Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] lini tunarudi kuichukua mji wa Kherson?
Huwa napenda comment zako kwani Zina staha...ila uwe mvumilivu Mambo yakibadilika usiwe unakimbia Uzi...muda siyo mrefu Mambo yataanza Tena kuikandamiza Ukraine kibabe...
Kwa Sasa Ukraine anafanya PR subiri mapigo mfululizo yanayokuja...I am writing from experience the way I know Russians...
 
Nimesoma sehemu jana kuwa kuna mzigo wa shaheed na missiles 1300 zinakuja Urusi.

Huenda ndo sababu ya Ukraine kupewa air defences zakutosha

Hivi Tanzania tuna air defence?
Tanzania tunategemea Buk SAM systems za Soviet era. Kama iliyoangusha ndege ya Malaysia pale Ukraine mwaka 2014 kama sikosei. Sio za kisasa, ila huwa sipendi kuisema JWTZ nitaonekana sio mzalendo. Wabongo wanataka usifie ambapo hakuna.

Hizo Shaheed zinatumika kumaliza missiles za Ukraine maana zile interceptors zina gharama kubwa. Ukituma Shaheed zikadondoshwa mara zikiacha kudondoshwa unajua hawa wameishiwa interceptors unatuma cruise missiles kama Kalibr. Israel ingeingia ulingoni ndio tungepata dawa halisi ya hizo Shaheed maana dawa ya silaha ya Iran anayo Israel anayekutana nazo miaka yote
 
Kwa sasa ngoja tufurahie kurudishwa kwa jiji la kherson.Hayo mengine tutajua utakapofika muda wa kuvuka mto.
Hilo jiji la Kherson for military strategist is nothing...it is better without Kherson at the moment...Worse things are in store for Ukraine in a few days to come...That is why NATO is worried..And that is why there are calls from various actors in the international system to Zelensky to aim for negotiations before it is too late...
 
Japo ukosoaji ndo unasaidia mtu kubadilika.

Kwa Ukraine nahisi kuna kitu wanaunda na wao ili wapeleke maumivu upande wa pili. Maana wanajua kabisa wasipojiongeza wataumia
 
Bosi wenu vip unakubaliana naye au unampinga?View attachment 2416469
NATO inaichukulia serious Russia, hapo Secretary kafanya comparison ya Russia dhidi ya Ukraine na mwenye akili yeyote anajua uwezo wa Russia dhidi ya Ukraine ambayo haikuwa hata within 20 of the greatest militaries kabla ya vita. Russia inajiamini na kujiona inajua sana na inajizidishia uwezo kwa imani sio kwa vitendo.

Huwa nawaambia huwezi nambia nchi isiyojua kutengeneza camera, laptop, magari ya kisasa, vifaa vya ujenzi, meli, smartphone na bidhaa nyingine muhimu kwenye soko la dunia eti inaweza kutengeneza silaha nzuri. Ni kwa sababu hatukuwa tunakutanisha silaha zao hawa, ila ukileta American made, German made au British made tank, jet, warship, missile dhidi ya Russian opponent Mrusi anapotezwa kwenye battle.

Nyinyi mnaoshabikia Russia humu mkipewa zile Lada zao mtazichukua kama mbadala wa Mercedes Benz, Ford, RR, Toyota, Volkswagen na wenzake? Kwanza wengi wenu hizo Lada hamzijui hata. Sasa nchi isiyoweza tengeneza gari la uhakika la barabarani iweze vipi kutengeneza kifaru cha uhakika.

Kwenye kazi zenu za engineering mnatumia CAT, HITACHI, JCB, Sany, Liebherr na Wachina wengine. Kwenye majenereta ya emergency hospitalini na maofisi makubwa na hospitali mnatumia Siemens, Honda, Triton, Cummins, CAT. Huyo Mrusi anakuwaje mkubwa vitani na uraiani awe mnyonge.

Nawaambia ukweli, mnapotoshwa na magwaride nyie. Hata mimi nilikuwa kama nyinyi
 
Japo ukosoaji ndo unasaidia mtu kubadilika.

Kwa Ukraine nahisi kuna kitu wanaunda na wao ili wapeleke maumivu upande wa pili. Maana wanajua kabisa wasipojiongeza wataumia
Wako wanaunda kamikaze drone. Nadhani unajua Ukraine wasivyo wageni kwenye aerospace engineering na hadi MotorSich iliacha kuwauzia Warusi injinia za helikopta walipovamia
 
Sasa kupiga maeneo ya raia wasio nahata manati siniutaahira huo?

