triga
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 1,029
- 5,712
Tupo pamoja,safi,
angalau upo wewe unayekuja na fact kuliko huyo jamaa niliye m'quote'. Kaja na taarifa ya uwongo kutetea na wenzake wenye mahaba mbele wamemsapoti.
binafsi hufuatilia taarifa toka vyanzo vyote west na east. Most of russian media ni state-owned.
Media huru zililazimika kufunga shughuli baada ya ile sheria ya march.
je uliwahi kusikia maandamano ya ndani ya urusi kupitia rt au tass?
uchumi wa urusi ume decline, je umesikia cost of living crisis kupitia hizo media kama unavyosikia crisis ndani ya western?
kulikuwa na anti war protest ndani ya urusi,je ulipata habari hizo via rt or tass?
Je hii inamaanisha hali ndani ya urusi ni shwari kabisa?
hiyo ya kutoa resource kutoka sector nyingine ni nadharia kweli kwa sababu hatujui kabisa yanayoendelea ndani ya urusi kwa sababu hakuna uhuru wa media.
-sawa mfumo wa swift umezuiwa lakini kama bado unaweza kuendelea kufanya biashara kama anavyouza mbolea afrika kwa nini asiuze na mafuta?
Idea ya Freedom of press ni mtambuka. Inategemea unaangalia kutoka angle ipi. Mm naamini hakuna media ambayo ni walau 60% free. Ni either inasave purpose kwa maslahi ya serikali, vikundi vya watu fulani wenye mamlaka nyuma ya mamlaka tunazozijua na agenda fulani, corporations, etc.
Kama ambavyo Russia wanaficha maandamano ya watu wao ndivyo west pia wanaficha maandamano ya watu wao wanaopinga NATO na vita! Baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa na mtizamo tofauti kuhusu hii saga vilifungiwa huko west pia kwenye mitandao yao ya kijamii.
Hakuna serikali duniani itayoruhusu habari mbaya isiyozitaka ziachiwe kwa public kwa kigezo cha uhuru wa habari. Mifano ipo mingi ya kina Assange na wiki leaks.
My point exactly ni kwamba vikwazo havijafua dafu na mfano mzuri ni huo wa swift. haumfungii mtu Swift unless una lengo la kumcripple asifanye biashara za kimataifa. Otherwise kwa nini umfungie Swift ilhali bado unampa nafasi ya kutrade international!? Ukiona mtu kafungiwa Swift lkn bado kwenye international trade yupo jua basi hiyo njia ya kumfungia swift imefeli/haijazaa matunda! Hao wafanyabuashara wa TZ walioagiza hiyo mbolea wameilipia kwa namna gani ikiwa swift urusi haifanyi kazi!? Au walibeba pesa wakapeleka au wamepewa bure!? Urusi ametafuta namna za kubypass hicho kikwazo cha swift na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Huo ni mfano mmojawapo unaoonesha namna vikwazo (vyote) vilivyobuma. Walitaka kuisusia gesi lkn Ameuza gesi zaidi, wamesusia mafuta lkn bado anayauza, wameweka price cap lkn bado anauza kwa bei yake, wamemfungia swift lkn bado anafanya biashara kimataifa, walitaka watu wamtenge na kumsusa lkn ndio kwanza kina Wang Yi wanasema uhusiano umezidi, walifunga makampuni yao yamechukuliwa na warusi nk. Nk.
Tukisema vikwazo vimebuma hatumaanishi havikuwa na impact kbs bali havikuwa na impact kusudiwa walau hata kwa nusu.