Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Haya mambo yana ujinga na kuhitaji kujua ukweli.

Mara USA anataka Angie yeye kama yeye. Hataki Tena ushirika na Ulaya.

Bomu likitua ndani ya Russia basi tena

Rais wa Ukraine bado yuko huko Kiev sema wapambe wa Putin wanataka akimbie nchi Kitu ambacho Hawezi kukifanya maana anauwezo wa kupambana kuilinda nchi yake dhidi ya wavamizi kutoa Russia,Kwa hiyo wanaosubiri akimbie nchi watasubiri sana tu.
 

Mkuu naomba niku sahihishe kidogo... US hauzi silaha hapo Ukraine

US yeye ndiye anapigana Vita hapo Ukraine. Sasa unawezaje kuwa wewe ndiye unapigana Vita halafu wewe ndiye "unajiuzia silaha".

Hiyo Vita hapo ni Kati ya US/NATO na Russia. Ukraine Wala sio yeye anayepigana Vita.

Ndio maana Zelensky kila siku anatoa demands... Ili muendelee kupigana Vita kwenye ardhi yangu, Sasa embu nipeni dollar kadhaa wa kadha...
 
Kipindi kile Cha barid Cha mwezi wa pili wakati Putin anavamia Ukraine watu walisema kipindi Cha kiangazi Russia ataichukua nchi sababu waliamin barid ilikua ni kikwazo kwa russia Leo Tena wamekuja na hadithi nyingine ukweli ni kwamba mambo sio marais kama waafrika wengi tunavyodhani
 
Wajuvi mtusaidie hii ishu hapa ina faida gani na hasara gani kwa RUSSO

Na imewekwa kwajili gani ama malengo yapi hasa !!?

T14 Armata
Qibsyl
Jesus Mlokozi
Galip Vrl
Mr Tyang
Nawengine woooote
Sorry mkuu Bwana Utam sikuwa na muda mzuri leo ila naamini baadhi ya wakuu washakupatia majibu (japo sijafikia comment zao) ila Acha namie niongezee kidogo ninacho fahamu kuhus Fortifications line au defense line.

NAOMBA KUANZA NA MAANA KWA UPANA;

Line of defense kwenye mambo ya kijeshi, ni muundo ambao unaundwa na jeshi chini ya wizara ya ulinzi au mamlaka za usalama wa eneo/nchi husika kwajili ya kulinda mipaka yake au kujilinda dhidi ya mashambulizi ya adui au Uvamizi.
Muundo huo unaweza ukawa wa aina mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Mifumo ya ulinzi ya kijeshi eneo husika , kama vile kuweka no fly zone, defensive weapons kama ant-missile, ku deploy vikosi maalamu vya ulinzi wa mipaka na nk. Mfano wa hapa ni;
☆The Three winter lines (Ambazo ni Gustav Line, the Bernhardt Line na hitter line) hizi ziliundwa na Italy dhidi ya majeshi ya Adolf Hitler wakati wa vita vya pili vya dunia kwajili ya kukinga eneo la magharibi mwa Italy.

2. Sera ya kujilinda, sana sana inakuwa ime base sana kwenye mambo ya kujilinda kijeshi au waswahili wanasema kujihami, mfano: inaweza pitishwa sera inayo sema, Nchi jirani ikirusha let say kombora likavuka "line of difense" basi hilo tukio litachukuliwa kama shambulio la kigaidi au Uvamizi juu ya mipaka husika, hivyo basi nchi italazimika kutangaza vita dhidi ya huo uvamizi kwa lengo la kulinda mipaka yake.

3. Defensive structure, hapa nchi au eneo husika linaweza kujengewa structure ya kiulinzi kama vile Ukuta wa kijeshi (Unaolindwa na wajeda), barrier ya kijeshi, target structures za kijeshi na nk, ifuatayo hapa chini ni mifano baadhi tu ya difensive structure;

☆ THE GREAT WALL OF CHINA- Huu ukuta ni line of defense ulio jengwa kwajili ya kuikinga China dhidi ya maadui wa Asia-Ulaya (Eurasia enemies)

☆The Mannerheim Line- hii ilijengwa na Finland kwajili ya kujikinga dhidi ya nguvu ya Soviet union, lakini kabla ya kukamilika ndo ikatokea "winter war" kati ya Finland Vs Soviet union.

