Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kuwajua au kuwasikia haihusiani na mijadala hii bali wengi tunasoma tu na mengine tukiwa karibu na wanapouwawa wapinzani wake
Unajua Gold Visa waliyopewa wale Russian Oligarchs
Hao matajiri waliingiza hela hapa London billions [emoji383] na kupewa moja kwa moja uraia

Hao jews sio wageni Russia kwani waliingia nchi hizi miaka mingi na leo sio wageni tena bali ni raia kama raia wengine

Tofauti na sisi Tz ambapo mtu unamtaja kwa asili yake hata awe ana generation ta tano

Acha tusubiri baridi la Dec maana kuna watu hapa wameanza kubana mpaka matumizi ya umeme kwa kuwasha tochi FACT
 

Well said mkuu, kwa bahati mbaya Zelensky akili hizo hana kabisa - anafikiri anaweza kuitunia misuri a super power halafu akategemea kwamba NATO/US watamkingia kifua ili yeye na Taifa lake waendelee kubaki salama, juzi alipo vuka/katiza a red line Urusi ilimfanya nini,hivi sasa anajuta kweli kweli kwa kuingizwa kwenye mkenge na washauri wake wa kijeshi wa NATO - na hapo bado makubwa yanakuja hasipo jisalimisha na kumuomba Putin yaishe.
 
Ww jamaa umekuwa ukiandika mambo mengi yasiyo kuwa na msingi na yaliyo jaa ujuaji mwingi wa kijinga.

Vita sio kitu rahisi kama ww unavyo fikiri na ndio maana hakuna kiongozi wa kijeshi kutoka nchi za magharibi ambaye umemsikia akilibeza jeshi la Urusi kwa sababu wanaujua ugumu wa vita na wao wamesha shindwa vita nyingi tu.

Wanajeshi wa Ukraine hawatumii mikuki kupambana bali wana tumia silaha nzito sawa na zinazo tumiwa wanajeshi wa Urusi ina maana mlinganyo kwenye vita hii ni mkubwa tena Ukraine imeizidi Urusi kwa idadi kubwa ya wapiganaji kwenye uwanja wa Vita.

Vita unavyo iongelea mdomoni ni tofauti na tunapo kuja kwenye uhalisia.

Tangu kumalizika kwa vita ya Pili ya dunia vita ya ardhini pekee ambayo Marekani amefanikiwa kushinda ni vita ya Iraq iliyo kuwa imedhohofika kiuchumi na kijeshi na penyewe alikuwa na rundo la washirika.

Vita nyingine alienda kakumbana na vipigo vya aibu na kukimbia tena dhidi ya mataifa dhaifu kabisa.
 

Endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe!!!
 

Maneno ya kujifariji hayo!!!!
 
Ongeza pia Libya.., marekani pia alishinda na kufanikiwa kuuangusha utawala wa dikiteta gadafi,[emoji1258][emoji1258][emoji123][emoji123]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Mnaoenda ushabiki na unazi, msijifanye mnajua kuliko Serikali za Russia, Ukraine na NATO. Punguzeni kujua…. Mnayoyapata huku ni masalia yanaitwa Propaganda.

Urussi wamesema hili, mla mihogo hapa Sengerema anapinga kwa nguvu zote. Yaani yeye ana Intel kuliko za Kremlin, kuliko za Uk na kuliko za huko Kyiv .

Tupeane tu updates na mawazo yetu , Tusijifanye tunajua zaid kuhusu Intels babu
 
Yaani kuna paragraph umeongea Pumba eti Scotland ijitenge na Uingereza kwa mtutu wa Bunduki..

Pro Russia Mnaa kili Matope sana

Leta maoni yako mbadala - mnapo kosa hoja za maana mnaishia kutukana watu kwamba wana akili za matope mara oh unazungumza pumba mambo ya kitoto toto tu - mtu mwenye elimu nzuri na uelewa wa kutosha hawezi ku-stoop so low na kuanza kuwatukana members wenzake out of the blue, tabia hizo zinadhilisha kitu kimoja nacho ni kwamba kumbe you're still mentally immature-ndicho ninacho kiona mimi!!

