Niliwahi kusema kwamba Uingereza inajihusisha sana na suala hili la Ukraine, nikaongezea kwa kusema kwamba niwajuavyo Waingereza wataleta maafisa wao wa kikosi chao cha makomandoo wa SAS kufundisha kikosi maalumu cha Ukraine katika masuala ya kufanya hujuma behind enemy lines ie partsians - Waingereza ni mabingwa sana kwenye nyanja hizo, lakini wakumbuke kwamba na Warusi si mchezo watawafatilia nyenendo zao na kuwashugulikia ipasavyo, juzi hapa makao makuu yao nchini Ukraine ilitiwa kiberiti na high precision missile ya Urusi sijui kama kuna mtu aliye nusurika.
Kama vipi na Warusi nao wafanye mpango wa kuwapatia silaha na mafunzo kwa mara nyingine tena wapigania uhuru wa I.R.A ili wafufue harakati zao za miaka ya 1970/80s, na ikiwezekana wawa instigate raia wa Scotland nao wajitenge na England kwa nguvu i.e kwa mtutu wa bunduki, tuonena hilo Serikali ya White Hall watalichukulia vipi?
Binafsi,kwa maoni yangu naona Urusi ikitaka kumaliza tatizo hili la Wamerikani na Waingereza kuitumia Ukraine kuihujumu Urusi, mchezo huu utaendelezwa indefinitly hivyo ili kumaliza tatizo hilo Warusi wafanye mpangowa kui-annex Ukraine kiujumla, hata kama itawalazimu kupigana na NATO/US moja kwa moja -hawana jinsi.