Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ndio watu wengi ni kwa sababu ya chuki dhidi ya Marekani ndio maana Wanakaa upande wa Russia lakini ukiwa unasimamia haki Russia ana makosa.
Kuna mtu kawaita wamarekani na Ulaya kuwa ni wanaharamu. Hivi kati yao na Russia nani ni nafuu kwa waafrika. Kuishi Russia ukiwa ni Mwafrika si kazi rahisi.
 
Hatujachukua Kherson wajameni maana mwezi mzima tunasema superpower wa mchongo mara kuchapo cha mbwa koko nk sasa Kherson vp. Ngapingapi huko
Ukraine na Russia, Ukraine ni hafifu kijeshi ila wana moyo mkuu.

Hawa watu utaifa wao umo mioyoni mwao na ndiyo kitu pekee kinachowapa morali wa kuendelea kupambana. Kila tone la mtu wa Ukraine linalomwagika ni sadaka kwa ajili ya nchi yao.

Russia mpaka wanaahidiwa kulipwa ndiyo wanapigana, wakati watu wa Ukraine wanaacha kazi kwingine wanaamua kurudi kwao ili kupigania nchi yao.

Ukraine inapigwa, ila Russia inatumia nguvu kubwa sana kuipiga Ukraine.
 
Kuna watu chuki zao kwa Marekani ndiyo zimewafanya wachague kukaa upande wa Russia, lakini kinachowashangaza ni kuwa adui yao Mwingine, Israel anamsaidia Russia.

Hii vita ukiitazama kwa mtazamo huo mwisho wa siku unatoka kwenye uhalisia unabaki kwenye matamanio. Kwa mfano Ukraine ikipigwa, faida kwa Tanzania ni ipi. Jee Russia ikirudisha maeneo iliyoyateka kwa Ukraine ama ikibaki nayo, sisi kama nchi tunafaidika nini?

Urusi ilifanya kosa kuivamia Ukraine na kama tungekuwa taifa letu lina misimamo kama ile ya zamani, saa hizi tayari tungekuwa tumeshaishutumu Russia kwa uvamizi huo. Kitu pekee kwenye vita hii ni kuona kama ilikuwa ni halali Russia kuivamia Ukraine??
Niombe ufafanuzi kwa nini unasema Russia ilifanya kosa kuivamia Ukraine?

Chanzo cha huo mgogoro mpaka Russia kuamua kuivamia Ukraine ni nini hasa?
 
Mara nyingi vita huwa ni ujinga mnakufa kwa vitu vya kijinga.
Hivi unaakili kweli watu wanapigania nchi Yao isimegwe kihuni unasema ni ujinga,

hivi unajua vita dhidi ya Uganda 1977 Tanzania ingesema ifuate ushauri wako Leo hii kagera ingekua sehemu ya uganda
 
Ukrain Hana jeshi pale mkuu wale wote unaowaona wanapogana upande wa Zele Ni mamluki pia nao wanalipwa ndo maana siku zote zele anaomba msaada wa fedha na silaha,ktk Hilo hata urusi pia hatumii jeshi lake labda baadhi tu ya viongozi ktk kutoa ushauri, baadhi ya vifaa vya anga na maji ndio anatumia wataalam wa jeshi lake
 
Winter is Coming!!

Ili kuepusha maafa, Vitaly Klitschko anazitaka nchi za Magharibi kutuma mablanketi na mavazi ya joto haraka.

View attachment 2401436Mwanamke akitembea kwenye kivuko cha theluji baada ya theluji nzito kuanguka katika mji mkuu wa Ukraine, kyiv, Februari 6, 2019.

Raia wengi wa Ukraine wanaweza "kuganda hadi kufa" katika miezi ijayo isipokuwa nchi za Magharibi ziwasaidie kukabiliana na tatizo kubwa linalokuja kutokana na mashambulizi ya anga ya Urusi kwenye miundombinu ya nishati ya taifa hilo, Meya wa Kyiv Vitaly Klitschko aliviambia vyombo vya habari vya Uingereza siku ya Ijumaa.

Akizungumza na The Daily Telegraph, Klitschko, bingwa wa zamani wa ndondi uzito wa juu, alikiri kwamba Ukraine itakabiliwa na changamoto kubwa. "Tunafanya kila tunaloweza kufanya kuokoa maisha ya watu wetu na kuwalinda," meya aliambia chombo hicho.

Afisa huyo alisema timu yake imeweza kununua idadi ya jenereta za umeme huku ikitayarisha vituo 1,000 vya kutengeneza joto huko Kyiv kwa kutarajia kile alichokiita "hali mbaya zaidi."

Klitschko aliashiria kwamba Ukraine inahitaji haraka sio tu silaha za Magharibi na mifumo ya ulinzi wa anga, lakini pia blanketi, nguo za msimu wa baridi na jenereta.

"Ni wakati muhimu kwa aina hii ya msaada," alisisitiza.

