mkuu tulia! Hii lugha ya ushoga
1) haina kazi kabisa katika habari hizo za vita. Marafiki wa Putin wanataka tu kuchochea watu dhidi ya Ukraine na "magharibi" kwa kudai eti hao wanatawaliwa na "mashoga" hivyo watu wazuri labda wanapaswa kuwapinga. Bila kujali ukweli au hali halisi.
2) hao wanaoitwa "mashoga" wako kila nchi ya dunia, hata TZ au wapi. Wanaweza kujificha nchi fulani au kutembea wazi nchi nyingine kutegemeana na mazingira. Wako takriban asilima 2-3 za binadamu kote. Hivyo hao ni sehemu tofauti ya uumbaji wa Mungu, sawa na watu waliozaliwa vipofu, wenye mguu mmoja, au wanaokosa mkono tangu kuzaliwa. Wasipoudhi watu wengine hawana madhara wanastahili heshima kama kila binadamu (na sawa na watu walio "kawaida" wanapaswa kudharauliwa na kuadhibiwa wakishambulia watoto au watu wasioweza kuwazuia)
3) Kwa hiyo bila shaka washoga Warusi wanaonekana kwa sababu Zanzibar siku hizi ni kati ya mahali pachache dunianini ambako Warusi wanaweza kufika. Kati wa watalii 1000 lazima wako 20-40 na kwa sababu Zanzibar tabia hizo zinafichwa, basi wanaonekana sana!
Ila usikate tamaa, zile 2-3% za washoga Warusi si tofauti na umati huohuo wa Watanzania, Wakongo, Waingereza, Waafrika Kusini au Waukraine.