☆Fortifications of Derbent (Caspian Gate)- hii ilijengwa na watu wa Persia ili kujikinga dhidi ya maadui wao wa Caspians

☆Tosa maganga Barrier- hii ni milima iliyotumiwa na jeshi la mkwawa kama line of difense dhidi ya jeshi la wajermani, ambapo jeshi la mkwawa lilifanikiwa kuyadhibiti majeshi ya kikoloni kuingia ndani ya himaya yao kwa kuwaporomoshea mawe na mvua ya mishale kutoka miliman juu, inasemekana hata hilo neno tosa maganga limetokana na Vita hiyo likimaanisha "Rusha/Shusha Mawe" (Sijui kama nimepatia, Ndugu zangu wahehe watanisahihisha). Hata ukifuatilia historia za falme mbalimbali duniani basi utakuta miji mhimu kama palace ilikuwa imezungukwa na kuta imara za ulinzi kama line of defense ambapo ukiivunja hiyo basi ni rahisi hata kupindua ufalme husika au kuangusha ufalme huo.

NAAMINI UTAKUWA UMEELEWA MAANA YA LINE OF DIFENSE NAOMBA TURUDI KWENYE SWALI LAKO NAMBA MBILI NA TATU.

KWANINI RUSSIA ANAJENGA LINE OF DIFENSE ENEO LA KURSK?
JIBU: Ili kujilinda dhidi ya maadui wake wa west ambao wamejipenyeza Ukraine, kumbuka hii oblast ya Kursk ipo russia mpakani na Ukraine pia kijografia Kursk ni eneo rahisi ambapo majeshi ya Ukraine au NATO yanaweza kupita kuingia Russia tofauti na hapo labda yapite Belarus, Georgia au Finland kitu ambacho ni ngumu kutokea kutoakana na sababu za kidiplomasia na kiusalama pia Belarus ni chawa wa Russia hivo basi njia rahisi ya NATO kuingia Russia ni kupitia Ukraine.

FAIDA ZA RUSSIA KUJENGA HIZO LINE OF DIFENSE NI ZIPI?

☆Kuwa na uwezo wa kumdhibiti adui kabla hajaingia ndani ya russia

☆Kujilinda dhidi ya maadui wao hasa NATO kwa mgongo wa Ukraine.

☆Kupata justification ya kutumia silaha yeyote ile ya kivita endapo adui atavuka line of defense au kutaka kuvuka line of defense.

☆Kui threat Ukraine isijaribu kuvuka eneo hilo au kurusha kombora kuvuka eneo hilo kwa hofu ya russia kutangaza Vita kamili dhidi ya Ukraine.

☆Kupata sababu ya kuishambulia Ukraine kwa level za kivita endapo itavuka hiyo line of defense, nadhani mfano mmeuona baada ya russia kutumia bomu la crimea bridge kama shambulio la kigaidi kuiadhibu Ukraine.

HASARA ZA RUSSIA KUJENGA HIZO LINE OF DIFENSE NI ZIPI?
JIBU: Hapa ukiondoa hasara za kiuchumi kama vile cost of construction and millitary equipments deployment, hakuna hasara nyingine hasa katika nyanja za kijeshi na kiusalama.

Nawasilisha kwako Mkuu Bwana Utam
Wako pro-Russia mchelewaji Mr Tyang
 
Mtu yoyote akisoma maelezo Yako,atajua kabisa wewe ni mtu unadhani unajua Kila kitu hapa duniani hasa masuala ya silaha lakini ukweli hauko hivyo.
Msingi wa majadala wetu wala Mimi sibishani Bali nachangia mada TU.

Msingi ni wewe ulisema Marekani haijawahi kuwaza kama itavamiwa,na hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuivamia Marekani .
Mimi nikakujibu zipo nchi zinazowaza kuivamia.
Nikakupa mfano Urusi,china na Korea Kaskazini.

Sasa hapa pengine tulitakiwa tutazame maana ya neno kuivamia.Hii sio shida,shida ni tafasiri TU.

Ujuaji wako ni shida sana,hivi wewe kwa akili Yako unadhani Korea Kaskazini wanatengeneza makombora TU?
In maana wewe unajua Kila kitu kuhusu Korea Kaskazini?
Je huamini kama Wana silaha nyingine zaidi ya Makombora TU?
Hujui kua Wana nyambizi zinzoweza kufika Hadi Marekani?(Sihitaji kujua kuhusu uwezo wake kiufanisi).

Au pengine sijajua ulimaanisha Nini kusema hakuna nchi inayowaza kuivamia Marekani.

Labda tuangalie sababu za kuivamia Marekani.

Hivi KK inatengeneza makombora ya masafa marefu zaidi,unadhani hayo ni kwa ajili ya south Korea?wakati SK IPO pua na mdomo?au unadhani hayo makombora ni kwa ajili ya kupiga Canada? Je KK Ina mzozo na Canada?
KK in mzozo zaidi kati yake na Marekani na south Korea TU.
Je hayo makombora ya masafa marefu ni kwa ajili ya SK?
Ni mara ngapi Marekani imetishia kuipiga KK?
Je huoni nayo KK itafanya Kila iwezavyo kujibu mapigo?
Sasa Mimi nakuambia hivi,kwa sababu Marekani imekua ikiitishia KK mara kadhaa nayo KK imeamua kutengeneza silaha za kuweza kufika Marekani.
KK Ina nyambizi na zinaweza kifika Marekani.
suala la ufanisi au uwezo Mimi sijui,ila ninachojua ni kua KK inaweza kuivamia Marekani,uwezo wanao,ila matokeo ndio sijui.
Hata Marekani na uwezo wake wote iliivamia Afghanistan na matokeo yake tunayajua.

