Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

m
Kusema upande ule hauna washirika wakati hawataki upande ule huungwe mkono. Nchi yoyote inayojitokeza kuwa upande ule unapewa sanctions za kumwaga
Ndiyo ujue kuwa huwezi kuweka "Sanctions" kama wewe siyo mbabe dhidi ya unayemwekea hizo "Sanctions". Kwa ivo kama watu hawakai upande wa Urusi ama Uchina wakati wa matatizo, ina maana nchi nyingine zinaona si salama kukaa upande wa Urusi au China zinapokuwa na mzozo na Marekani.
 
Line hipi anayo zungumzia, hivi huyu Blinken wakati mwingine akili zake zikoje - ie anaishi kwenye Dunia gani, yaani Blinken hana hata habari kwamba Taifa kama Uchina, North Korea, Iran na Urusi haziwezi kuendeshwa puta na USA - Dunia siku hizi imebadirika sana sana ki-Geopolitical na US wasipo kuwa makini wakaendeleza vurugu zao kwenye mataifa tajwa hapo juu watamchangia na kumpa kipigo kitakatifu bila ya kujali silaha alizo nazo - watamu-netrualise hata amini macho yake - hivi sasa wanasubiri an opportune time ya kumshughurikia kikamilifu - hawawaze kumuacha hivi hivi bila ya kumchangia maana hawajui kesho atamvamia/chokoza nani baina yao consequently time ya ku-deal naye is now not later - we mwache asombe sombe vifaru vyake vya kizamani sina shaka siku zijazo ataongezea na ndege za kivita nk - Biden yuko obsessed na kumshinda vita Putin kuliko maelezo - Biden anacho sahau ni kwamba Urusi ilisha jipanga siku nyingi jinsi ya kudeal na NATO specifically the USA na safari hii Warusi/Wachina na Korea kasikazini wata hakikisha vita hii inapiganwa nchini Merikani kwenyewe sio Ulaya na far east tu.
 
Urusi anapigana vita hii kwa kutumia misuli (Askari na Mamluki wa Wagner) wakati zama zimebadilika kwa vita kuendeshwa kielektroniki zaidi. Ina maana hata teknolojia ya "Drone" Urusi iko nyuma sana na ndiyo maana wananunua hizo Drone toka Iran.
 
Ndio maana sanctions zinakwenda kupatiwa dawa muda sio mrefu, BRICKS wanakuja na mfumo mwingine wa kibenki ku replace SWIFT ya marekani.

Muda sio mrefu hata vinchi vidogovidogo vitamdindishia mmarekani. Marekani akileta mikwara yake mbuzi ya sanctions, nchi hizo zitaachana na mfumo wa marekani na kuamia mfumo wa BRICKS
 
safari hii Warusi/Wachina na Korea kasikazini wata hakikisha vita hii inapiganwa nchini Merikani kwenyewe sio Ulaya na far east tu.
Haya ni matamanio ambayo hayawezi kutokea hata siku moja. Hizo nchi ulizozitaja si adui wa Marekani bali zinashiriki (Share) kwa pamoja harakati za kuitawala dunia.

Unawazaje Urusi, na Uchina kuishambulia Marekani wakati zinaitegemea kwa chumi zao? Hiyo Korea Kaskazini ni kikaragosi tu cha Uchina haifanyi kitu mpaka iruhusiwe na Uchina!!
 
Hii ni nadharia ambayo kusimama kwake kunaitaka Marekani iruhusu. BRICS bila ya Marekani hakuna nguvu wanayodhania kwamba wanayo!!

Euro ilianzishwa kuipiku Dollar, imefanikiwa kwa kiasi gani!!??
 
Urusi anapigana vita hii kwa kutumia misuli (Askari na Mamluki wa Wagner) wakati zama zimebadilika kwa vita kuendewshwa kielektroniki zIaidi. Ina maana hata teknolojia ya "Drone" urusi iko nyuma sana na ndiyo maana wananunua hizo Drone toka Iran.
Kwamba warusi wasiweze kutengeneza drone lakini wairan waweze?kweli hakuna Team NATO aliyesafi upstairs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…