Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 20,546
- 38,093
Darasa la bure hiliSorry mkuu Bwana Utam sikuwa na muda mzuri leo ila naamini baadhi ya wakuu washakupatia majibu (japo sijafikia comment zao) ila Acha namie niongezee kidogo ninacho fahamu kuhus Fortifications line au defense line.
NAOMBA KUANZA NA MAANA KWA UPANA;
Line of defense kwenye mambo ya kijeshi, ni muundo ambao unaundwa na jeshi chini ya wizara ya ulinzi au mamlaka za usalama wa eneo/nchi husika kwajili ya kulinda mipaka yake au kujilinda dhidi ya mashambulizi ya adui au Uvamizi.
Muundo huo unaweza ukawa wa aina mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Mifumo ya ulinzi ya kijeshi eneo husika , kama vile kuweka no fly zone, defensive weapons kama ant-missile, ku deploy vikosi maalamu vya ulinzi wa mipaka na nk. Mfano wa hapa ni;
☆The Three winter lines (Ambazo ni Gustav Line, the Bernhardt Line na hitter line) hizi ziliundwa na Italy dhidi ya majeshi ya Adolf Hitler wakati wa vita vya pili vya dunia kwajili ya kukinga eneo la magharibi mwa Italy.
2. Sera ya kujilinda, sana sana inakuwa ime base sana kwenye mambo ya kujilinda kijeshi au waswahili wanasema kujihami, mfano: inaweza pitishwa sera inayo sema, Nchi jirani ikirusha let say kombora likavuka "line of difense" basi hilo tukio litachukuliwa kama shambulio la kigaidi au Uvamizi juu ya mipaka husika, hivyo basi nchi italazimika kutangaza vita dhidi ya huo uvamizi kwa lengo la kulinda mipaka yake.
3. Defensive structure, hapa nchi au eneo husika linaweza kujengewa structure ya kiulinzi kama vile Ukuta wa kijeshi (Unaolindwa na wajeda), barrier ya kijeshi, target structures za kijeshi na nk, ifuatayo hapa chini ni mifano baadhi tu ya difensive structure;
☆ THE GREAT WALL OF CHINA- Huu ukuta ni line of defense ulio jengwa kwajili ya kuikinga China dhidi ya maadui wa Asia-Ulaya (Eurasia enemies)
☆The Mannerheim Line- hii ilijengwa na Finland kwajili ya kujikinga dhidi ya nguvu ya Soviet union, lakini kabla ya kukamilika ndo ikatokea "winter war" kati ya Finland Vs Soviet union.
☆Fortifications of Derbent (Caspian Gate)- hii ilijengwa na watu wa Persia ili kujikinga dhidi ya maadui wao wa Caspians
☆Tosa maganga Barrier- hii ni milima iliyotumiwa na jeshi la mkwawa kama line of difense dhidi ya jeshi la wajermani, ambapo jeshi la mkwawa lilifanikiwa kuyadhibiti majeshi ya kikoloni kuingia ndani ya himaya yao kwa kuwaporomoshea mawe na mvua ya mishale kutoka miliman juu, inasemekana hata hilo neno tosa maganga limetokana na Vita hiyo likimaanisha "Rusha/Shusha Mawe" (Sijui kama nimepatia, Ndugu zangu wahehe watanisahihisha). Hata ukifuatilia historia za falme mbalimbali duniani basi utakuta miji mhimu kama palace ilikuwa imezungukwa na kuta imara za ulinzi kama line of defense ambapo ukiivunja hiyo basi ni rahisi hata kupindua ufalme husika au kuangusha ufalme huo.
NAAMINI UTAKUWA UMEELEWA MAANA YA LINE OF DIFENSE NAOMBA TURUDI KWENYE SWALI LAKO NAMBA MBILI NA TATU.
KWANINI RUSSIA ANAJENGA LINE OF DIFENSE ENEO LA KURSK?
JIBU: Ili kujilinda dhidi ya maadui wake wa west ambao wamejipenyeza Ukraine, kumbuka hii oblast ya Kursk ipo russia mpakani na Ukraine pia kijografia Kursk ni eneo rahisi ambapo majeshi ya Ukraine au NATO yanaweza kupita kuingia Russia tofauti na hapo labda yapite Belarus, Georgia au Finland kitu ambacho ni ngumu kutokea kutoakana na sababu za kidiplomasia na kiusalama pia Belarus ni chawa wa Russia hivo basi njia rahisi ya NATO kuingia Russia ni kupitia Ukraine.
FAIDA ZA RUSSIA KUJENGA HIZO LINE OF DIFENSE NI ZIPI?
☆Kuwa na uwezo wa kumdhibiti adui kabla hajaingia ndani ya russia
☆Kujilinda dhidi ya maadui wao hasa NATO kwa mgongo wa Ukraine.
☆Kupata justification ya kutumia silaha yeyote ile ya kivita endapo adui atavuka line of defense au kutaka kuvuka line of defense.
☆Kui threat Ukraine isijaribu kuvuka eneo hilo au kurusha kombora kuvuka eneo hilo kwa hofu ya russia kutangaza Vita kamili dhidi ya Ukraine.
☆Kupata sababu ya kuishambulia Ukraine kwa level za kivita endapo itavuka hiyo line of defense, nadhani mfano mmeuona baada ya russia kutumia bomu la crimea bridge kama shambulio la kigaidi kuiadhibu Ukraine.
HASARA ZA RUSSIA KUJENGA HIZO LINE OF DIFENSE NI ZIPI?
JIBU: Hapa ukiondoa hasara za kiuchumi kama vile cost of construction and millitary equipments deployment, hakuna hasara nyingine hasa katika nyanja za kijeshi na kiusalama.
Nawasilisha kwako Mkuu Bwana Utam
Wako pro-Russia mchelewaji Mr Tyang
Shukran sana sana sana MKUU nimekuelewa hasaaaa