Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kama jambazi anakuwa anarudia rudia kuja kukunyang'anya mali zako dawa ni kupambana nawe ukiendelea kumchekea na kuwa muungwana kwake ipo siku atakuoa kabisa.
Kama Zelenski angekuwa muungwana haya yote yasingetokea.
Jambazi anakuja ndani mwako anakuambia lete pesa zote ulizo nazo. Wewe unajua pesa iko kabatini badala ya kuitoa ubaki salama unajifanya kidume mbegu kuwa mbabe.
Kwa hakika utapigwa kama ngoma na ngumi ya ndoige. Unaeza ukawa kilema au kufariki.
(PESA NA MALI ZINATAFUTWA ILA UHAI UKIENDA UMEENDA)
Ndio jambazi anaeza kukamatwa na polisi akahukumiwa maisha jela au kifungo au wananchi wakamkamata na kumpa kipigo cha mbwa mwizi.
Au jambazi anaeza kutoroka asikamatwe na akaenda kula raha dubai na makahaba huku wewe ukiugulia.
Russia ni jambazi na aliyevamiwa ni Ukraine. .
Ukraine angetumia busara haya yote yasingetokea.
Sasa hivi alipo ni kipigo tu kila siku nchi inaharibika na matatizo kede kede huku mrusi akila bata Moscow.
Nb: Mpaka Nzi atakapotua kwenye korodani ndipo utajua si kila tatizo linaamuliwa kwa ubabe na manguvu.
Ukraine kalitambua hili huku kashachelewa. Anapigwa kama ngoma!!!