Urusi.
Nilisema Urusi inaweza kuivamia Marekani.
Kutokana na mvutano wa miaka mingi kati ya Urusi na Marekani Urusi iliwahi kuonesha hata maeneo itakayopiga.
Urusi inaweza ku strike na ku invade,wewe na Mimi hatujui kama wangeamua kushambulia maeneo waliyayaainisha wangetumia njia Gani,hatuwezi kuwapangia.

Nishindwe kujua tofauti kati ya strike na invasion.?

Hoja yangu Iko hivi.Kila uvamizi una sababu,kama Urusi akiona Kuna sbabu ya kuivamia Marekani wataivamia.Uwezo wanao na vifaa vya kuvamia anavyo,lkn je? ni sababu zipi,Mimi sijui,ila point yangu ni kwamba Urusi ana uwezo wa kuivamia Marekani kama ambavyo hata Marekani ana uwezo wa kuivamia Urusi,matokeo yatakuaje Mimi sijui.

Vivyohivyo kwa china.

Kwa Nini nimezitaja nchi hizo tatu,Urusi,china na KK.
Nimezitaja kama nchi zinazowaza kuivamia Marekani pale zikiona Kuna sababu ya kufanya hivyo kwa sababu hizi nchi tatu Zina mizozano sana na Marekani.
Sio mara moja wala mara mbili,Marekani imeonesha dalili mbaya juu ya mataifa haya,mfano Marekani kupeleka makombora ya nyukilia Uturuki,ama kujaribu kupeleka aircraft carrier ukanda wa Korea kwa lengo la kutaka kushambulia KK.

Vivyo hivyo ,nazo Kila moja kwa wakati wake ziliamua kuandaa majeshi Yao, yanayoweza kufika Marekani,hasa kwa kuzingatia jiografia kati Yao na Marekani.

Lakini mwisho kabisa napenda nikukumbushe kua, Japan iliwahi kuivamia Marekani na kupelekea maafa makubwa sana huko Marekani.
Sasa sijui kwako wewe uvamizi unaueleza kwa namna Gani.
 
Kitendo Cha USA Tena akiwa na NATO kupigwa na wavaa makobazi Kule Afghanistan mpk kukimbia nchi kumemfanya kua super power wa mchongo.
Russia mbona yeye alishindwa vibaya na mujahedeen akiwemo osama bin laden Afghanistan tatizo la elimu bure ni changamoto kubwa sana Tanzania

Russia au U.SA kushindwa vita hakutawaondelea status kwamba wao ni super power,
 
Russia kaipiga DUNIA combined!! Uchumi wa taifa moja unahimili Muungano wa yaliyokuwa yakijiita mataifa tajiri duniani!! Hii ni aibu ya karne.

Kitendo Cha Urusi kupewa msaada na Iran kimemwondoa kwenye super powers
Halafu kwa taarifa yako, hizo drone za Iran🇮🇷 ni teknolojia ya Urusi ila Warusi wenyewe wanazalishia Iran. Unajua kwa nini wapuuzi Marekani wamepiga sana kelele? Sio tu kwa sababu Iran amepakaziwa kutia msaada, sababu kubwa ni Israel, ngoja tukusaidie kufikiri. Tayari Iran imeonekana kuwa tishio kwa Israel kama inamiliki hizi suicide drones. Usalama wa Israeli umewekwa rehani, hili ndilo tatizo
 
Nadhani ni mkopo siyo msaada na ndiyo maana hii vita ni ngumu kuisha, maana EU na US hawatakubali kirahisi Urusi ashinde. Mikoa yenye mali nyingi kaibeba, hapo wanawaza hela zao zitarudi VP.
Kwa kifupi huwa inakuwa hivi ikimpa mtu mikopo kwenye vita akishindwa hakuna kulipwa. Sasa watu lazima wakomae
 
Unafikiri akili za wazungu ni sawa na akili za mwafrika utasubiri sana, tofauti yako wewe mwafrika unaangalia Leo wenzako wanaagalia miaka 10 ijayo

Na kwa kukusaidia Israel alishapigwa supprise attack nyingi na akafanya counter attack akashinda, Israel ndo nchi ambayo wananchi wake wanajua fika mda wowote na saa yeyote wanaingia kwenye vita sio wajinga kama unavyotaka kutuaminisha
 

Mkuu,sijasema Urusi na Korea Wana mpango wa kuivamia Marekani.

