Labda nikuombe ufafanuzi how does it work technically kama mimi nina account ya pesa za madafu NBC nataka kumlipa mchina mwenye akaunti ya yuan China merchant bank wakati hizi bank mbili hazina kbs uhusiano wa kibiashara. Bear in mind swift is not a real transfer of money but messages.
Usiwaze bro,
Dah mfumo wa pesa upo complicated ila ukifahamika ni mwepesi kueleweka.
Kwanza nianze kwa kusema walio na dhamana ya Fedha ya nchi husika ni Central Government kupitia Central bank. Hizi banks zingine zooote zipo chini ya Central bank ambayo inapima uingiaji na utokaji wa fedha nchini. Wao kama akina nani? Of course as regulators! So kwa hapo it's not about NBC na certain bank in China bali its about Tanzania na China.
And how does that happen technically kama ulivyo uliza tuishereheshe kwa namna hii.
Bank zote zina account Bank Kuu amean BoT. Ambapo ni huko ndio hukabidhiwa hii kitu tunaita "float' ama "electronic money"... Hii floats inaweza kua at the currencies of their desires.
Most banks za hapa TZ nimeona wamehold into currencies za EA(UGX, KES, Rwanda, Burundi n.k) vile vile na popular currency kama tulizozizoea like USD, Euro, Pound Yen na Yuan n.k
So when a customer comes na akahitaji lel say kama ulivyouliza Tsh kwenda China ambako kuna Yuan. Endapo kama bank hiyo ambayo ni NBC ina floats za Chinese Yuan. Itafanya direct transfer ya moja kwa moja kwa kutumia rates za TSH/CNY.
Ila kama haitakua na floats ya Yuan, basi itatumia mbadala ule unaofikria wewe... kwamba kwa safari ya AC wanapitia AB then BC kwasababu means ya wao kupitia AC hawana.
Kama bado tuzidishe mifano kwa kutumia mitandao ya sim tuliyonayo hapa TZ.
Qibsyl anatumia mtandao wa TIGO anahitaji kumtumia pesa
triga ambae anatumia mtandao wa Airtel. Lakini alipo
Qibsyl kunapatikana Agents wa TIGO na Vodacom tu pia aliko
triga kuna wakala wa Airtel na Vodacom tu.
So ambacho atakifanya
Qibsyl ni kuhamisha fedha zake kutoka TIGO kuziweka Voda then azitume kwa wakala wa Voda aliye kwa Triga kisha wakala yule afanye kuzihamisha kwenye Airtel ili Triga aweze kuzipata.
Huo mfano ndio scenario niliyoisema juu ya how comes dollar ama pesa nyingine inakuja kutumika katkati baina ya intl transfer betn two countries.
Na labda tufafanue deep how hizi bilateral agreements zinavyofanya kazi. Ni nchi zinaingia makubaliano kati yao ya each one of them ku'acquire currency ya mwenzie... kwamba country A anakua na float ya Currency kutoka country B and Vice versa so whenever transaction between wao ikihitajika basi kuna kua hakuna uhitaji wa kupita Mtwara kwenda Morogoro ukitokea Tanga.
Leo hii its possible Hata kwa Mobile money kutuma pesa kwenda Kenya Uganda Rwanda n.k kwa mfumo kama huo, kumbuka kwa kila international transfer cha kwanza kinachofanyika ni ununuzi kisha transfer ndio ifanyike.
Unataka kutuma 2000Tsh kenya, inaanza exchange first ambayo mtandao husika wataifanya on your behalf, since watakua na floats za KES watakachokifanya ni kukuuzia kwa rate itakayo kua sokoni kwa mda huo. Then watakuonesha na charge of transfer kisha tukio linafanyika.
Ambapo kinachoenda kule ni KES sio TSH.
Na kwa kua mifumo ni ile ile tunaweza kuingia mitaani kwa mawakala ambao tunakutana nao kila siku kuchukua mifano. Wakala anaenda na pesa taslim kwa agent mkuu. Kisha anapewa floats "E Money" then ndipo anakua na uwezo wa yeye kumuekea mtu Pesa. Hiyo aina ya pesa anayoweka kama floats ndio aina ya pesa anayoweza kuifanyia miamala.
Kama ni USD basi atafanya kwa USD, kama ni Kwacha basi atafanya kwa Kwacha... na kama ikihitajika ambayo hana basi ataangalia best option kwake ili aweze kutimiza hitaji lililo mbele yake.
Na of course hatutafikia hatua ya kutokomeza kabisa matumizi ya teuzi moja ya currency kutumika na wote. Kama nilivyosema awali sio rahisi kwa nchi kua na all global currencies kwenye reserves zao kwa lengo la kutumia each kwa kila taifa linalofanya nalo biashara.
Standard is needed for convenience. Jana kama sikosei nilitoa historia ilivyokua kabla ya US dollar, ilikiwa ni british pound. Tukaona effects za WW1 na WW2 na kurise kwa dollar kuanzia kwa Bretton Woods Agreement ya 1944, Kurise kwa Petro dollar n.k hadi kua na hali hii iliyopo leo.
So hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, hata enzi zile ambapo British Pound ilikua kama Global Currency nobody thought kama ingekuja kutoweka na kuwa replaced na USD.