Kama kwenye ufafanuzi wangu kuna kitu ambacho hukukielewa vizuri ungeniuliza ili ni clarify zaidi, mfano: nilizungumzia suala la Scotland - wewe kwa akili zako ulifikiri ninacho kisema ni kama ndoto za mchana au, si ajabu huna hata habari kwamba watu wa Scotland wanazungumza lugha yao tofauti ambayo si kiingereza wana tamaduni zao tofauti kabisa na tamaduni za England, wanataka kujitenga na England wawe na Serikari yao na Bunge lao, visima vya mafuta na gesi vya North Sea wanataka viwe mali yao na madai mengine chungu mzima, je wewe hayo unayajua au unapinga tu hutaki members wengine walete maoni mbadala ili members ambao wako interested wajifunze kitu.
 
Hoja hii inapingana na swali kwann Nato wasimvamie na kumtoa kwa nguvu pale Ukrain kama walivuotaka kufanya Syria ,Libya ,au jiulize kwann marekan anatumia washirika ktk kuikabili urusi, hapo ndipo utajua uwezo halisi wa kijeshi wa urusi mkuu,
 
Ripoti murua kabisa
 
Mkuu sina uhakika wewe unajuaje kivipi kile ambacho mimi najua au sijui?? Angalau najua kuna mambo ambayo siyajui.
Pia sina uhakika picha yako ya historia unapata wapi? Labda uangalie orodha ifuatayo List of wars involving the United States - Wikipedia na uhakikishe kama bado ungerudia yale uliyoandika. Nakubali kabisa kwamba hasa katika Asia Kusini-Mashariki walijiingiza katika vita ambako hawakuwa tayari kuwekeza nguvu ya kutosha kuzimaliza; na Vietnam walikuwa na hali inayofanana kidogo na hali ya Urusi katika ukraine wakiingia kwa kuamnini adui anaweza kupuuzwa na wenyewe wanaweza tu. BAsi walistahili kupigwa kabisa.
Ila ile vita kubwa na hatari zaidi (ambayo haitajwi katika orodha) walishinda kwa namna mbili: Vita Baridi (hadi 1990) wallipofaulu kutoingia katika Vita ya Moto na pili kumshinda mpinzani yaani Umoja wa Kisovyeti.
Unaonaje?
 
Hoja hii inapingana na swali kwann Nato wasimvamie na kumtoa kwa nguvu pale Ukrain kama walivuotaka kufanya Syria ,Libya ,au jiulize kwann marekan anatumia washirika ktk kuikabili urusi, hapo ndipo utajua uwezo halisi wa kijeshi wa urusi mkuu,
Mkuu, asante kwa jibu lako. Hadi sasa ninaelewa ni silaha za nyuklia pekee na hofu ya matumizi zao zinazozuia mashambulio ya moja kwa moja dhidi ya Urusi; pia siasa ya Marekani na Waingereza ambao wanakataa kuwapa Ukraine habari kuhusu shabaha ndani ya Urusi, ilhali wanawapa picha na habari zote kuhusu miendo ya Warusi ndani ya Ukraine...
Ila udhaifu wa jeshi hili kubwa kwenye ardhi ya Ukraine - kama habari hizi kuhusu rushwa na ufisadi ndani ya jeshi la Urusi (jinsi inavyosemekana katika dola la Urusi kwa jumla) zina ukweli, naelewa vizuri zaidi sababu za kukwama
 
Kuna balaa ila naona putin inabidi wam_eliminate sio kiumbe ambae tuna maslahi nae kama wana wa dunia hii!! Alitaka kudhihirisha ubabe ila mambo yameenda tofauti kabisa ss ana tuhatarisha wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…