Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Bado nipo palepale kwanini uone kosa Ukraine kushambulia ndani ya Urusi?! Kama Russia anashambulia mpk apartments na mashule ndani ya Ukraine kwanini isiwe halali kwa Ukraine kufanya mashambulizi ndani ya Urusi?!

Kulipuliwa Kwa Daraja la Crimea si sababu ya Urusi kuanza kushambulia miundombinu ndani ya Ukraine sababu Peskovu mwenyewe alikiri kwamba wanashambulia miundombinu ya nishati na mingineyo ili kuifosi Ukraine ikubali mazungumzo,juzi hapa Russia ilisuggest kuwe na short truce Ukraine ilikataa na mpaka sasa sioni Zelenksy akikubali kufanya mazungumzo na Putin kisa eti Putin kabomoa miundombinu ya Umeme.

Kama mnangoja Ukraine ipige magoti kwa Russia kisa kulipuliwa Kwa transfoma za Umeme mtasubiri Sana.
 
Hii ndio 'Russian Apache'.....wanadai sio nzuri Sana kwenye mission za usiku.
T14 Armata
Sio Ka-52 pekee hata Mil Mi-28 ambayo vita hii sijaona kwa sana bado nayo haifanyi vizuri usiku. Kwa Apache ya Marekani ile hata ukionyeshwa night footage utakubali kuwa usiku inaona vizuri kwa kutumia various sensors.

Tatizo la night vision kwa Russia nishaligusia humu, defense industry ya Russia haiko vizuri kwenye teknolojia ya kuona usiku. Scopes za bunduki somehow sio ngumu ila hawana the best kama wengine. Kwenye vifaru Ukraine walipokamata T-90M pale Kharkiv ambayo ndio latest Russian tank kwenye inventory ilienda kuchunguzwa na NATO na labda watatoa majibu. Previously vifaru vya Urusi vilivyokuwa vinakamatwa miaka ya nyuma vilikuwa na weakness kwenye aiming systems kama thermal sites, uwezo wake kufanya aiming usiku unapungua maradufu. Naamini Wachina washawapita kwenye hilo
 
Mazungumzo ya nini uwanja wa Vita.acha boli litembee.Putin kashasema kabisa ukija kwa ajili ya mazungumzo basi kabla ujaingia kwenye chumba cha mazungumzo basi unatakiwa kutambua mikoa aliyoichukua Urusi, ni sehemu ya ardhi ya Urusi.kama uwezi basi haina aja ya kuingia kwenye chumba cha mazungumzo
 

Huo upuuzi wake anaujua yeye na machizi wenzake maana alianza na mbwembwe za kutisha nyuklia kama hayo maeneo yaliyopiga kura yatashambuliwa baada ya kuona mkwara haujazaa matunda ss hv kaufyata na hayo maeneo yote yanachezea Makombora km kawa. Hiyo mikoa ni ya Urusi kwenye makaratasi lkn halisia watachezea mkong'oto mpk watakimbia wenyewe km walivyokimbia Kharkiv na Kherson.
 
Una mapenzi mazito sana na USA.sijui kama wenyewe wanajua kuwa unawapenda kupitiliza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hoja sio uharamu au uhalali!? Pia, Nothing is fair in this world when it comes to love and War. Sio kwa sababu wewe umefanyiwa basi ni halali na wewe umfanyie aliyekufanyia. NATO wanajua kwamba ardhi ya Ukraine imeshambuliwa vby na urusi lkn hawataki kumuona Ukraine anaishambulia ardhi ya urusi. NATO wanajua haitakikani kupigana vita ambayo hupati chochote hata ukiishinda na ukiishindwa unapoteza kila kitu. Umefanikiwa kushambulia daraja sawa, umepata nini!? Wiki mbili baadae daraja limejengwa upya na wewe raia wako milioni 10 wanaihama nchi kukimbia baridi na wanaobaki wanaunga foleni na ndoo za maji kama wako makongo juu huku umeme hauwaki na hali ya uwanja wa vita haibadiliki. A lot of doing but nothing done!

Hakuna anayemtaka zelensky akapige magoti. Haijawahi kutokea kwenye historia ya dunia mtu kupiga magoti kwa kushindwa vita hata Saddam alinyongwa akiwa amesimama. wasiotaka Mashambulizi yafanyike ndani ya Urusi ni wote wenye busara wakiongozwa na NATO ambao ndio wadhamini wakuu wa Zelensky. Sio wanaomsubiri zelensky akapige magoti. Kwanza hakuna watu hao.