Mimi nilichangia hoja ya T14 Armata kua Marekani haijawahi kuwaza kama itavamiwa,na wala hakuna nchi duniani inayoweza kuwaza huo ujinga wa kutaka kuivamia Marekani.

Mimi nilimjibu kama mjadala unavyotaka,kua zipo nchi zinazowaza kuivamia Marekani,nikazitaja nchi tatu,Urusi, china na Korea Kaskazini.
Nchi hizi sio chokozi,Bali kutokana na tabia za Marekani juu Yao,ndipo nazo zikawa na mawazo ya kutaka kuivamia Marekani.
Unajua Kila uvamizi una sababu,da a u nzuri ama mbaya
Kwa Urusi,china na KK kwao sababu ni kujilinda.
Maana yangu ni kwamba zikiona Kuna sababu ya kupelekea kuvamia,zitavamia.
Urus,China na KK Wana sababu kabisa za kuivamia Marekani.
Mfano Kila mara Marekani walijaribu kupeleka meli vita Korean peninsula.hiyo ni sabau tosha kabisa ya KK nayo kusogeza nyambizi zake katika pwani ya Marekani.

Kadri Marekani anavyoongeza silaha Kali Ukraine ,ndivyo Urusi nae anavyosogeza silaha zake Kali karibu na Marekani
Hapa Sasa ni kama vile wachezaji mpira wanavyosubiri refarii apulize kipenga. TU mpria uanze.
Maana yake ni kwamba kwa ulinzi na usalama wa Urusi,Marekani wakivuka mstari ambao Urusi wameweka TU Urusi watavamia Ndani ya marekani.iki hivyo kwa china na KK.
Kwa kifupi Urusi haiwezi kukaa ikatazama TU kama ikona dalili zote kuwa Marekani ataishambulia ndani kabisa.

Ukae ukijua Japan iliwahi kuivamia Marekani.
 
Yote haya hayaonyeshi ni namna gani North Korea inaweza vamia Marekani. Makombora ya nyuklia ndio yanavamia? Narudia kukuuliza unajua tofauti ya invasion na strike au unaongea uonekane nawe upo?

Japan ilishambulia Marekani. Ile ni strike au attack, sio invasion. Ndio maana ilitumia lisaa tu wakalipualipua wakakimbia. Ungesoma tangu mwanzo kuelewa ungeelewa ila kwa vile umekuja kichwa kichwa kubisha na bado unakaza kichwa huwezi elewa.

Nakuuliza tena. North Korea anaivamia Marekani kwa kutumia nini? Hizo diesel subs chache zenye crew ya watu 30 sijui ndio zitafanya beach landing na kusecure shores? Au atatuma paratroopers kwa kutumia ungo?

Yani ukae hapa usubiri Marekani aanze kuchimba trenchs, ajenge concrete pyramids kwenye line kumzuia adui? Unaishi dunia gani mzee.

Tukianza kusema China itaivamia Taiwan, silaha za kuvamia zipo na mechanism ipo inaonekana. Ukianza kusema nchi fulani itaivamia Marekani, nikiuliza utumie mwezi hapa kuomba ushauri ni nini kitatumika kuivamia Marekani jibu huna. Hutoona boots on ground ya adui kwenye ardhi ya Marekani. Pigs flying!
 
Nashukuru MKUU

Nahaya sio maoni yako ndio uhalisia wenyewe huu

.. Ikitokea RUSSIA akashinda hii OP inakua hasara kubwa sana sana sanaa kwa US na shost zake maana wanakua wametupa pesa maana wamewekeza ila hawakupata walichotarajia

Mkuu kama umepitilia historia ya mistari hii ya maboma /ngome za kuzuia maadui,
natumaini umejifunza pia sehemu zilisaidia kwa muda tu, nyingine zilikuwa bure kabisa.
Sijaona ulitaja LIMES ya Kirumi, mfumo mkubwa sana, au MAGINOT LINE ya Ufaransa.
Maginot Line ya Vita Kuu ya pili ilikuwa bure kabisa; ATLANTIC WALL ya Hitler haikusaidia, UKUTA MKUBWA WA CHINA ulivunjwa mara kwa mara, ukuta wa Uajemi kando la Bahari Kaspi ilisaidia kwa muda tu, vivyo hivyo LIMES ya Warumi . . . .
Zote zilimlazimisha mjenzi kuweka iadi kubwa ya askari kuzilinda na kutetea, zilitosha kuzuia washenzi wachache, kila wakati adui mwenye nguvu alivunja sehemu moka mteteaji alikosa wanajeshi wa kutosha kwa sababu aliwahi kuwasambaa kwenye mstari ndefu . . . .
 
Kandi ya drone,Kuna Fateh-110,hiiiiiiii!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…