USA alitamka mwanzo kua Urusi itaivamia Ukraine mwezi Feb 2022.
Wengi wanadhani ni uwezo mkubwa wa intelligence ya USA,lkn sio,Bali ni kutokana na mtililiko wa matukio.
Kabla ya SMO kuanza Urusi ilifanya juhudi kubwa sana kuepusha vita hii kutokea.
Urusi ilikua Kila siku inaiomba Ukraine kubaki nyutro yaani kubaki bila kuegemea upande wowote lkn Ukraine ikadharau.
Urusi iliiomba USA isiruhusu Ukraine kujiunga na NATO,USA ikadharau,Urusi ikaziomba nchi za NATO zisiipe Ukraine uanachama wa NATO,wakadharau.ingawa haikua imejiunga bado lkn maandalizi ya kujiunga yalikia yanaendelea kiaina.
Urusi ikaziandikia barua nchi za NATO na hasa USA juu ya ombi lake,hawakuweza hata kumjibu.
Wakati hayo yakiendelea Ukraine ikaendelea kuvunja mkataba wa minsk.ikiwa ni pamoja na kuwapiga wa donesk na WA luhansk.
Urusi ikachora mstari mwekundu kwa NATO na Ukraine,wakivuka isije ikalaumiwa.wakavuka bana.
USA na Russia ni maadui wakubwa lkn wenye vikao vingi sana kuhusu usalama wao na WA dunia.wanajuana sana kitabia.
Hivyo baada ya juhudi zote za Urusi kutafuta maridhiano kushindikana USA ikasoma tabia za Urusi kwani walikua kua wamewakatalia maombi Yao yote na wamechora mstari mwekundu hivyo watafanya Nini,Urusi wakanza maandalizi Huku USA akifatilia kwa umakini mkubwa ndipo akatoa tahadhari kua Urusi ataivamia Ukraine mwezi Feb.
Nao USA Kwa malengo Yao ya kuidhoofisha Urusi kwa njia hii wakafurahi kua hatimae Urusi imeingia kwenye mtego.
Suala la vikwazo halikuja kwa bahati mbaya au michango ya silaha haikua Kwa bahati mbaya,Bali ni mipango iliyokuwepo kwa Nia ya kuidhoofisha Urusi kijeshi na kiuchumi,mtego ulikua ni kua akianzisha vita na Ukraine atamalizwa kwa vikwazo vikali sana na vita ya mda mrefu.
Ni dhahiri USA hawakua na taarifa za kutosha juu ya uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa Urusi.
SMO ilipoanza USA ilitoa tamko kuwa nchi yoyote isijaribu kuisaidia Urusi.,hapa walilenga kijeshi zaidi,walikua kua itafika mahali Urusi itazidiwa,ama itaishiwa sulaha ama fedha na itadhoofika nalo lengo lao litakuja limetimia.
Tamko hilo lililengwa zaidi kwa china,kua huenda china ikaisaidia Urusi,lakini china kwanza walilipuuza na kusema Urusi ina uwezo wa kupigana peke yake,haihitaji msaada wowote.
USA hawakua na taarifa za kutosha juu ya uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa Urusi kwa sababu Hadi Sasa Urusi haijaishiwa silaha kama walivyokua wanadhania USA na NATO,Cha ajabu Kila siku Urusi anapeleka silaha mpya kwa njia ya barabara na reli,Tena sio kutoka makambi mengine Bali mpya kabisa huenda kutoka viwandani.
Cha kushangaza zaidi waliokua wanasema ataishilwa silaha wao ndio wamekua.wa kwanza kulalamika kua maghala Yao ya silaha yamepungukiwa na silaha,zimebaki za akina,wameshasema hivyo USA, UK,Poland,German,Canada na NATO wengine.
Kilio hiki sio kwenye silaha TU,Bali kimesikika pia kwenye uchumi.tumeona tumesikia na kusoma kua sio ulaya TU Bali hata USA maisha yamepanda,ajira zimeshuka,vitu vimeoanda bei hakuna nishati na uchumi kuanza kuporomoka.urusi bado Iko ngangari.
Hatukatai hata yeye kwa sababu alikua anafanya nao biashara kwa namna moja ama nyingine lazime ayumbe hasa kwenye masoko.