Hakuna anayetaka kuona nuclear inatua kyiv. Mbungi ipo sebuleni kwake zelensky apambane hapo hapo. Asitake kuumusha mgogoro kwa vishambulizi uchwara. Akikaza kalio labda atawashinda warusi na kuwalazimisha kuondoka kwenye ardhi yao but that is a very big freakin MAYBE
 
Wanajifanya hawaoni au niwataje kabisa. Nyie Warusi wa Kakonko mbona airbase yenu inashambuliwa na mnasema mna au defense systems nzuri zaidi duniani huku mnaishangaa Ukraine yenye systems chache za kupewa ikishambuliwa
Na Leo imepigwa nyingine [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanajifanya hawaoni au niwataje kabisa. Nyie Warusi wa Kakonko mbona airbase yenu inashambuliwa na mnasema mna au defense systems nzuri zaidi duniani huku mnaishangaa Ukraine yenye systems chache za kupewa ikishambuliwa
Kushambuliwa kwa RUSSIA hakuuondoi ukweli wakwamba ana best AD

Au best AD hua haziruhusu shambulizi hata kidogo

Katika zile AD kutoka OTAN walizopewa UKRAINE zimeisaidia nn UKRAINE kwamba haijashambuliwa toka ipokee ama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukraine ina AD systems ngapi alizoanza kupewa mwishoni mwa mwaka huu? Sasa unalinganisha Russia inayotengeneza systems miaka yote hiyo na bado inapigwa kila shambulizi, hakuna shambulizi kubwa Ukraine wamefanya likazuiwa na hizo systems ila kuna mashambulizi Russia imefanya na yanazuiwa kwa kiasi chake.

Years of defence spending, manufacturing, training na stocking ya the so called superpower huyo Russia mbona matokeo hamna
 
Hakuna sehem nimezifananisha

Ila yamezuia nini UKRAINE mwisho jana imepigwa na wanalalama lalama

[emoji96] In the aftermath of yesterday's strikes on Ukraine, Kiev officials say it will take 2 days for the system to stabilize in order to at least partially return to the previous system of "predicted rolling blackouts", as now a wave of emergency power outages is rolling across Ukraine, accompanied by massive accidents in the power grids.

@NewResistance

Huko RUSSIA mashambulizi mangapi wanasema wanazuia toka UKRONAZI jamaa wanapambana nayo sanaaa

Ama hufatilii na hayo mashambulio makubwa walofanya UKRAINE huko RUSSIA kama yapi yakafanikiwa !!!??


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chizi wewe sio mzima kabisa.mara ngapi mifumo ya Urusi inatungua drone na makombola.au unataka mpaka waje kwenye kiota chako wakwambie.

Shida mnapenda sifa kama vile nyie sio binadamu,mnaisifia mifumo ya magharibi wakati ukweli hamna mifumo pale
 
Huyo bwana wako Marekani pamoja na kutengeneza mifumo kila siku base zake zinapigwa Syria.
 
Nadhani ulishawahi kusikia kuhusu Sputnik.
Siku moja october 1957 asubuhi USA wanaamka na habari kwamba Soviet wamerusha satellite ipo kwenye orbit inazunguka, lakini habari hii ilikuwa imepokelewa tofauti na majenerali wa jeshi la USA , kwamba Soviets wanaweza rusha kombra la nuke sehemu yeyote ile ndani ya USA provided kwamba wana weza rusha satellite kwenye orbit.
Hiko kiliwashtua sana USA, kwa sababu bado walikuwa hawajafikia huo uwezo.

Rocket science ambayo huwa inachukuliwa ni ngumu wenzako wamefanya 1957, soviets wapo mbali sana muda mrefu. Endelea kurefer Mi-28 na vifaru kwamba ndio silaha ambazo zinaonyesha udhaifu wa Russia, Russia hailindwi kwa Mi-28 na vifaru vya T-90M mkuu, helicopter ya Mi-28 na kifaru cha T-90M sio kielelezo kuelezea uwezo, morali, teknolojia na nguvu waliyonayo Russia unless uwe ushabiki.

Tukianza kuelezea weakness ya silaha za NATO kwenye vita ya Ukraine hatutomaliza.

Nimekuambatanishia gazeti la New York Times 1957 october USA wakishangazwa na satellite hio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…