T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,924
- 47,173
Mkuu hapo Kherson hicho kipande tiyari Ukraine ishasema inaenda kukishambulia kabla ya leo. Tena wataalamu wanasema walikuwa waanzishe bridgehead kwenye hiyo kona hapo mbele ya Kakhovka maana mto ni mpaka sana Russia ndio pagumu sana kuwa supplied na Russia. Kisha wangepiga hapo juu kulia ya Snihurivka kukata kipande kukizingiraNimesikia mshauli wa rais wa Ukraine akisema kuwa bado Urusi hajaondoka kherson na Ukraine haiwezi kuingia kwenye mtego wa kijinga ulitegwa na Urusi.
Ukraine haitaki kupoteza wanajeshi wengi. Haipendi kupiga kwa sifa inawapa pressure sehemu fulani wanaretreat. Ndio maana sometimes inatangaza inaenda shambulia wapi ili Warusi waondoke. Haishtukizi kushambulia ila hawa pro Russia unawakuta humu wanashangilia "hiyo Kherson mliyosema mnakomboa tangu mwezi jana mbona tunayo". Kumbe Ukraine imewaachia fupa gumu. Imepiga supply lines sasa majenerali muamue majeshi yenu yavamiwe yakiwa hayana supplies za kutosha na hayana uwezo wa kuretreat bila mashambulizi, muambulie kuua Ukrainians kadhaa ila mwishowe mpigwe eneo hilo. Au muondoke bila kuwaua Ukrainians wachache ila muokoe wanajeshi wenu na silaha zenu kisha mkazipange sehemu mliyo na advantage kulinda.
Tabia ya kufa kishujaa ni doctrine ya USSR/Russia. Majeshi kama British au Israel wenye population ndogo na wanaotumia gharama sana kufundisha wanasisitiza kuepuka kupoteza wanajeshi kizembe. Ukimcheki Marshal Zukhov au Marshal Rokossovsky wa USSR na Field Marshall Montgomery wa Britain kwenye WW2 utaelewa kwanini Russia ilipoteza wanajeshi wengi mno kuliko wenzake