Lakini kaweza kugeuza shingo na Sasa anafanya sana biashara na nchi za Asia hasa zile zenye idadi kubwa ya watu mfano chinana India pamoja na mataifa mengine.
Hali hii USA na NATO hawakuitegemea hata.
Kibaya zaidi Kuna nchi kubwa kiuchumi hazijaitenga Urusi kama vile Saud Arabia na nchi nyingine za kiarabu na mashariki ya mbali.
NATO wakiingilia kijeshi Kuna nchi lazima zitaingia vitani upande wa Urusi,nasema lazima kwa sababu ya mahusiano ya nchi hizo na USA.
Nchi amabzo ni wazi zitaingia kupigana pamoja na Urusi ni zile nchi zinazochukiwa sana na USA,zinazowindwa sana na USA na zinazoshutumiwa sana na USA.
Nchi hizi hata kama haziungwi mkono hadharani kijeshi na Urusi lakini USA anashindwa kuzivamia kwa sababu anajua Urusi atazisaidia,na nchi hizo zinajua fika kua NATO waliingiza majeshi kumsaidia Ukraine na Urusi ikatokea akashindwa basi nazo n hi hizo zitaenda na maji,yaani zitapigwa na kuwekwa chini ya mikono ya USA,kwa hiyo kuliko kumuacha Urusi ashindwe ni Bora zisaidiane na Urusi kwa ajili ya usalama wao.nchi hizo ni china,Korea Kaskazini na iran.kuna nchi ziko marafiki na Urusi lakini hazina bifu na USA,hizi zitaweza kuingia Vitani pia lkn hizo tatu nilizozitaja kama Urusi akishindwa maisha mustakabali wao utakua Mgumu mno.
Tuziangalie uwezo wao kijeshi na mchango hatuhitaji maelezo mengi wote tuanjua uwezo wa kijeshi wa nchi hizo na ukilinganisha na baadhi ya nchi za ulaya ama NATO.
Maajabu ya kujimudu Urusi kijeshi na kiuchumi katika vita hii ni kama yalipangwa.
Urusi ilijipanga kwa haya yanayotokea Leo hii kinyume kabisa na matarajio ya USA
Urusi na USA zimekua zikisomana Kila siku,ila Kwa hapa Urusi alimsoma USA kitabia hatua kumi mbele,tabia za USA zinatia mashaka mno na ni rahisi kujua matarajio yake,hapo ndipo Urusi anapompiga BAO.wote mnajua kuhusu kujitanua kijeshi Kwa USA kumzumguka Urusi,sio mpango wa kawaida Bali ni mpango dhidi ya Urusi,Urusi hushitukia na hutibua mipango hiyo.
Mfano mmoja,kwa wafuatiliaji wazuri wa mambo haya,nadhani wengi mnakumbuka jinsi USA alivyokua anatamani kuweka mfumo wa rada Romania na mfumo wa kudungua makombora Cheks au Poland kama sijakosea,kwa kisingizio kua ni kuilinda ulaya dhidi ya mataifa ovu ya Iran na Korea Kaskazini.dunia ikabaki inashangaa,mbona hakuna bifu kati ya Iran na ulaya?,au KK na ulaya?
Urusi walipinga kwa nguvu sana na kutoa vitishi juu,hatimae USA akaachana na mpango ule.
Kusema ukweli mpango ule ulikua ni juu ya kuiangamiza Urusi.na huenda pengine yalikua ni maandalizi ya vita kama hizi.urusi alijua fika Nia ovu hiyo na kutoa vitisho vikali sana kwa USA na nchi zitakazo wekewa mitambo hiyo kua zitakua shabaha namba moja.
Kwa kuamalizia ni kwamba Urusi alijiandaa kwa Kila kitu kijeshi na kiuchumi,
hata wakichangishana silaha na wao pia zianpungua,
NATO waliingia upande wa Ukraine,Kuna nchi zitaingia upande wa Urusi,
Urusi aloshajua janja ya USA siku nyingi kumchonganisha na Ukraine ili akipigana Nae amchoshe kijeshi na kiuchumi,kilichotokea wanachoka wao,
Walitegemea kukamata.Assets za Warusi Warusi wangemfanyia fujo Putin lkn utulivu umetamalaki Urusi.
Sehemu kubwa ya Dunia haijamlaumu urusi.Latin Amerika,Afrika,middle east,far east na Asia hawana shida na Urusi.