Huyu Supa-pawa wa mchongo alikuzwa tu na propaganda za uongo ila kiuhalisia ukitoa hizo 'nyuklia' ni wa kawaida Sana.
Alikuzwa na nani???Vitu vingi mnajitengenezea wenyewe, mfano embu tafuta credible source yako halafu tupe list ya powerful countries (military power). Hao wazungu mnaowaabudu kama miungu watu ndo wanawatengenezeeni hizo list......au basi nao wanaongopa??
Ndo maana huwa tunasema tunaongea humu utafikiri watoto wa form four.......
"Et wa kawaida sana" kwa sababu unamapenzi tu...na unaandika tu na hisia.....Yaani hivyo vi drones vinavopenya na kuripuka ndo unatumia justification....
Wapalestina mara kibao wamewaotea wayahudi..(Utasema Israel wa kawaida kisa wapelistina wanawaoetea siku moja moja)
Wakurdi wanawasumbua kupita maelezo Turkey (Utasema Turkey ni wa kawaida)
Al Quida walifanikiwa kupenya mpaka wakalipua (Pentagon & NY ):Utasema Wamarekani wa Kawaida
US-Afghanistan wamekipiga 20 yrs...wameondoka..Taliban wamerudi (Utasema US wa kawaida)
Yemen pale Houthi...wanampa tabu Saudia Arabia pamoja na washirika wake..( Utamlinganisha Saudia na hao Houthi kweli...Hao Houthi wanarusha maroketi yanapenya tu utafikiri Saudia hajawekeza billions kwenye ulinzi)
US aliondoka Somalia 1994...(Utasema US wa kawaida)
Wa Viet-cong..walimpa tabu US..kaamua kusepa (Kweli utalinganisha USA na Vietnam:Utasema US wa kawaida)
Wa-Japan walimpa usumbufu wa ajabu USA kwenye vita vya pili..mpaka wakaamua kutumia nyuklia...Utasema USA wa kawaida sio-we unafikiri USA angeamua kukaza kwelikweli..hata bila nyuklia Japan asingesalimu?)
Haya Ujerumani ya Hilter alipokea kichapo baada ya miaka 6 ya kutwangana.....(Kwa akili zako utasema Ujerumani ya Hilter ilikuwa superpower ya mchongo..kisa tu alishindwa???
Waafrika tunawekaga chuki zetu mbele, utafikiri kuna kitu zitabadirisha....
Tunachambua vita utafikiri....ni ugomvi kati ya mke na mme..au Wakina Mandonga....
Aibu sana