Mmmh kawaida kutizama kitu kimoja kila mtu akawa na uelewa wake kulingana na kile ambacho tayar anakifaham juu ya kile alichokiona.
Ngoja nijaribu kufupisha kwa paragraph 4 ama 5 ikizidi sana unisamehe kwa maelezo mengi ila zaidi nitakisema kile unachowaza ndicho.
Foreign exchange ni free market haiko under any government ya nchi yoooooyote duniani. It's market itself that determines rate ya pesa husika kulingana na demand and supply yake sokoni. Hil la kwanza lishike....
Pili ndani ya Forex as nilivyosema mwanzo kuna kitu inaitwa trade pair. Zipo kama hivi lel me screen shot some ya hizo trade pair.
View attachment 2561308
That way ndivyo Exchange hufanyika, I mean one currency to another... kwa kukuuza na kununua.
Conditions pekee ya scenario kama unayo izungumzia zitatokea endapo kutakua na mfano wa mambo kama haya...
1. Bank husika haina ile fedha unayo ihitaji.
Kwa mfano naenda bank kama TPB, nahitaji kutuma "Angolan Kwanza" kwenda Angola. So kama TPB bank on their reserves hawana hii pesa ya Angola itawabidi watumie mbadala kama huo unaouzungumzia na sio lazima iwe dollar ni pesa yoyote iliyo kwenye reserves yao ambayo pia iko available sehem inakohitaji kwenda.
Inaweza ikatumika pound, euro n.k watakayoona ina faida kwao kwa wakati huo kulingana na rates zilizopo.
Lakini endapo kama Bank husika inakua na reserves ya pesa husika unayo ihtaji basi haitakua na uhitaji wa kuibadilisha kwanza to X ndio iende kua Z.
Mfano kama unataka Canadian dollar na bank husika wanayo hiyo pesa basi itatumwa moja kwa moja kwa kutumia rate za TSH/CAD directly.
Mfumo wa pesa ndivyo unavyofanya kazi kwa float, duniani hakuna nchi iliyo na reserves ya 200 currencies kutoka nchi zote duniani. Ndio maana unaona kile unachokiona kikifanyika... Na hapo ni if and only if bank husika inakua haina currency husika.
Hivyo basi kwa exchanges mfano kama KES, UGX, EURO, British Pound n.k mbali na USD hizi kwa bongo hufanyika directly wala dollar haihusiki kwasabab 'floats' ya hizo currency bank nyingi wako nazo. Exception ipo kwa currencies ambazo banks hazina kwenye reserves zao.
Condition ya pili ya situation unayoizungumzia ipo kibiashara zaidi.
Kwa mfano labda unakuta TSH imeshuka thaman against Dollar au any other currency. Af mhusika anayehitaji mathalan currency ake ipo strong against dollar au any other currency kwa mda huo. Ndio atahitaji kifanyike hicho unachokizungumzia hapo no matter trade pair husika ipo au haipo.
Atataka first uibadil yako to the strongest agaisnt yako kwa wakati huo ambapo utaingia gharama zaidi. Kisha yeye kuibadilisha ile strongest kwako ambayo n week kwake kwa bei ya chini hivo kupata kingi zaidi.
Kama mwanzo ilikua ni ye apate 200 kwa direct exchange basi anapata 250 kwa indirect exchanges.
I can agree with you kwa jicho jepesi kua ni ngumu ila kwa jicho pana inawezekana saaana tu. Nchi nyingi zilikua na hadi sasa zimejivika utumwa wa aina wake wa kuhifadhi pesa za hawa wehu kama reserves currencies. Ukitembelea banks nyingi utakuta zina USD, EURO, POUND, CAS, YEN, YUEN n.k yani zile top notch.
Lakini kila kitu kina sababu na siku sababu ikiondoka ndio mwanzo wa kitu husika kutoweka.
Hii safari ya kila day tunasikia bilateral agreements zikifanyika baina ya nchi na nchi ndio mwanzo wa kumuondoa dalal wa kati.
Asante kwa kuuzingatia mfano wa EU na Euro yao,
Umoja huo una nchi zaidi ya 27, kila nchi ilikua ina currency yao. Mfano German hadi 2002 alikua akitumia Deutsche Mark later akaingia EURO mazima. Poland kuna Polish Zloty, ambayo hadi sasa wanaitumia nje ya Euro. Tangu kuanzishwa kwa Euro kuna zile zilzo ditch currencies zao za awal mazima na kuna zile ambazo bado wanazitumia.
It has been 24 years sasa, na huenda bila ujio wa pesa ile na ukuaji wa uchumi kwa Asia huenda leo hii kusingekua na currency nyingine yoyote tofauti na USD.
Mwisho tu nirudie nilichokisema awali, once sababu ya pesa hizo kujazana hazina ikitoweka kitakachofata ni [emoji706][emoji706][emoji706].
Kibaya zaidi hizi currencies za hawa washenzi haziko pegged to anything... Ziko solely zategemea demand yake sokoni. As demand goes off the chart kwa supply iliyopo thaman zake inaenda zinashuka.
Last year nakumbuka niliwah toa mfano enzi zile thaman ya Euro against Tsh inavyoporomoka. Kutoka around 2700+ iliposhuka hadi kua almost sawa na dollar. Anguko la over 10% in Values ikiwa na maana ya kama mtu alitumia Mil 100 Tsh kuiweka akiba in Euro basi leo hii akihitaji pesa yake kwa rates zilizopo basi hatopata ile Mil 100 bali less than 90Mil Tsh kwasabab ya kuporomoka thaman Euro against Tsh.
Kama hiyo ni just Mil 100 tu kuna upotevu wa zaidi ya Mil 10 je National reserves wamepoteza kiasi gani?????
Ukiona na uchawa wetu wote tunaamua kuingia agreement na nchi kama India kufanya bilateral trade kwa kutumia currency zetu wenyewe ujue hali ni tete ingawa as a country hutokaa usikie serikali wanasema hivi na vile maana kutazuka tafran ya aina ake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Na hapo hatutotumia dollar kwa biashara kati ya TZ na India ila haina maana ya kujitoa kwenye SWIFT system ambayo unahisi transaction zote within ni lazima ziwe kwa dollar.
Any way bro Triga nisikuchoshe, nilisema paragraph 4 hii sijui naandika ya ngapi.