Ukraine ya wapi unayoizungumzia Ndugu yetu???!!! Yaani mpaka sasa bado umeng'ang'ania fikra mgando za kwamba eti Ukraine inapambana na Russia??!! Hutaki kuukubali ukweli kuwa Russia inapambana na nchi 54 duniani? Yaani Nchi zote za NATO zinapambana na Russia halafu kuna nchi nyingine kama Australia, New Zealand na kadhalika yaani zote hizo jumla yake ni 54......Yaani zinapambana kijeshi, kiuchumi, kijamii, kiuandashi wa habari, kipropaganda (yaani west wameingia kwenye mitandao yote ya kijamii duniani na kwenye mainstream media kusambaza propaganda ) na kadhalika. Yaani Russia, dude kubwa, bado limesimama tu na linaendelea kusonga mbele huku maelfu ya askari wa Ukraine na wale wa NATO (ambao wanapambana kwa kificho au isivyo rasmi) wakiendelea kuteketea. Zele leo analia kwa nguvu kuwa Russia inaharibu kila kitu waliko manazi na wapinga utu. Kilichobaki ni kwa NATO kuingia rasmi mzigoni na kuteketezwa kimoja na kuwa mwisho wa enzi.