Kwa hali jinsi inavyoendelea Ukraine haiwezi ikarudi mezani kama Russia inataka iwe hivyo! Russia kama inataka kuwarudisha Ukraine mezani inawabidi wafanye unyama wa hali ya juu utakaowafanya Ukraine wasalimu wenyewe amri!
Kwa sababu kwa aina ya mashambulizi wanayoyafanya sasa na tangu awali ijapokuwa ni yenye faida kwao ila kwa Ukraine ni kwamba bado wanaweza kuyahimili.
Ijapokuwa wanakufa wengi ila Ukraine bado wanayahimili anachokitafuta yeye kwa sasa ni kuleta hasara kwenye mambo muhimu kwa Russia. Ndiyo maana Zelensky anahangaika kuomba zana zenye uwezo wa kupenya moja kwa moja Russia na si kwamba hajui madhara yake bali wanachokitaka ni kumtia hasara Russia. Yaani umenipiga ila kwako nimeacha madhara makubwa na hasara kubwa. Na wakipata hiyo nafasi wanaitumia na ndiyo maana wanahangaika na mbinu za kigaidi. Yaani paaap! Kombora limetua Moscow kwao ni mafanikio makubwa hawatojali kuwa watatwangwa.
Haya yote yanatokana na nini? Haya yanatokana na aina ya mashambulizi Russia wanayoyafanya. Wasidhani kama hii hali wanaweza kui maintain muda wote. Muda wowote hali yoyote inaweza kubadilika.
Mbali na hapo kwa hii operation jinsi wanavyoiendesha hakuna kitakachobadilika na Russia inaweza ikapata madhara makubwa ijapokuwa linaweza likatokea moja moja ila yatakuwa ni makubwa yenye kuleta hasara kubwa kwao.
Wengi wa watu wataona mbn Ukraine wanafanya mambo yasiyotarajiwa kwenye ardhi ya urusi na urusi yuko tu idly by bila reaponse ya maana.
Kuna mambo mengi hapo na Urusi anaact kwa uangalifu sana with strategy wala sio kwa kukurupuka na mihemko. Mimi kwa mtazamo wangu nahisi response ya Urusi ni kinyume na inavyotarajiwa na wengi kwa sababu;-
1. Kwanza, Nyingi ya taarifa zinazoletwa zimejazwa chumvi. Propaganda. Inategemea na upande unapoptoa taarifa. Sasa hivi hata tukio la kawaida tu alimradi litaashiria udhaifu wa Urusi litahusishwa na vita. Situation kwenye ground ni tofauti kbs. Na Kremlin hawawezi fanya maamuzi kwa kufuata propaganda za namna hii. Inakuingia akilini anga la Ukraine linalolindwa na s300 drone zote zinazotumwa zinadunguliwa alaf anga la Urusi linalolindwa na s400 drone zikitumwa zinafika!? Basi ni muda tu hatuna ila tungeanza kuchambua kila taarifa ya kila tukio inayotumwa hapa kupitia vyanzo mbalimbali ili tujaribu kupata picha ya hali halisi ya propaganda kwenye hii saga.
2. Labda Response ya kukurupuka kutoka kwa Urusi ndio hasa kusudio la Ukraine! Urusi hawezi kucheza mziki/kwenda na mdundo wa Ukraine. Zipo sababu kwa nini Urusi hakuanza mashambulizi mazito hapo mwanzo. Sababu hizo hizo ndio zinazofanya anakwenda kwa step along tha way. Hakuna sababu ya kuacha plan yako ya vita ukikimbilia kujibu shambulio lililofeli la drone kwenye ardhi yako.
3. Urusi wanaupima uwezo wao wa kivita wenyewe na hawajali wengine wanasema nini! Hakuna haja ya kufanya mambo nje ya plan zako ili tu uprove kwa dunia kwamba unaweza. Ikiwa wewe unajua kwamba unaweza basi inatosha. The rest of the world's opinion doesn't matter. Lengo la propaganda na uongo kwenye baadhi ya report ni kuonesha udhaifu wa Urusi. Urusi yeye anajua sio dhaifu ndio maana hahitaji kufanya jambo kubwa ili tu aprove hasa kama hilo jambo haliko kwenye plans zake kwa sasa. Ndio maana Surovikin aliomba kuhamisha wanajeshi ukingo wa pili wa mto dnipro na akasifiwa na Shoigu licha ya kuwa the rest waliona kama ni dalili ya udhaifu. Haina haja ya kuabandon wanajeshi wako wafe eti unataka usionekane mdhaifu.
Mwisho, Wapo wanaosema Urusi hakutegemea kama vita ingechukua muda mrefu hivi. Pengine wao ndio hawakutegemea. Kwa mzigo wa vikwazo na misaada waliyompa Ukraine walikuwa na uhakika kbs it was only a matter of time kbl Urusi hajarudisha majeshi nyuma na kuregret kuingia Ukraine.
Vita kuchukua muda mrefu ni swala la kumpongeza Urusi considering all circumstances.
i. Misaada. Juzi Biden wamtetangaza kifurushi kingine cha msaada kwa Ukraine cha dola bilioni 45. Endapo kifurushi hiki kikipitishwa bungeni (which is most likely to happen) Kwa jumla ukichanganya na zile za mwanzo ni zaidi ya dola bilioni 90 kutoka US tu ndani ya miezi 10. Hicho ni kiwango kikubwa kuliko bajeti yote ya defence ya urusi kwa miezi 12. Bado msaada kutoka ulaya na mataifa mengine. Unawezaje kupigana na taifa linalosaidiwa namna hii kutoka mataifa yenye nguvu duniani kwa miezi kumi bila kuyumba huku ukifanya advances!?
ii. Mwanzo wanajeshi wa Urusi waliokuwa deployed Ukraine ni around laki 2.5 to 3. Hawa wanashikilia zaidi ya kilomita laki za mraba imagine hiyo line ya frontline ni ndefu kiasi gani kuanzia kharkiv mpk kherson!? Dhidi ya jeshi la Ukraine lililokuwa na wanajeshi 300k jumlisha mobilization iliyofanyika nchi nzima na wanaume kuzuiwa kutoka jumlisha maelf ya foreign mercenaries.
iii. Vikwazo
iv. Style ya upiganaji wa urusi yenye kujali zaidi maisha ya raia na wanajeshi wake.