Ukrainians ng'ambo waliambiwa wasirudi nyumbani msimu huu wa baridi

Akitoa mfano wa "hatari ya suala la kibinadamu," pia aliwataka Waukraine ambao wamekimbia nchi kukaa mbali msimu huu wa baridi kama wanaweza. "Lakini lengo letu kuu ni kuwarudisha watu wetu, thamani kubwa ya Ukraine ni raia wetu na watu wetu," aliongeza.

Maoni ya meya yanalingana na matamshi ya awali yaliyotolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Irina Vereshchuk. Wiki hii, alitoa wito kwa Waukraine walioondoka baada ya kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Urusi kutorejea nyumbani kabla ya majira ya kuchipua, kutokana na mgomo wa Moscow kwenye miundombinu ya nishati.

Wakati huo huo Yuri Vitrenko, mkuu wa kampuni kubwa ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Naftogaz, amewaonya raia wenzake kwamba Ukraine inakabiliwa na majira ya baridi kali zaidi kuwahi kutokea, huku akidai kuwa mashambulizi ya anga ya Urusi yameharibu "karibu 40% ya mitambo ya kuzalisha umeme".

Ukraine imekuwa ikikabiliwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara tangu Moscow ilipoanzisha mgomo mkubwa diidi ya vituo vyake vya nishati, ikiwa ni pamoja na vituo vya nishati mnamo Oktoba 10, baada ya kuishutumu Kyiv kwa mashambulizi ya kigaidi kwenye miundombinu ya Urusi, ikiwa ni pamoja na daraja la kimkakati la Crimea.

Katika jaribio la kuepusha maafa ya kibinadamu, EU wiki iliyopita ilitangaza mpango mpya wa makazi ya dharura na vifaa vya msimu wa baridi kwa Ukraine, ikiahidi kutoa zaidi ya Euro milioni 175 ($ 174 milioni) katika usaidizi wa kibinadamu kwa sehemu zilizo hatarini zaidi za idadi ya watu nchini Ukraine na. nchi jirani ya Moldova.

Mapema mwezi huu Marekani, mfadhili mkuu wa kimataifa wa Ukraine, iliahidi kuunga mkono Kyiv kwa usaidizi wa dharura wa dola milioni 55. Mfuko huo ni pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya kutengeneza joto, ununuzi wa jenereta na njia zingine za kuwapa joto Waukrainia.

My Take:
Nmpongeza Klitschko kwa kusema ukweli. Suala hilo ni muhimu na halihitaji propaganda za Zelensky!!
Kabla ya umeme na gesi walikua wanaishije ulishawahi jiuliza hili swali ewe kijana mwenye upeo mdogo
 
Ukraine na Russia, Ukraine ni hafifu kijeshi ila wana moyo mkuu.

Hawa watu utaifa wao umo mioyoni mwao na ndiyo kitu pekee kinachowapa morali wa kuendelea kupambana. Kila tone la mtu wa Ukraine linalomwagika ni sadaka kwa ajili ya nchi yao.

Russia mpaka wanaahidiwa kulipwa ndiyo wanapigana, wakati watu wa Ukraine wanaacha kazi kwingine wanaamua kurudi kwao ili kupigania nchi yao.

Ukraine inapigwa, ila Russia inatumia nguvu kubwa sana kuipiga Ukraine.
Nani kakwambia Ukraine awalipwi?.unajua Ukraine kapewa msaada wa fedha kiasi gani na pia kapewa mkopo wa fedha kiasi gani?.
 
Niombe ufafanuzi kwa nini unasema Russia ilifanya kosa kuivamia Ukraine?

Chanzo cha huo mgogoro mpaka Russia kuamua kuivamia Ukraine ni nini hasa?
Kwanza huu mgogoro siyo mpya wala si wa 2014 bali ni wa kutoka mwaka 1991 wakati Soviet inasambaratika. Wakati huo kulikuwa na makundi mawili yanayopingana kifalsafa na kimtazamo kuhusu hatima ya Soviet.

Kundi la kwanza ni la wakomunist waliokuwa wanaamini kunahitajika mabadiliko kidogo sana katika mifumo ya kuendesha nchi na kundi jingine lilikuwa linaamini kunahitajika mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa siasa wa Soviet.

Mgogoro wa makundi haya mawili ukasababisha majimbo 12 kujitoa Soviet na kujitangazia Uhuru wao na kutaka kutambuliwa kimataifa. Nchi hizo 12, Ukraine ni mojawapo. Kwa ivo tangu wakati huo, Russia imekuwa ikiona ni wajibu wake kurudisha yale majimbo yaliyojitoa Soviet ile yawe sehemu ya Russsia.

Na nchi zile zilizojitoa toka Soviet zinaona ni salama zaidi kuegemea NATO na Ulaya kwa Usalama wao. Kwa ivo kila kijisababu kikipatikana kutakuwa na hizi vita na mapambano kila wakati. Hoja ni kurudi ama kutokurudi Russia.
 
Hatujachukua Kherson wajameni maana mwezi mzima tunasema superpower wa mchongo mara kuchapo cha mbwa koko nk sasa Kherson vp. Ngapingapi huko
Uliaga humu jukwaani na kusema utakuja baada Russia kuungurumisha nyukria,Sasa kipi kimekurudisha?

