Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

😀 😀 😀 😀 😀 Alpha Squad kiboko ya magaidi
Urusi Kuna units za aina nyingi sana za namna hii.
Wapo Hadi wanaoitwa "frogmen"
Hawa vurugu zao ni ndani ya maji TU,shughuli zao sio za kitoto.

Russian Frogmen.

(spetsnaz) unit of the Russian Naval Infantry, trained to conduct land and sea operations behind enemy lines, and to conduct underwater combat, mining and clearance diving.
 
Hahahahahah US hatoboi
 
Muuza nishati ya mkaa na kuni ndo anaweza kuishiwa pesa sio petrol na gas
Mkuu hii tutaona. Swali la kwanza ni, je Mrusi anaweza kuendeleza kiwango chake cha uzalishaji baada ya kuondoka kwa makampuni ya magharibi? Maana Urusi ilikaribisha makampuni hayo (hasa BP, Shell, Wintershall Dea, ExxonMobil, TotalEnergies, Equinor, OMV, na Trafigura) kwa sababu vyanzo vyake vya awali vinapungua na kufungua vyanzo vipya katika kaskazini (eneo gumu penye baridi chini ya 0 muda wote ndani ya ardhi) kunahitaji pesa na tekinolojia za pekee. Makampuni yote ya nje yameondoka.
HAdi sasa Rosneft (kampuni kubwa ya Kirusi, ilikuwa 20% mkononi mwa BP) iliuza ndani ya Urusi kwa bei nafuu ikiweza kupunguza bei kutokana na faida zake katika biashara na Ulaya. Ila soko la Ulaya limeenda halitarudi.
Watafanyeje?
Pia, ilhali mafuta ghafi inaweza kusafirishwa kwa meli, gesi inategemea hasa mabomba. (isipokuwa ukiwekea pesa nyingi kwa viwanda vya kubadilisha gesi ghafi kuwa LPG, pia hakuna meli nyingi za LPG kama za mafuta). Kwa hiyo: Urusi haiwezi kuuza gesi yote ilyouza Ulaya kwa China, mabomba hayatoshi.
Kwa hiyo si ajabu hata mtajiri kama Deripaska (aliyesimama upande wa Putin) anaonya kuhusu matatizo mwaka ujao....

Basi tutaona, ila usiseme haiwezekani!
(Haiwezekani walisema marafiki wengi wa Urusi kabla ya Putin kuanza vita.....)
 
Urussi mwisho wa siku ni lazima amtwange USA tu. Bila kufanya hivyo maisha yatakuwa magumu sana. Kumpiga USA ni akili tu amfute kabisa kwenye ukiranja maana ni sawa na mwanamke mchawi na mnafiki anaechonganisha watu bila sababu huku akitaka kuonekana mwema.
 
Mkuu unamaanisha nini? Kumtwanga kwa namna gani? Kumpiga vipi? Kiuchumi ? Kijeshi ????
 
Mkuu unamaanisha nini? Kumtwanga kwa namna gani? Kumpiga vipi? Kiuchumi ? Kijeshi ????
Kivyovyote vile lazma wamchangie hata ikibidi wao na China wamkung'ute wammalize kabisa. Amekosa ustaarabu wa kuishi na nchi zingine. Yeye sikuzote ndo chanzo cha vurugu na kero duniani.

USA akishadhoofishwa akawa mdogo kama piritoni utaona kama hao anaowaona washirika wake watabaki nae. Wanaishi nae kinafiki tu ila kimsingi hawamfagilii.
 
Hapo ndio Unajiuliza NATO Generals ndio akili zao za kufanya assessments zipo za namna hiyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…