSSIA kashaanza kula matunda ya SMO ila kwaupande wawest wao wanawekeza wanasubiria final itakuaaje acha tuone


Mwisho :-kwamaoni yangu kupitia hili la silaha US na wenzie bado hawajaanza kufanikiwa nakuvuna pesa kama uliposema kule awali hapa faida ya US na wenzake wataiona baada ya hii vita nabaada yenyewe niwategemee UKRAINE aibuke mshindi la sivyo imekula kwao
 
Baada ya Urusi kushambulia miundombinu ya umeme katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, mji huo na meneo mbalimbali ya nchi hiyo yamelazimika kuingia katika mgao wa umeme huku hatua kali za udhibiti wa matumizi ya umeme kama vile kuzima taa za barabarani zikichukuliwa.

Picha:












Ratiba:

 
Umeongea la maana ndugu yangu. Binafsi nimeshalisemea sana hili na hata kuliripoti kwa hao moderators. Katika platforms nyingine kama yahoo, comments mbovu zote hufutwa. Kwa hili la matusi, ni wazi jamiiforum wamelala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…