Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Watu mnashangilia msaada wa tanks as if ndio ushindi!Tatizo mnasahau game changer himars ambapo zilishangiliwa hivi hivi!
Muwe na kumbukumbu basi Ili walau mbalance kelele zenu hizi!
Na zikienda zisipofua dafu mtajizima data!Baadaye zikitolewa silaha nyingine mtakuja na kelele kama hizi hizi!
 

Mzee kuna aliyesema mfumo mbovu?! Hilo wewe ndiye umezungumza!!! Tunachojiuliza inakuaje wale ambao kila siku wanazisimanga nchi za US & Europe na West kiujumla ndio haohao wanapeleka watoto wao wakasome na kuishi kwenye hizohizo nchi ambazo kila siku wanasema ni mbaya!!!!! Kwanini wasiwaache hapohapo Urusi,wakasoma hapohapo.
 
Himers zilileta mabadiliko makubwa ktk vita na Russia akafurushwa ktk miji kadhaa.

Na sasa hayo magari ya kivita na vifaru yanayotolewa pamoja na zana zingine na Himers zikiwepo basi vita vinakua virahisi sn
 

Punguza hasira hata Urusi ilisaidiwa vifaa na Marekani wakati wa WWII, Marekani ni Baba mwenye huruma[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu msipende kujisahaulisha,Himars si juzi hapa hata mwezi haujaisha zimechoma na kuzika wanajeshi wenu karibu 400!!!! AD zenu zikashindwa kudaka vikombora sita tu vya Himars [emoji16]
 
Western propaganda now we know who is Russia
 
Where have you got this?
 
Msemaji wa Urusi Dmitry Peskov ametoa maoni yake juu ya uwezekano wa kupelekwa wa vifaru vya Abrams vya Marekani kwenda Ukraine, akisema kwamba vitateketezwa kama vifaru vingine vyovyote.

"Ni kwamba tu kwa upande wa kiteknolojia, huu ni mpango ulioshindwa, na muhimu zaidi ni kukadiria wazi uwezo ambao itaongeza kwa vikosi vya kijeshi vya Ukraine. Huu ni udanganyifu mwingine mbaya sana," aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Kulingana na yeye, maoni ya mamlaka ya Urusi yanashirikishwa wataalam, lakini hawakufafanua ni nani hasa.

Awali, Peskov alizungumza hivyo hivyo juu ya kupelekwa kwa vifaru "Leopards" vya Ujerumani huko Kyiv.

"Tumesema mara kwa mara kwamba vifaa kama hivyo havitabadilisha chochote, lakini vitaongeza matatizo kwa Ukraine na kwa watu wa Ukraine," alisema wiki iliyopita.

Wataalamu wa nchi za Magharibi, wakati huo huo, wanaamini kwamba vifaru vizito vya Ujerumani na Marekani, pamoja na Challenger-2 ya Uingereza, uhamisho ambao London ilithibitisha katikati ya Januari, itaruhusu Vikosi vya Wanajeshi kuachana na kudhibiti wanajeshi wa Urusi hadi kuanza kuwafukuza nje ya Ukraine.
 
Hebu tueleze,Huwa wanazisimanga vipi?Maana tusiwe tunajadili kitu ambacho hatukielewi!
Nitajie mmoja aliyesimanga mfumo wa elimu wa nchi za west halafu akapeleka mtoto kusoma!
Nashukuru tumemaliza mjadala juu ya mfumo wa elimu wa Russia!
 
Himers zilileta mabadiliko makubwa ktk vita na Russia akafurushwa ktk miji kadhaa.

Na sasa hayo magari ya kivita na vifaru yanayotolewa pamoja na zana zingine na Himers zikiwepo basi vita vinakua virahisi sn
Ok sawa,tunasubiri hivyo vita virahisi Kwa Ukraine!
Watoaji wa silaha wanaandaa bajeti ya miaka mitano,pro NATO wa nanjilinji anasema baada ya tanks hizo kufika vita vitakuwa virahisi😀😀!
 
