Bosi wenu vip unakubaliana naye au unampinga?
View attachment 2416469
NATO inaichukulia serious Russia, hapo Secretary kafanya comparison ya Russia dhidi ya Ukraine na mwenye akili yeyote anajua uwezo wa Russia dhidi ya Ukraine ambayo haikuwa hata within 20 of the greatest militaries kabla ya vita. Russia inajiamini na kujiona inajua sana na inajizidishia uwezo kwa imani sio kwa vitendo.
Huwa nawaambia huwezi nambia nchi isiyojua kutengeneza camera, laptop, magari ya kisasa, vifaa vya ujenzi, meli, smartphone na bidhaa nyingine muhimu kwenye soko la dunia eti inaweza kutengeneza silaha nzuri. Ni kwa sababu hatukuwa tunakutanisha silaha zao hawa, ila ukileta American made, German made au British made tank, jet, warship, missile dhidi ya Russian opponent Mrusi anapotezwa kwenye battle.
Nyinyi mnaoshabikia Russia humu mkipewa zile Lada zao mtazichukua kama mbadala wa Mercedes Benz, Ford, RR, Toyota, Volkswagen na wenzake? Kwanza wengi wenu hizo Lada hamzijui hata. Sasa nchi isiyoweza tengeneza gari la uhakika la barabarani iweze vipi kutengeneza kifaru cha uhakika.
Kwenye kazi zenu za engineering mnatumia CAT, HITACHI, JCB, Sany, Liebherr na Wachina wengine. Kwenye majenereta ya emergency hospitalini na maofisi makubwa na hospitali mnatumia Siemens, Honda, Triton, Cummins, CAT. Huyo Mrusi anakuwaje mkubwa vitani na uraiani awe mnyonge.
Nawaambia ukweli, mnapotoshwa na magwaride nyie. Hata mimi nilikuwa kama nyinyi