In late 1960+ ilikua ni kama ufahari kwa watu kua na reserves ya US dollar kuliko hata vyenye thaman like Gold and so... Kitu ambacho hadi sasa kimefanikiwa kupandikizwa katika mind za walio wengi.
Kilichokosewa ama sijui kimefanywa makusudi au ndio vile hulka za kibinadam ukizidiwa sifa unaanza kuyapuyanga ni hiki ambacho kimeanza kufanyika toka 2014. Weaponizing dollar, yan USD kutumika vibaya hasa kuwekeana restrictions kwenye uchumi hivyo kupelekea different countries kuanza kusakua alternative na ndio hicho tukionacho kwa sasa kimeshamiri.
Hizi bilateral agreements daima tutaziona kwa nchi ambazo zinafanya biashara baina yao kwa wingi ambapo itakua ni profitability. Later tutegemee kuanzishwa kwa bloc currency, ambayo haitakua inamilikiwa na nchi flan wa flani bali umoja husika. Lel say BRICS ambayo itatumika na wana chama husika.
Ama pia wanachama hao wanaweza ku-opt pia kutrade with other nations outside the bloc lwa pesa hiyo nje ya pesa zao za Taifa. Mda ni mwalim mzuri, tutaona mengi tu. Kilichokua kinasumbua mwanzo ilikua ni ile fear waliyopandikizwa mataifa mengi na viongozi wao kufanyiwa mapinduzi kama hayo ambayo tumekwisha yaona sina haja ya kuyataja.
Nizidi kukumbusha kwa data, miaka ya 1990+ Global share ya dollar ilifikia hadi around 90%, Toka kwa kuanzishwa kwa Euro kuliishusha hadi around 71% na 2021 ilikua imeshuka zaidi hadi 57% na kwa hii pace iliyopo nisiseme mengi.
I don't know lkn nakumbuka kuna kitu niliwahi kusoma nafkiri hapahapa jf kuhusu brexit, great thinkers kule kuna baadhi ya wataalamu walidai kujiondoa kwa uk kwenye eu ni mpango wa kuipungiza nguvu eu na euro ndio maana nikakuuliza lile swali. Pengine kweli Euro ilikuwa tishio kwa usd na us. Kama una lolote kuhusu hilo hebu jazia hapo
Kabla ya kuanzishwa kwa Euro mnamo 1999, pesa iliyokua na nguvu Europe ilikua british Pound. Ila baada ya kuanzishwa kwa sarafu ya umoja huo wa ulaya. Euro ndio ikawa kama ina nguvu over all currencies zilizokuepo. Hapo ndio utaona kuna baadhi kama Austria, Germany to mention but few wali discontinue kabisa matumizi ya pesa zilizo kuepo na officially kutumia EURO.
Kuhusu BREXIT kila mtu ana yake kulingana na wingi wa taarifa alizo nazo akilin mwake. So sijui nikubali ama nikatae kwa hilo ulisemalo. Ila as far as I know brexit ina mahusiano mapana na hiki kinachoendelea leo pale Ukraine.
Moja ya target kubwa ya mgogoro huu ambao ulikua ukisukwa miaka nenda rudi sio kwa Russia tu bali ilikua ni kupiga ndege wengi kwa jiwe moja.
Post itakua ndefu ila acha niendelee kutype tupeane mitizamo mipya.
US and UK lao ni moja, ndani ya Europe Germany ni Pasua kichwa wa US. So kuiteketeza Europe ni kuiharibu Germany so as wanaendelea kua weak na dependant wa Zee la kaskazini. At that time kwa vyovyote vile UK ilibidi atoke kwenye jahazi linalozama il maji yakizidi asiwe miongoni mwa watakao hangaika.
Kuiingiza Europe katika machafuko ni moja katika mipango mahsus za kuiharibu Euro, na Europe kwa ujumla. Lengo haswa ikiwa ni kuimarisha Interest za US. Na njia shortcut ya kuiharibu Europe ni kuuharibu uchumi wa Germany.
So hapo ndio ujiulize kwanini Germany anaandamwa sana tena kwa kushinikizwa kufanya vitu ambavyo vinauathiri uchumi wake kwa jina la Ukraine? Energy ndio backbone ya Uchumi wa taifa lolote lile, katika wote ye ndie mmufaika nambari moja wa cheap gas kutoka Russia, Kushinikizwa kutengana nae kuna maanisha nini? Ok, Who bombed nord streams? Anamtia hasara Russia au inaharibiwa Germany? Na nini outcome ya kuanguka kwa uchumi wa Germany ndani ya Taifa la Ulaya?
So ile solidarity unayoona wanalazimishana leo hii ifanywe ndani ya mataifa hayo ndio ilikua main thing, main agenda ya Brexit nyuma ya pazia. They know much nn mbele kinaenda tokea so wakajiandaa kwalo.
Naandika ila najishtukia post kua ndefu sana. Mwisho niseme as usual, kila mtu hua anaelewa jambo flan kulingana na kile ambacho tayari kwenye kichwa chake kuna taarifa za jambo hilo.
Tunaweza kaa hapa wawili ukawa unatusimulia kuhusu daraja la kigamboni hapo ila imagination yangu na ya mwenzangu zikapishana kutokana na kila mmoja wetu namna gani analjua daraja hilo.