Peskov: Vifaru vya Marekani "Abrams" 'vitaunguzwa kama vifaru vingine vyovyote'

Msemaji wa Urusi Dmitry Peskov ametoa maoni yake juu ya uwezekano wa kupelekwa wa vifaru vya Abrams vya Marekani kwenda Ukraine, akisema kwamba vitateketezwa kama vifaru vingine vyovyote.

"Ni kwamba tu kwa upande wa kiteknolojia, huu ni mpango ulioshindwa, na muhimu zaidi ni kukadiria wazi uwezo ambao itaongeza kwa vikosi vya kijeshi vya Ukraine. Huu ni udanganyifu mwingine mbaya sana," aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Kulingana na yeye, maoni ya mamlaka ya Urusi yanashirikishwa wataalam, lakini hawakufafanua ni nani hasa.

Awali, Peskov alizungumza hivyo hivyo juu ya kupelekwa kwa vifaru "Leopards" vya Ujerumani huko Kyiv.

"Tumesema mara kwa mara kwamba vifaa kama hivyo havitabadilisha chochote, lakini vitaongeza matatizo kwa Ukraine na kwa watu wa Ukraine," alisema wiki iliyopita.

Wataalamu wa nchi za Magharibi, wakati huo huo, wanaamini kwamba vifaru vizito vya Ujerumani na Marekani, pamoja na Challenger-2 ya Uingereza, uhamisho ambao London ilithibitisha katikati ya Januari, itaruhusu Vikosi vya Wanajeshi kuachana na kudhibiti wanajeshi wa Urusi hadi kuanza kuwafukuza nje ya Ukraine
 
Kwamba mtu akichoma Biblia nayenyewe fresh tu yani.

Najaribu nikuelewe ila wapi, nakosa tathmini ya aina yako.
Ukitaka we choma tu wala hutaona kelele sababu Mungu wetu mkubwa.
Hicho kikaratasi chenu kikichomwa mnateseka sana
 
Punguza hasira hata Urusi ilisaidiwa vifaa na Marekani wakati wa WWII, Marekani ni Baba mwenye huruma[emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 2495308
Tueleze,hiyo vita haikumuhusu US?US alichangia silaha,Russia akatoa man power!Unajua walikufa wamarekani wangapi dhidi ya warusi wangapi?
Mnapoleta hoja Huwa mnafikiri kweli?
 
Hebu tueleze,Huwa wanazisimanga vipi?Maana tusiwe tunajadili kitu ambacho hatukielewi!
Nitajie mmoja aliyesimanga mfumo wa elimu wa nchi za west halafu akapeleka mtoto kusoma!
Nashukuru tumemaliza mjadala juu ya mfumo wa elimu wa Russia!
Nadhani hujaelewa! Rudia tena kusoma nilichoandika
 
Halafu msipende kujisahaulisha,Himars si juzi hapa hata mwezi haujaisha zimechoma na kuzika wanajeshi wenu karibu 400!!!! AD zenu zikashindwa kudaka vikombora sita tu vya Himars [emoji16]
Kwahiyo himars zinafanya kazi mpaka watu wakusanyike kwenye sherehe?😀,Battle field vipi?
Halafu hata hiyo figure ni questionable maana Urusi kasema hivi,huku Ukraine anasema hivi?Nani wa kuaminika?
 
Tueleze,hiyo vita haikumuhusu US?US alichangia silaha,Russia akatoa man power!Unajua walikufa wamarekani wangapi dhidi ya warusi wangapi?
Mnapoleta hoja Huwa mnafikiri kweli?
Kwani kule Ukraine US kapeleka manpower,si anapeleka silaha tu,tena hata sio silaha za maana kihivyo kama ambazo USSR ilisaidiwa. USSR ilipewa karibu ndege 10,000. Ukraine Leo haijapewa hata ndege moja,hata long range missiles hawajapewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…