Sawa hiyo ni tafasiri Yako.
Lakini je unaweza kunieleza tofauti hii safari hii inasababishwa na Nini?
USA na NATO wakipeleka majeshi kamili huko ghuba kwenda kuipiga Iraq kwa sababu Iraq iliivamia Kuwait.Hawakutuma silaha,Bali majeshi kamili yalienda Iraq.
NATO walipeleka majeshi kamili kwenda kuipiga Yugoslavia wakati Yugoslavia/Serbia walipokua wakiwapiga Kosovo,Bosnia na Herzegovina.Hawakutuma silaha,Bali majeshi kamili ya NATO yalienda Yugoslavia.
USA na baadhi ya washirika wa NATO kama Ufaransa walipeleka majeshi kamili Libya kwenda kuwapiga majeshi watiifu kwa Muamar Gadafi wakati wanajeshi hao walipokua wakiwapiga waasi waliokua wakimpinga Gadafi.Hawakutuma silaha ,Bali majeshi kamili ya USA na France na UK.
USA akisindikizwa na marafiki zake wa NATO alipeleka majeshi kamili Afghanistan kwenda kuwapiga Al-qaida na Watalaban,hawakuoeleka silaha kwa Northern Alliance wala namna yoyote Ile.
Kwa mara ya pili USA alikwenda mwenyewe kijeshi na washirika wake wa NATO kwenda kumpiga Sadam Husein wa Iraq kwa madai kua anatengeneza na kumiliki silaha za maangamizi.WMD.ambazo kiukweli Sadam hakua nazo.na kazi ya kumnang'anya silaha hizo ilitakiwa kufanywa na UN,lakini UN haikutoa ruhusa kwa USA lakini USA iliwakusanya mashoga zake na kwenda kijeshi kumpiga sadam.walipomshinda hawakukuta hata sumu ya Kuua panya.
USA ilikwenda Somalia kwa madai kuwasaidia watu waliokua wanateswa na waasi wababe wa kivita akila General Morgan, General Mohamed Farah Aidiid na wababbe wengine,haikutumia silaha kwa wasomali.
USA ilipelekea jeshi nchini panama kupigana na Jeshi la panama kwa madai kwamba Rais wa Panama bwana Mannuel Antonio Noriega anafanya biashara ya cocaine.
Hakupeleka silaha.jeshi la Marekani lilienda..
Kwa uchache ni hayo TU.
Sasa nataka uniambie ni kwa sababu Gani USA na NATO na west hawaingizi majeshi kamili kwenda kumuokoa Ukraine ambae anapewa kipigo ambacho kinawaumiza mno NATO.
Kinawaumiza kiasi ambacho hakuna nchi hata moja duniani iliwahi kupewa misaada ya kijeshi na fedha na logistics kama anayopewa Ukraine.
Silaha anazipewa Ukraine ni za kisasa mno,Bora mno na za gharama kubwa mno hakuna hata nchi moja iliyowahi kupewa misaada ya namna hiyo.
Inaonesha NATO wameguswa mno na mateso anayoyapitia Ukraine ni kwa Nini hawaingizi majeshi kamili?
Kumbuka hakuna nchi hata moja duniani ambayo imewekewa vikwazo vingi kama Urusi,hii yote ni katika kuisaidia Ukraine na kuiunga mkono,vikwazo hivyo vimeweza hata kuziathiri nchi za west.Hii inaonesha wameumizwa mno na mateso au mapito anayoyapitia Ukraine,je huoni hapo ndio ulikua ni fursa nzuri kabisa ya kupeleka majeshi Kili ya NATO?
Kwani anachopitia Ukraine kina tofauti Gani na walichopitia Akina Kosovo,Bosnia na hezegovina,Libya au waafghanistan?.
Hutaki unaacha.
Kauli ya Putin ilikua ni dhahiri kabisa na inaishi.
Hata Putin asingetoa kauli hiyo bado hakuna Cha NATO wala baba Yao NATO angethubutu kuingiza jeshi lake pale.
Kuingiza jeshi kunahitaji Ruhusa ya mabunge ya nchi husika.
Je Kuna bunge la nchi hata moja limeidhinisha jeshi lake kuingia Vitani dhidi ya Urusi?
Kupeleka silaha sio ruhusa rasmi ya vita,ndio maana hata Iran anapeleka silaha zake ili kuzijaribu.