Nyukria bado Mzee,endelea kutulia huko huko mafichoni.., Russia akingurumisha nyukria tutakutag[emoji2957]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Yani..kuna watu maakili ndogo sana..sawa sawa na kukata maji dodoma na kusema watu wa dodoma watakufa kwa kiu.

Kumbuka hao watu wameishi maeneo hayo kabla hata huduma ya gesi haijafika hapo...na walishi na baridi lao tokea kitambo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukraine na Russia, Ukraine ni hafifu kijeshi ila wana moyo mkuu.

Hawa watu utaifa wao umo mioyoni mwao na ndiyo kitu pekee kinachowapa morali wa kuendelea kupambana. Kila tone la mtu wa Ukraine linalomwagika ni sadaka kwa ajili ya nchi yao.

Russia mpaka wanaahidiwa kulipwa ndiyo wanapigana, wakati watu wa Ukraine wanaacha kazi kwingine wanaamua kurudi kwao ili kupigania nchi yao.

Ukraine inapigwa, ila Russia inatumia nguvu kubwa sana kuipiga Ukraine.
Hapa nimekupata . Maana kwa video za Bwana vunjo ungedhani jamaa wa Russia hakuna jeshi Ukraine wanatembea tu kama boli la mgunda
 
Nan aliwai tishia nyuklia ? huyo huyo ndo muuaji asie na akili ningekuwa mm ningepiga pale moscow ili apate uchungu wa vita
Sio rahisi hivyo,asingekuwa na uthubutu kuyanyanyasa mataifa 30+ beberu mkuu Marekani akiwemo😄😄
 
Ukraine na Russia, Ukraine ni hafifu kijeshi ila wana moyo mkuu.

Hawa watu utaifa wao umo mioyoni mwao na ndiyo kitu pekee kinachowapa morali wa kuendelea kupambana. Kila tone la mtu wa Ukraine linalomwagika ni sadaka kwa ajili ya nchi yao.

Russia mpaka wanaahidiwa kulipwa ndiyo wanapigana, wakati watu wa Ukraine wanaacha kazi kwingine wanaamua kurudi kwao ili kupigania nchi yao.

Ukraine inapigwa, ila Russia inatumia nguvu kubwa sana kuipiga UkraineKwanza

Kwanza kabisa fahamu jambo moja Russia haijatumia nguvu kubwa kuipiga Ukraine...Kama Russia ingetumia nguvu zake zote saa hizi Ukraine ingekuwa majivu....Pili siyo kweli kuwa Ukraine wana moyo wa kupigana ....wanalazimika kupigana kwa kuwa West wanawalazimisha kufanya hivyo...Kwa askari wa Ukraine wanaojaribu kukimbia uwanja wa vita hupigwa risasi na Azov ambacho ni kikundi kilichopo kila kikosi cha Ukraine...Azov wana mlengo mkali na itikdi ya NAZI
 
Kwanza kabisa fahamu jambo moja Russia haijatumia nguvu kubwa kuipiga Ukraine...Kama Russia ingetumia nguvu zake zote saa hizi Ukraine ingekuwa majivu....Pili siyo kweli kuwa Ukraine wana moyo wa kupigana ....wanalazimika kupigana kwa kuwa West wanawalazimisha kufanya hivyo...Kwa askari wa Ukraine wanaojaribu kukimbia uwanja wa vita hupigwa risasi na Azov ambacho ni kikundi kilichopo kila kikosi cha Ukraine...Azov wana mlengo mklai na itikdi ya NAZI
Kuna mambo mnakuza sana kuliko uhalisia. Ukraine inawezaje kuwa majivu bila maeneo kadhaa ya Russia nayo kuwa majivu. Halafu msidhani Puttin ni mjinga kiasi cha kutumia mabomu ya Nyukilia kirahisi.

Sasa hao Azov na Wagner tofauti yao ni nini? Kiuhalisia ni kwamba tunaposema nguvu kubwa hatumaanishi nguvu yote. Mtu mzima mcheza karate akimpiga mtoto wa miaka mitano mateke na ngumi, ni lazima isemwe katumia nguvu kubwa.

Kama Russia ingekuwa inatumia nguvu sawa na Ukraine, sasa hivi ingekuwa imeshafurushwa toka kwenye yale maeneo iliyokwisha kuyateka.
 
Uliaga humu jukwaani na kusema utakuja baada Russia kuungurumisha nyukria,Sasa kipi kimekurudisha?

Nyukria bado Mzee,endelea kutulia huko huko mafichoni.., Russia akingurumisha nyukria tutakutag[emoji2957]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Nimechungulia nikadhani uzi umekatika baada ya dirty bomb kunguruma kumbe BADO mna dribble .

Ok kabla sijarudi rest house naombeni temperature ya Ukraine hali ya hewa ipoje maana na hii issue ya winter sijui mbona hatusikii au mpaka lini tutafika mtu kuganda
 
Back
Top Bottom