Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ishu ya Urusi hakuna anayejua kuwa wamepoteza askari wangapi ni wao wenyewe wanajua , na hawajasema wala nini.
Ipa NATo wanajua Ukraine inaskari wangapi maana ni wao waliokuwa wanawapa mafunzo na siraha so wanaelewa kuwa wamepoteza askari wangapi.
Pro Russia bhana.

Kama watu walijua Russia ataivamia lini Ukraine watashindwa kuestimate waliokufa?
 
Ngoja nikuambie dogo ..mnamo mwaka 1989 (pengine ulikuwa hujazaliwa) kulikuwa na vuguvugu la maandamano ya wanafunzi pale beijing wakipinga mamlaka ...Waliokuwa msitari wa mbele ni wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu. Basi bwana waanfunzi wale wakajazana pale kwenye uwanja maarufu beijing na china nzima ujulikanao kama Tiananmen Square. Dola ya China ikatoa ultimatum kwa wanafunzi hao kuwa waondoke pale uwanjani. Wanafunzi wale wakapuuza. Dola ya China ikapeleka vifaru, lakini kwa kejeli kubwa wanafunzi wale kwa maelfu wakawa wanawakejeli askari wale kwenye vifaru ambao walikaa tuli wakisubiri amri. Vijana wale wengine wakadiriki hata kupanda juu ya vifaru na kuwakejeli askari...Wanafunzi kwa maelfu wakawa wanashinikizwa na nyimbo wakidai ni za kimapinduzi...ikumbukwe huko ulaya Mashariki dola kadhaa za kikomunisti zilikuwa zimeanguka tayari...Huko Soviet Union alikuwepo Mikhail Gorbachev na glasnost na perestroika yake. kwa China alikuwepo kiongozi wa kikomunsti Huo Yaobang ambaye inadaiwa alikuwa mwanamageuzi lakini akafa ghafla na ikawa chanzo cha wanafunzi kwa maelfu kuandamana wakishinikiza reforms.
China ikatoa ultmatum tena kwa wanafunzi hao waondoke lakini wakakaidi. basi bwana usiku mmoja ukaingia na wanafunzi wakaendelea na vitimbwi vyao. Asubuhi moja watu wakaamka lakini wasiwaone maelfu ya wanafunzi pale uwanjani. Dunia ikashangaa na wengine na hasa USA na West wakahamaki. Vifaru usiku ule vilifanya kazi yao. Lakini hakuna hata tone la damu lilionekana uwanjani pale. Na wala hakuna hata picha moja iliyopigwa kudhihirisha 'mauaji' yale ya kutisha. inadaiwa wanafunzi wale waliokuwepo uwanjani pale walikanyagwa kanyagwa kama udongo. inadaiwa usiku ule ule uwanja ukasafishwa hata tone la damu hakuna. Na wala ushahidi haupo. Mawasiliano yote ndani ya China yalikuwa jammed. Hata satellites za kibeberu hazikuweza kupiga picha hata moja.
Huo ukawa mwanzo na mwisho wa vuguvugu la kinachoitwa reforms huko China. Communist Party ikaendelea kushika dola mpaka leo. Kale kanafunzi kalikokuwa kanaongoza maandamano hayo kakaenda Marekani baadaye. Inasemekana hakukuwepo uwanjani wakati wa tukio, kalikuwa kamejificha mahali huku kakiwachagiza wenzake waendelee na maandamano.

Wewe Acha kufanya watu wote matahira au hawana hizo information,video za maandamano ya Tianamen Square mpaka YouTube zipo wewe unakuja kupiga fix hapa eti hakukua hata na tone la damu,Aiseee ongopea watoto wenzako


Kama hakukua na ushahidi ilikuaje baada ya lile tukio Uchina ilipigwa sanctions na West?!

Kama Urusi kweli iliua wanajeshi 600 na kwenye eneo la tukio hakukua hata na ambulance wala aina yoyote ya vikosi vya Ukraine hiyo miili yote 600 ilienda wapi?! Au ndo ilikua ndani ya Yale mahandaki yaliyochimbwa na Makombora yao?!
 
Back
Top Bottom