Piga sehemu yenye wanajeshi.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Mji wa kherson unajua umeanzia wapi nakumalizia wapi

Hizi MSM zinawadanganya sana nyie watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hata Urusi nadhani alipochukua yale maeneo kuna sehemu majeshi ya Ukraine walikuwa bado wameshika na ilikubalika kuwa Ukraine imenyang'anywa eneo. Kwa hapa usione aibu kuipongeza Ukraine kwa alichofanya mpaka pale mambo yatakapobadilika.
 
Hizo NASAMS hujui kwamba hata kutengenezwa zilikuwa bado? Yani zikitolewa kwenye factory ndio zinaenda Ukraine. Gepards zilikuwa kwenye storage facilities na zilihitajika kurekebishwa ndio ziende Ukraine. Na nyinyi air defence zenu hazina lolote mnaficha aibu kwa vile Ukraine haina silaha za kushambulia kwenu. By the way tumeona Moskva imeshambuliwa, Snake island ikiwa na AD systems imeshambuliwa na video zipo, makao makuu ya Black Sea fleet yalishambuliwa, kituo cha umeme Belgorod

Pia silaha za NATO huwa haziendi kwa mbumbumbu, lazima wapewe mafunzo makali ya kuzitumia. Marekani hutumia 2 years kufundisha air defence operators. Hawa Ukrainians wanaofundishwa systems mpya kabisa kwao wanatumia muda mfupi sana. Hizi sio kama silaha zenu za Warusi ambazo accountant anakamatwa uko mjini anafanyiwa mobilization anapewa kifaru aendeshe kikifeli kidogo tu anatelekeza. Ndio maana kila retreat mnaacha vifaa kibao nyuma vikiwa intact
 
Mkuu hata Urusi nadhani alipochukua yale maeneo kuna sehemu majeshi ya Ukraine walikuwa bado wameshika na ilikubalika kuwa Ukraine imenyang'anywa eneo. Kwa hapa usione aibu kuipongeza Ukraine kwa alichofanya mpaka pale mambo yatakapobadilika.
Wakati kheson ikijiunga na urusi ulisema kwamba wananchi wa Ukraine wameamua kwa mapenzi Yao wenyewe kuwa sehemu ya Russia..,tukakuambia kwamba kile ni kiinimacho Wala hakuna referendum, ukakataa kata kata huku ukisema kwamba wananchi walitakiwa kuonesha hisia zao kuukataa kuwa sehemu ya Russia..,Leo hii mji wa kheson umerudi mikononi mwa ukraine.., hatuoni wale walipopiga kura kujiunga na urusi wakiandamana wakidai kuendelea kuwa sehemu ya Russia..,kwa Hali hii umejifunza nini?

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Nimejifunza kuwa sikuwa sahihi katika hilo.
 
What do you expect kutoka kwa Hawa watu si hawa walisema sadam ana silaha mbaya za hatari?? Hawa ni mashetani
 
Wako wanaunda kamikaze drone. Nadhani unajua Ukraine wasivyo wageni kwenye aerospace engineering na hadi MotorSich iliacha kuwauzia Warusi injinia za helikopta walipovamia
Nimeona pia wanafanya fundrise ya USV kama zile zilizofanya shambulizi juzi kati
 
kweli bwana utamu utakua umelewa saa hii.. anaesonga mbele na anayerudi nyuma nani ndo anampiga mwenzake? 🙄 wenzako washachinjwa laki moja
 
Russia wanapaswa kuimaliza hii kadhia. Hii SMO inamgharimu sana.
Unashindwa kutambua Ukraine kama Ukraine ilishamalizwa siku nyingi sana?
Hujui kua west,na wala Sasa sio NATO Tena,Bali ni west wote wanapigana na Urusi kwa kuchangishana silaha,fedha na taarifa za Kijasusi kwa kumpa Ukraine?
Magenerali wote wa west kazi ni kuchakata mipango ya vita na kuipatia Ukraine?
Hujui kua Kuna askari wengi wa kulikodiwa wanapigana upande wa NATO na Ukraine..
Kama unaangalia vita hii kiumakinj nakuambia nchi ya kupongezwa ni Russia.
Hebu fikiria vikwazo kwa urusi,na michango ya silaha anayopewa Ukraine.
Na hapo kubali kataa Urusi hajaingiza jeshi lake lote,anasubiri upepo ukibadilika,yaani NATO waliingiza majeshi sio hivi vimisaada.
Baba usiidharau Urusi Hadi hapo vita ilipofikia.
NATO walidhani watailaza mapema Urusi hasa baada ya kuiwekea mavikwazo yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…